Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 95

Yunus 10:95

يونس

وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ فَتَكُونَ مِنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ

Maana

Na kamwe usiwe miongoni mwa wale waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, ukawa katika waliohasiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kabisa usiwe miongoni mwa wale wanao zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, usije kuwa katika walio khasiri. [95]

[95] Wala usiwe wewe, wala yeyote katika wanao kufuata, miongoni mwa wanao kadhibisha hoja na Ishara zilio wazi, msije mkaingia khasarani na ghadhabuni, kama hali ya makafiri wasio amini. Na akisemezwa Nabii basi ndio wanasemezwa wote wanao mfuata.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usiwe, wala usiwe, ewe Mtume, ni miongoni mwa waliokanusha hoja za Allah Mtukufu na dalili Zake, ukawa ni katika waliopata hasara ambao Allah Mtukufu Amewakasirikia na wamepata mateso Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net