Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 1

Yusuf 12:1

يوسف

الٓر ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُبِينِ

Maana

Alif Laam Raa.[1] Hizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. [1]

[1] Alif, Lam, Raa. Hizi harufi na mfano wake, zinazo fanya maneno yenu, enyi Waarabu, ndizo hizo hizo zinazo fanya Aya za hichi Kitabu, ambacho ni muujiza unao waemea watu kuuiga. Muujiza ulio wazi unao fafanua kwa kila mwenye kutafuta uwongozi ndani yake, na uwongofu. Na kwa hizi harufi za kutamkika zikasikilizana sauti yake wanazinduliwa watu watanabahi. Basi wasikilize, ijapo kuwa waliwafikiana kuwa wasisikilize.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Alif, Lãm, Rã’. Maneno yametangulia juu ya herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqrah. Hizi ni aya za Kitabu kilichobainika kilicho wazi katika maana yake, mahalalisho yake, maharamisho yake na uongofu wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net