Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 123

Hud 11:123

هود

وَلِلَّهِ غَيْبُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ ٱلْأَمْرُ كُلُّهُۥ فَٱعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَـٰفِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ

Maana

Na ni ya Mwenyezi Mungu tu ghaibu ya mbinguni na ardhi, na mambo yote yatarejeshwa kwake. Basi muabudu Yeye na umtegemee. Na Mola wako Mlezi haghafiliki mbali na yale mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo fichikana katika ardhi na mbingu, na mambo yote yatarejezwa kwake. Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki na yale mnayo yatenda. [123]

[123] Ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kujua yaliyo ya ghaibu katika mbingu na ardhi. Anayajua yatakayo kufikieni, na yatakayo tufikia sisi. Ni kwake Yeye tu yanarejea mambo yote kuendeshwa. Ilivyo kuwa mambo ni hivyo, basi muabudu Mola wako Mlezi peke yake, na mtegemee Yeye, wala usimwogope yeyote isipo kuwa Yeye. Na Mola wako Mlezi haghafiliki kabisa na yote myatendayo, enyi Waumini na makafiri. Na kila mmoja atalipwa hapa duniani na Akhera kwa mujibu anavyo stahiki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni wa Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, ujuzi wa kila kisichoonekana mbinguni na ardhini. Na Kwake yanarejeshwa mambo yote Siku ya Kiyama. Basi muabudu Yeye, ewe Nabii, na umtegemezee mambo yako Kwake. Na Mola wako Hakuwa ni mwenye kughafilika na yale mnayoyafanya ya wema na uovu na Atamlipa kila mtu kwa matendo yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net