Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je mnajua ni nani aliyefilisika?" Wakasema: Aliyefilisika kwetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yule asiye na Dirham (pesa) wala mali yoyote. Akasema: "Hakika aliyefilisika katika umma wangu ni yule atakayekuja siku ya Kiyama akiwa na (ibada za) swaumu na swala na zaka, na akaja akiwa kamtukana huyu, na kamzulia machafu huyu, na kala mali ya huyu, na amemwaga damu ya huyu na amempiga huyu, hivyo atapunguziwa huyu kutoka katika mema yake, na huyu katika mema yake, yakimalizika mema yake kabla hajamaliza kulipa anayodaiwa yatachukuliwa kutoka katika makosa yao yatatupwa kwake kisha atatupwa katika moto".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.