Kutoka kwa Maliki bin Ausi bin Hadathani yakuwa yeye alisema: Niligeuka nikasema ni nani anayechenji pesa? Twalha bin Ubaidillah akasema wakati akiwa kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yao wote: Tuonyeshe Dhahabu yako, kisha tuletee, atakapokuja mfanyakazi wetu tutakupa pesa yako, akasema Omari bin Khattwab: Hapana, ni lazima utampa haki yake, au umrejeshee Dhahabu yake, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono".
Pale ambapo Ensaiklopidia ya Hadithi za Mtume Zilizotafsiriwa (HadeethEnc.com) ina maandishi yaleyale ya hadithi, tafsiri yake huonyeshwa chini ya hadithi hiyo pamoja na jina la chanzo. Zimeoanishwa na programu, kwa Kiarabu pekee: maandishi yote ya hadithi katika ensaiklopidia, pamoja na Sahaba anayetajwa ndani yake, ndiyo mwisho wa hadithi hiyo herufi kwa herufi. Hakuna aliyekagua uoanishaji huu, na wahakiki wa Sabīl hawajaichunguza tafsiri. Kiarabu ndiyo maandishi yenyewe.
Maandishi ya Kiarabu, namba, majina ya vitabu na madaraja vinaonyeshwa sawasawa na vilivyo katika seti ya data iliyo wazi (hadith-api). Sabīl bado haijathibitisha usahihi wake wala haki zake, na uhakiki wake wa wanazuoni haujaanza. Hadi hapo, linganisha hadithi na toleo lililochapishwa kabla ya kuitegemea.