Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa inatakiwa kuwa hali ya waislamu baadhi yao kwa baadhi katika kupendeleana kheri na kuhurumiana na kusaidizana na kuteteana, na kuudhika kwa yale madhara yanayowafika, kama mfano wa kiwiliwili kimoja, kikiugua kiungo kimoja, mwili mzima unashiriki kwa kukesha na maumivu pia.
- Ni lazima kuziheshimu haki za waislamu na kuhimiza kuwasaidia na kuhurumiana wao kwa wao.
- Ni lazima kwa watu wa imani kuwe na mapenzi na kuteteana.
صحيح البخاري (8/ 10) (6011). صحيح مسلم (4/ 1999) (2586). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 246). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 317). كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (4/ 405). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص173). المعجم الوسيط (1/ 492).