Ibrahim 14:3
ابراهيمٱلَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا عَلَى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ فِى ضَلَـٰلٍۭ بَعِيدٍ
Wale wanaoupendelea uhai wa dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wako katika upotovu wa mbali.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wamepotelea mbali. [3]
[3] Hao ndio walio khiari uhai wa duniani kuliko Akhera, na wanawazuia watu wasifuate Sharia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotoa Sharia katika macho ya watu ili wapate kuikataa. Hao ndio wanao elezwa katika yaliyo tajwa kuwa wamepotelea mbali na Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawa wenye kugeuka wasimuamini Allah Mtukufu na wasimfuate Mtume Wake ndio wanaochagua maisha ya dunia yenye kutoweka na wanaacha Akhera yenye kusalia, wanawakataza watu kufuata dini ya Allah Mtukufu na wanaitaka iwe ni njia iliyopotoka ili iafikiane na mapendeleo yao. Hao waliosifiwa kwa sifa hizi wamo ndani ya upotevu wa kutoiona haki, wako mbali na njia zote za uongofu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net