Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 1 · Aya ya 2

Al-Faatiha 1:2

الفاتحة

ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.[1]

[1] Mola Mlezi ni yule anayewalea walimwengu wote. Nao walimwengu ni kila kisichokuwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; [2]

[2] Sifa njema za namna yote na katika kila hali ni za Mwenyezi Mungu pekee. Na tunamsifu Yeye kwa sifa zote kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuviumba viumbe vyote na mwenye kuviangalia na kuvilea. (Neno Rabb, kwa Kiarabu, lina maana ya Ubwana na Ulezi na Utengenezaji. Ndiyo tukatumia Mola Mlezi. Neno Baba lina upungufu.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kila jinsi ya sifa njema ni ya Allah Mtukufu, Mwenye sifa ambazo zote ni za ukamilifu, Mwenye neema za nje na za ndani, za kidini na za kidunia. Na ndani yake kuna amri ya Allah Mtukufu kwa waja Wake wamsifu Yeye kwa kuwa Yeye Ndiye Mstahiki wa kusifiwa Peke Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Faatiha

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net