Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 16

Hud 11:16

هود

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ إِلَّا ٱلنَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا۟ فِيهَا وَبَـٰطِلٌ مَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Hao ndio ambao hawana kitu katika Akhera isipokuwa Moto, na yataharibika yale waliyoyafanya humo, na yatabatilika yale waliyokuwa wakiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hao ndio ambao hawatakuwa na kitu Akhera ila Moto, na yataharibika waliyo yafanya, na yatapotea bure waliyo kuwa wakiyatenda. [16]

[16] Hao ambao hima yao ni kushughulikia dunia tu, Akhera hawana lao jambo ila adhabu ya Motoni, na kuharibikiwa na yote waliyo yafanya duniani, kwa sababu hawakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hayo wayatendayo pia yatakuwa yameharibika vile vile, kwani kitendo kisicho leta mafanikio ya daima ni kama kwamba hakikupata kuweko.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hao hawana huko Akhera isipokuwa Moto wa Jahanamu wakiadhibika kwa joto lake, na yatawaondokea wao manufaa na yale mema waliyoyatenda, na matendo yao yatatenguka kwa kuwa hayakuwa yanakusudiwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net