Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 14

Yusuf 12:14

يوسف

قَالُوا۟ لَئِنْ أَكَلَهُ ٱلذِّئْبُ وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّآ إِذًا لَّخَـٰسِرُونَ

Maana

Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na ilhali sisi ni kundi lenye nguvu kabisa, basi bila ya shaka sisi tutakuwa tumehasirika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kundi lenye nguvu kabisa, basi bila ya shaka sisi tutakuwa khasarani. [14]

[14] Wakasema: Tunakuapia, akiliwa na mbwa, na hali sisi ni kundi lenye nguvu, basi itakuwa ni fedheha na khasara kwetu! Likitokea hilo unalo liogopa basi sisi tutakuwa tumekhasiri kila linalo pasa kulishughulikia, na kuwa lisitokee. Basi tuwa kwa hayo! Hatutadharau kumlinda, ikiwa hivyo itakuwa tunajipelekea wenyewe kupotea na kupuuza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wakasema ndugu zake Yûsuf kumwambia baba yao, «Ikiwa mbwamwitu atamla na hali sisi ni kikundi chenye nguvu, sisi wakati huo tutakuwa ni wenye kupata hasara, hatuna wema wowote, na hakuna manufaa yoyote yanayotarajiwa kutoka kwetu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net