Ibrahim 14:22
ابراهيموَقَالَ ٱلشَّيْطَـٰنُ لَمَّا قُضِىَ ٱلْأَمْرُ إِنَّ ٱللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ ٱلْحَقِّ وَوَعَدتُّكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِىَ عَلَيْكُم مِّن سُلْطَـٰنٍ إِلَّآ أَن دَعَوْتُكُمْ فَٱسْتَجَبْتُمْ لِى ۖ فَلَا تَلُومُونِى وَلُومُوٓا۟ أَنفُسَكُم ۖ مَّآ أَنَا۠ بِمُصْرِخِكُمْ وَمَآ أَنتُم بِمُصْرِخِىَّ ۖ إِنِّى كَفَرْتُ بِمَآ أَشْرَكْتُمُونِ مِن قَبْلُ ۗ إِنَّ ٱلظَّـٰلِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Na shetani atasema itakapokatwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya kweli. Nami niliwaahidi; lakini sikuwatimizia ahadi yangu. Na sikuwa na mamlaka yoyote juu yenu, isipokuwa niliwaita, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikufuru tangu zamani huko kunishirikisha kwenu na Mwenyezi Mungu. Hakika madhalimu wana adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu. [22]
[22] Mwenyezi Mungu atapo pitisha amri yake, ya kuwaneemesha watii'fu, na kuwa adhibu wenye kuasi, Iblisi atawambia wanao mfuata, Hakika Mwenyzi Mungu amekuahidini ahadi ya kweli, kuhusu kufufuliwa na malipo, na ametimiza. Na mimi nimekuahidini ahadi ya uwongo ya kwamba hakuna kufufuliwa wala malipo, na mi mimwekenda kinyume na ahadi yangu. Nami sikuwa na nguvu juu yenu hata nikulazimishieni kunifuata lakini nimekuitieni kwa ushawishi wangu wa upotovu nanyi mukaja mbio kunitii, basi musinilaumu kwa sababu ya ushawishi wangu, na zilaumuni nasfi zenu kwa kuniitikia. Wala mimi hii leo siwakukuokoweni na adhabu, na nyinyi hamuwezi kunioa mimi. Mimi leo nakataa huko kunishirikisha mimi na Mwenyezi mugnu huko duniani mulipokuwa mukinit'ii, kama mtumwa anavyo mti'ii bwana wake. Hakika makafiri watapata adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Shetani atasema baada ya Allah Mtukufu kuamua jambo Lake na kuwahesabu viumbe Vyake, na kuingia watu wa Peponi Peponi na watu wa Motoni Motoni, Allah Mtukufu Aliwaahidi nyinyi ahadi ya kweli ya kufufuliwa na kulipwa, na mimi niliwaahidi ahadi ya urongo kwamba hakuna kufufuliwa wala kulipwa, nikawaendea kinyume na ahadi yangu. Na mimi si kuwa na nguvu zozote za kuwalazimisha kunifuata, wala si kuwa na hoja. Isipokuwa mimi niliwaita kwenye ukafiri na upotevu mkanifuata. Basi msinilaumu, jilaumuni nyinyi wenyewe. Dhambi ni dhambi zenu wenyewe. Mimi si mwenye kuwaokoa na nyinyi si wenye kuniokoa na adhabu ya Allah Mtukufu. Mimi nimejiepusha na jambo la nyinyi kunifanya mimi ni mshirika pamoja na Allah Mtukufu katika kutiiwa ulimwenguni. Hakika madhalimu, katika kuupa mgongo kwao ukweli na kuufuata urongo, watakua na adhabu kali iumizayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net