Ibrahim 14:33
ابراهيموَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ دَآئِبَيْنِ ۖ وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ
Na akawatiishia jua na mwezi vinavyokwenda daima dawamu, na akawatiishia usiku na mchana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akalifanya jua na mwezi kwa manufaa yenu daima dawamu, na akaufanya usiku na mchana kwa manufaa yenu. [33]
[33] Na akalifanya jua na mwezi yakufaeni daima dawamu, kwa mwangaza na maslaha ya mimea na wanyama. Na akajaalia usiku ukufaeni kwa kupumzika na mchana kwa kufanya kazi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Akawadhalilishia nyinyi jua na mwezi, haviachi kutembea kwake, ili maslahi yenu yatimie kwa viwili hivyo. Na akawadhalilishia nyinyi usiku, ili mtulie humo na mpumzike, na mchana ili mtafute fadhila Zake na mpange maisha yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net