Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 23

Ibrahim 14:23

ابراهيم

وَأُدْخِلَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ ۖ تَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَـٰمٌ

Maana

Na wale walioamini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani yapitayo mito kwa chini yake, wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi. Maamkizi yao humo yatakuwa: Salaam (Amani)!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio amini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani yapitayo mito kati yake, wadumu humo kwa idhini ya Mola wao Mlezi. Maamkio yao humo yatakuwa: Salaam. [23]

[23] Na Akhera wataingizwa wenye kuamini, na wakatenda vitendo vyema, katika Mabustani yanayo pitiwa na mito chini ya majumba yake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na amri yake. Maamkio yao humo kutokana na Malaika ni kufahamisha amani na utulivu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema, watatiwa ndani ya mabustani ya Pepo ambayo chini ya miti yake na majumba yake ya fahari inapita mito. Hawatatoka humo milele, kwa idhini ya Mola wao na uwezo Wake na nguvu Zake. Watasalimiwa humo kwa salamu itokayo kwa Allah Mtukufu, Malaika Zake na Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net