Yusuf 12:15
يوسففَلَمَّا ذَهَبُوا۟ بِهِۦ وَأَجْمَعُوٓا۟ أَن يَجْعَلُوهُ فِى غَيَـٰبَتِ ٱلْجُبِّ ۚ وَأَوْحَيْنَآ إِلَيْهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَـٰذَا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Basi walipokwenda naye, na wakakubaliana kwamba wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hakika utakujawaambia jambo lao hili, na wala wao hawatambui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao hili, na wala wao hawatambui. [15]
[15] Walipo kwenda naye mbali na baba yake, na wakakubaliana rai yao ya kumtumbukiza ndani ya kisima, walifanya hayo waliyo yaazimia. Sisi tukamtia moyoni mwake Yusuf atulie, na awe na imani ya Mwenyezi Mungu, kuwa bila ya shaka atakuja waeleza haya mambo yao waliyo yapanga na wakayatenda, na wala wao wenyewe hawajui hapo utapo waambia kwamba wewe ndiye Yusuf waliye mfanyia vitimbi, na wakadhani wamekwisha mmaliza na wameepukana naye!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo baba yao akawaachia wawe naye, walipokwenda na yeye na wakaamua kumtupa ndani ya kisima (na wakafanya hivyo) na hapo tukamletea wahyi Yûsuf, «Utawaambia ndugu zako mbeleni kuhusu kitendo chao hiki walichokufanyia na hali wao hawakitambui».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net