Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kusema kumwambia ndugu yake muislamu: Ewe kafiri, basi atakuwa kastahiki neno kafiri mmoja wao, na ikiwa ni kweli kama alivyosema (utamthibitikia), na kama si kweli ukafiri utarejea kwa msemaji aliyesema kumwambia ndugu yake.
- Amekemewa muislamu kusema kumwambia ndugu yake muislamu mambo asiyokuwa nayo, kama sifa ya uovu na ukafiri.
- Tahadhari ya kusema maneno haya machafu, na kwamba msemaji wake yuko katika hatari kubwa atakaposema kumwambia ndugu yake, na lazima kuhifadhi ulimi, na muislamu asizungumze ila kwa elimu.
صحيح البخاري (8/ 26) (6104). صحيح مسلم (1/ 79) (60). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 390). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (9/ 65). النهاية في غريب الحديث والأثر (91).