Yunus 10:96
يونسإِنَّ ٱلَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ
Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwishathibitika juu yao, hawataamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwisha thibitika juu yao, hawataamini, [96]
[96] Hakika wale iliyo kwisha pita juu yao hukumu ya kuwa wao ni makafiri, kwa kujuulikana inadi yao na chuki zao, hawatoamini hata ukijihangaisha vipi nafsi yako kuwakinaisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika ya wale ambao limethibiti kwao neno la Mola Wako la kuwafukuza kwenye rehema Yake na kuwaadhibu, hawaziamini hoja za Allah Mtukufu, hawaukubali upweke Wake wala hawazifuati sheria Zake kivitendo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net