Al-Faatiha 1:3
الفاتحةٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.[1]
[1] Katika misingi waliyokubaliana juu yake watangulizi wema wa umma huu na maimamu wake ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ana majina na sifa nzuri nzuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu; [3]
[3] Na Yeye ndiye Mwenye rehema ya kudumu, na rehema inatokana naye. Ananeemesha kwa neema zote ndogo na kubwa. (Arrahman ni jina lake Mwenyezi Mungu tu, na hafai mtu kuitwa hivyo.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mwingi wa rehema Ambaye rehema Zake zimewaenea viumbe vyote, Mwenye kuwarehemu Waumini.Na majina mawili haya ni miongoni mwa majina ya Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net