Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Tafsiri za Aya

Hadithi 10

Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَإِذَا طَلَعَتْ فَرَآهَا النَّاسُ آمَنُوا أَجْمَعُونَ، فَذَلِكَ حِينَ: {لاَ يَنْفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِنْ قَبْلُ، أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا} [الأنعام: 158] وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَقَدْ نَشَرَ الرَّجُلاَنِ ثَوْبَهُمَا بَيْنَهُمَا فَلاَ يَتَبَايَعَانِهِ، وَلاَ يَطْوِيَانِهِ، وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَقَدِ انْصَرَفَ الرَّجُلُ بِلَبَنِ لِقْحَتِهِ فَلاَ يَطْعَمُهُ، وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَهُوَ يَلِيطُ حَوْضَهُ فَلاَ يَسْقِي فِيهِ، وَلَتَقُومَنَّ السَّاعَةُ وَقَدْ رَفَعَ أَحَدُكُمْ أُكْلَتَهُ إِلَى فِيهِ فَلاَ يَطْعَمُهَا».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: "Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini, na wakati huo: ((Mtu haitamfaa imani yake ambaye alikuwa hakuamini kabla, au imani yake haikufanya mambo ya kheri:158)) na kwa hakika kitasimama Kiyama na hali yakuwa watu wawili wametandaza nguo zao kwa ajili ya kuuza na kununua na wala hatoweza kuzikunja kutokana na uharaka wa Kiyama, na kwa hakika kitasimama Kiyama ghafla, na kwa hakika ataondoka mtu na maziwa aliyoyachukua kwenye chuchu za mnyama na wala asiwahi kuyanywa, na kitasimama Kiyama wakati anatengeneza josho la kunyweshea na wala asiwahi kunywesheleza, na kwa hakika kitasimama Kiyama na mmmoja wenu atainua tonge kupeleka mdomoni na wala asiweze kula."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa alama kubwa za Kiyama, ni kuchomoza jua kutoka upande wa Magharibi badala ya upande wa Mashariki, na watu wakiliona wataamini wote, Na wakati huo haitomfaa kafiri imani yake, wala hayatomfaa matendo mema wala kutubia. Kisha akatoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Kiyama kitatokea ghafla; Kitatokea na watu watakuwa kwenye hali walizokuwa nazo na wapo kwenye mambo yao ya kimaisha; Na kitasimama Kiyama hali ya kuwa muuzaji na mnunuzi wamesambaza nguo zao lakini hawataweza kuuziana wala hawataweza kuzikunja. Na kitasimama Kiyama na hali ya kuwa mtu ameshika maziwa aliyoyakamua kutoka kwa Ngamia wake na wala hatoweza kuyanywa. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa anatengeneza josho la kunyweshezea wanyama na kulisiriba na wala hatowahi kunywesheleza humo. Na kitasimama Kiyama na mtu atakuwa kainua tonge lake ili kulipeleka kinywani mwake ili ale na wala hatoweza kulila tonge hilo.

Mafunzo
  1. Uislamu na toba hukubalika kabla jua halijatoka upande wa Magharibi.
  2. Kuhimizwa kujiandaa kwa ajili ya Kiyama kwa kuwa na imani na kutenda yaliyo mema; Kwa sababu Kiyama kitakuja ghafla.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 106) (6506)، صحيح مسلم (1/ 137) (157)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (23/ 92).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يُؤْتَى بِالْمَوْتِ كَهَيْئَةِ كَبْشٍ أَمْلَحَ، فَيُنَادِي مُنَادٍ: يَا أَهْلَ الجَنَّةِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ، فَيَقُولُ: هَلْ تَعْرِفُونَ هَذَا؟ فَيَقُولُونَ: نَعَمْ، هَذَا المَوْتُ، وَكُلُّهُمْ قَدْ رَآهُ، ثُمَّ يُنَادِي: يَا أَهْلَ النَّارِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ، فَيَقُولُ: وهَلْ تَعْرِفُونَ هَذَا؟ فَيَقُولُونَ: نَعَمْ، هَذَا المَوْتُ، وَكُلُّهُمْ قَدْ رَآهُ، فَيُذْبَحُ ثُمَّ يَقُولُ: يَا أَهْلَ الجَنَّةِ خُلُودٌ فَلاَ مَوْتَ، وَيَا أَهْلَ النَّارِ خُلُودٌ فَلاَ مَوْتَ، ثُمَّ قَرَأَ: {وَأَنْذِرْهُمْ يَوْمَ الحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ} [مريم: 39]، وَهَؤُلاَءِ فِي غَفْلَةٍ أَهْلُ الدُّنْيَا {وَهُمْ لاَ يُؤْمِنُونَ} [مريم: 39]».
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe,kisha muitaji ataita; Enyi watu wa peponi, basi watainua vichwa vyao na kuangalia, basi mwenye kuita atasema: Je mnamjua huyu? Nao watajibu: Ndiyo hayo ni Mauti, na wote kwa hakika wameyaona, kisha mwenye kuita atawaita: Enyi watu wa Motoni, basi watainua shingo zao na kuangalia, basi atawaambia na je mnamjua huyu basi watamjibu ndiyo haya ni Mauti, na wote kwa kakika wameyaona, hivyo basi yatachinjwa kisha atasema: Enyi watu wa Peponi,kaeni humo milele na hakuna kufa, na nyie watu wa motoni kaeni humo milele na hakuna kufa, kisha akasoma: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa Nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" (Surat Maryam:39)
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mauti yataletwa siku ya Kiyama, kwa mfano wa dume la kondoo lilochanganya rangi nyeupe na nyeusi, Basi ataita mwenye kuita: Enyi watu wa peponi! Basi watainua shingo zao na watainua vichwa vyao na wataangalia, Basi atawaambia: Je mnamjua huyu? Basi watasema: Ndiyo haya ni mauti, na wote kwa hakika wameyaona na kuyajua, Kisha muitaji ataita: Enyi watu wa Motoni, na watainua shingo zao na vichwa vyao na wataangalia, Basi atasema: Je mnamjua huyu? Hivyo watamjibu: Ndiyo, haya ni mauti, na wote wameyaona; Basi atachinjwa, kisha atasema mwenye kuita: Enyi watu wa peponi bakieni humo milele na hakuna kufa, na enyi watu wa Motoni bakieni humo milele na wala hakuna kufa, Na kumefanywa hivyo ili iwe ni ziada ya neema kwa waumini, na iwe ni adhabu yenye kuumiza kwa makafiri. Kisha akasoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Na uwaonye siku ya majuto wakati hukumu ya kuingia peponi na motoni itakapotolewa, nao wapo kwenye kughafilika na wala hawaamini" Hivyo basi siku ya Kiyama watatenganishwa watu wa Peponi na watu wa Motoni, na wataingia wote kule walipopangiwa na kukaa humo milele, Basi atajuta mkosaji atapata mshituko na kujuta kwa nini hakufanya mema, na mwenye matendo machache pia kwa nini hakuzidisha mambo ya heri.

Mafunzo
  1. Mafikio ya mwanadamu huko Akhera ni kukaa milele Peponi au Motoni,
  2. Kunatolewa tahadhari kubwa kutokana na mshituko utakao kuwa siku ya Kiyama, na kuwa siku hiyo ni siku ya mfadhaiko na majuto.
  3. Kumewekwa wazi kuhusu furaha ya kudumu kwa watu wa Peponi, na huzuni ya kudumu kwa watu wa Motoni,
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 93) (4730)، صحيح مسلم (4/ 2188) (2849)، التوضيح شرح الجامع الصحيح (22/595)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (19/ 52)، البحر المحيط الثجاج (43/686).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mayahudi wameghadhibikiwa, na Wakristo ni wapotofu

عَنْ ‌عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الْيَهُودُ مَغْضُوبٌ عَلَيْهِمْ، وَالنَّصَارَى ضُلَّالٌ».
Kutoka kwa Adiy bin Hatim kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mayahudi wameghadhibikiwa, na Wakristo ni wapotofu".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mayahudi ni watu waliokasirikiwa na Mwenyezi Mungu; kwa sababu waliujua ukweli na wala hawakuufanyia kazi. Na Wakristo ni watu waliopotea; kwa sababu walifanya matendo bila ya elimu.

Mafunzo
  1. Kukusanya kati elimu na matendo ni kuokoka na njia ya waliokasirikiwa na waliopotea.
  2. Kutahadhari njia ya Mayahudi na Wakristo, na kushikamana na njia iliyonyooka ambayo ni Uislamu.
  3. Wote kati ya Mayahudi na Wakristo wamepotea na wamekasirikiwa, lakini sifa maalum kwa Mayahudi ni hasira, na sifa maalum kwa Wakristo ni upotovu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 71) (2954)، النهاية في غريب الحديث و الأثر ( ص 548)، المنهل العذب المورود (5/250)، البحر المحيط الثجاج (9/248).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya

عَنْ ‌عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: تَلَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ هَذِهِ الْآيَةَ: {هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ، وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ، وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ} [آل عمران: 7]. قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَإِذَا رَأَيْتِ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ فَأُولَئِكَ الَّذِينَ سَمَّى اللهُ، فَاحْذَرُوهُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Aya hii :{Yeye ndiye ambaye alikuteremshia kitabu hiki ndani yake kuna Aya muhkam -zilizo wazi- aya hizo ambazo ndiyo msingi wa kitabu hiki na zipo nyingine zinatatiza, wale ambao nyoyoni mwao kuna upotofu watafuata zile zenye kutatiza kwa kutaka kufitinisha na kutaka kujua uhakika wa maana yake, na hakuna ajuaye uhakika wa maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wale wabobezi katika elimu wanasema tumeziamini zote zimetoka kwa Mola wetu na hawakumbuki isipokuwa wenye akili} (Al- imaraan 7) Anasema Aisha: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisoma aya hii: {Huwal ladhii Anzala alaikal kitaab minhu aayaatu muhkamaatun hunnaa ummul kitaab,wa ukharu mutashaabihaat,fa-ammal ladhiina fii quluubihim zaighun fayattabiuuna maatashaabaha minhu ib-tighaal fitnat wabtighaa taawiilihi,wamaa yaalamu taawilahu illa llahu warrasikhuuna fil ilmi yaquuluuna aamanna bihi kullu min in-di rabbinaa wamaa yaddhakkaru illa ulul al-baab}, Ndani ya aya hii Mwenyezi Mungu Mtukufu amefahamisha kuwa yeye ndiye aliyeteremsha Qur'ani kwa Mtume wake Qur'ani ambayo kuna aya zinazofahamika kwa uwazi, hukumu zake zinafahamika na hazitatizi, na aya hizo ni msingi wa kitabu hiki na ndiyo marejeo yake, nayo Qur'ani ndiyo marejeo inapotokea kutofautiana, na katika Qur'ani hiyo kuna aya zingine zinachukuwa maana zaidi ya moja maana zake zinawatatiza baadhi ya watu, au wanadhani kuwa kati ya aya na aya nyingine kuna mgongano, kisha akaweka wazi Mwenyezi Mungu namna watu wanavyozifanyia kazi aya hizi, basi wale ambao katika nyoyo zao kuna upotofu wa kuiwacha haki huziwacha aya zilizokuwa wazi, na wanachukuwa zile zenye kutatiza wakitaka kuibua utata na kuwatatiza watu, na kufanya hivyo wanataka kwa kutumia maana hiyo iafikiane na matamanio ya nafsi zao, ama wale ambao wamebobea kwenye elimu wanaujua utata huu, na wanazirudisha kwenye maana zilizo wazi na wanaziamini kuwa aya hizo zimetoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na haiwezekani zikapingana lakini hilo hawalikumbuki wala kupata mawaidha isipokuwa wale wenye akili iliyo salama, kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia mama wa waumini Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa ikiwa atawaona wenye kufuata aya zenye kutatiza basi hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika maneno yake aliposema: {Basi wale ambao katika nyoyo zao kuna maradhi} basi tahadhari nao na wala usiwasikilize.

Mafunzo
  1. Al-muhkam katika aya za Qur'ani: Ni zile ambazo ni nyepesi kuzifahamu maana zake zipo wazi, na zenye kutatiza ni zile zenye kuchukua zaidi ya maana moja na zinahitajia uchunguzi wa kina na ufahamu.
  2. Kuchukua tahadhari ya kutochanganyikana na watu waliopotoka, na watu wazushi na wenye kuleta mambo yenye kutatiza kwa ajili ya kuwapoteza watu na kuwatia mashaka.
  3. Katika kumalizia aya kwa maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu "Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili" Inaashiria kuwapinga wapotofu na kuwasifia waliojikita katika elimu, yaani asiyekumbuka wala kupata mawaidha, na akafuata matamanio ya nafsi yake huyo si miongoni mwa wenye kutumia akili.
  4. Kufuata mambo yenye kutatiza ni sababu ya kuupotosha moyo.
  5. Ni wajibu kuzirudisha aya ambazo maana zake zinatatiza na hazifahamiki maana zake, katika aya ambazo maana yake ni nyepesi kufahamika.
  6. Mwenyezi Mungu Mtukufu amezifanya baadhi ya aya kuwa ni nyepesi na zingine ni zenye kutatiza; Ili awajaribu watu na kuwapambanua wenye imani na watu waliopotea.
  7. Kwa kutokea aya zenye kutatiza katika Qur'ani: Ni kudhihirisha ubora wa maulamaa kuliko watu wengine, na kuifahamisha akili kuhusu mapungufu yake; ili ijisalimishe kwa muumba wake na ikubali kushindwa kwake.
  8. Ubora wa kujikita katika elimu na ulazima wa kudumu katika elimu.
  9. Na maulamaa wa tafsiri kwenye kusimama katika neno (Allah) katika maneno yake aliposema {Wamaa ya'alamu taawilahuu illa llahu warraasikhuuna fil ilmi} kuna kauli mbili, kwa yule atakayesimama katika neno (Allah), basi yanakuwa makusudio ya neno Taawiil ni ujuzi wa uhakika wa kitu kwa namna ambayo hakuna njia ya kuujua, kama vile jambo linalohusu roho na kiyama katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha katika elimu yake, na wale wabobezi katika elimu wao wanaziamini na wanaegemeza uhakika wake kwa Mwenyezi Mungu, hivyo basi wanajisalimisha na wanasalimika, na mwenye kupitiliza bila ya kusimama kwenye neno( Allah) basi inakuwa maana ya neno Taawili ni tafsiri na kuweka wazi, hivyo inakuwa Mwenyezi Mungu anajua na waliobobea katika elimu vilevile wanajua, hivyo wanakuwa ni wenye kuziamini na wana zirudisha kwenye aya zilizo nyepesi.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 33) (4547)، صحيح مسلم (4/ 2053) (2665)، فتح الباري (8/211)، شرح النووي على مسلم (16/217)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 407، 465)، فتح الودود في شرح سنن أبي داود (4/415)، تحفة الأبرار شرح مصابيح السنّة (1/129)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (41/ 559).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa

عَنْ ‌عَائِشَةَ رضي الله عنها: أَنَّ رَجُلًا قَعَدَ بَيْنَ يَدَيِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ لِي مَمْلُوكِينَ يَكْذِبُونَنِي وَيَخُونُونَنِي وَيَعْصُونَنِي، وَأَشْتُمُهُمْ وَأَضْرِبُهُمْ، فَكَيْفَ أَنَا مِنْهُمْ؟ قَالَ: «يُحْسَبُ مَا خَانُوكَ وَعَصَوْكَ وَكَذَّبُوكَ وَعِقَابُكَ إِيَّاهُمْ، فَإِنْ كَانَ عِقَابُكَ إِيَّاهُمْ بِقَدْرِ ذُنُوبِهِمْ كَانَ كَفَافًا، لَا لَكَ وَلَا عَلَيْكَ، وَإِنْ كَانَ عِقَابُكَ إِيَّاهُمْ دُونَ ذُنُوبِهِمْ كَانَ فَضْلًا لَكَ، وَإِنْ كَانَ عِقَابُكَ إِيَّاهُمْ فَوْقَ ذُنُوبِهِمُ اقْتُصَّ لَهُمْ مِنْكَ الْفَضْلُ»، قَالَ: فَتَنَحَّى الرَّجُلُ فَجَعَلَ يَبْكِي وَيَهْتِفُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَمَا تَقْرَأُ كِتَابَ اللهِ: {وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا}، الْآيَةَ»، فَقَالَ الرَّجُلُ: وَاللهِ يَا رَسُولَ اللهِ، مَا أَجِدُ لِي وَلهُمْ شَيْئًا خَيْرًا مِنْ مُفَارَقَتِهِمْ، أُشْهِدُكَ أَنَّهُمْ أَحْرَارٌ كُلُّهُمْ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kuwa mtu mmoja alikaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika mimi nina watu niliowamiliki, wakati mwingine wananidanganya na wananifanyia hiyana na wanakwenda kinyume na amri zangu, nahuwa nawatia adabu kwa kuwatukana na kuwapiga, hivyo naulizia kuwa ni vipi itakuwa hali yangu kwa kuwafanyia hayo?Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa basi ikiwa adhabu uliyowapa ipo sawa na makosa yao basi itatosha na hapatakuwa na chochote kwako wala kwao, na ikiwa adhabu uliyowapa ni ya chini kulingana na kosa walilofanya basi utalipwa na utazidishiwa kwenye malipo yako, na ikiwa umewaadhibu zaidi ya walivyokosea yatapunguzwa kutoka kwako malipo ya ziada" Akasema: Basi yule bwana alijitenga na akawa analia kwa sauti ya juu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia: "Hivi husomi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema: "Na Sisi tutaweka Mizani ya uadilifu siku ya Kiyama na hakuna nafsi yoyote itakayodhulumiwa kwa chochote", mpaka mwisho wa Aya, yule bwana akasema: Nakuapia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijaona kheri iliyopo kati yangu na yao zaidi ya kuwaachia huru, na ninakupa ushuhuda kuwa wao wote kuanzia sasa wako huru".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaDhaifu
Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akishitakia kuhusu matendo ya Watumwa wake, Watumwa hao wanamdanganya na kumfanyia hiyana katika amana, na wanafanya ghushi katika miamala, na wanakwenda kinyume na maelekezo yake, naye huwatia adabu kwa kuwatukana na kuwapiga, hivyo akaulizia kuhusu hali yake itakavyokuwa siku ya Kiyama, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Watahesabiwa kwa kile walichokufanyia hiyana na kwenda kinyume na maelekezo yako na kukudanganya na wewe utahesabiwa ulivyo waadhibu, basi ikiwa adhabu uliyowapa itakuwa sawa na makosa yao basi hutokuwa na kosa lolote, na ikiwa adhabu uliyowapa ni ndogo ikilinganishwa na kosa walilofanya basi ni jambo zuri utalipwa na utazidishiwa katika malipo yako, na ikiwa adhabu uliyowapa ni zaidi ya walichokifanya, basi utaadhibiwa na malipo yako uliyozidishiwa yatachukuliwa na watapewa wao, basi yule bwana akakaa pembeni akawa analia kwa sauti ya juu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia: "Hivi husomi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema: "Na Sisi tutaweka Mizani ya uadilifu siku ya Kiyama na hakuna nafsi yoyote itakayodhulumiwa kwa chochote, hata kama jambo hilo litakuwa na uzito sawa na punje ya Hardal tutalileta Nasi tunatosha kuwa wajuzi wa hisabu" (Al-Anbiyaa 47), hivyo basi hatodhulumiwa mtu yoyote siku ya kiyama, na kipimo cha watu kitakuwa cha uadilifu, yule bwana akasema: Nakuapia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijaona kheri iliyopo kati yangu na wao zaidi ya kuwaacha huru ninakupa ushuhuda kuwa wao wote kuanzia hivi sasa wako huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu; kwa kuogopea hesabu na adhabu.

Mafunzo
  1. Ukweli wa Swahaba katika kuwaacha huru watumwa wake kwa kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu.
  2. Inafaa kumuadhibu dhalimu ikiwa adhabu hiyo itakuwa sawa na makosa yake au kumwadhibu adhabu ndogo ikilinganishwa na kosa lake, ama kumzidishia adhabu ni haramu na haifai.
  3. Himizo la kuamiliana vizuri na watumishi na watu madhaifu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 227) (3165)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 804)، مرقاة المفاتيح (8/3533)، تحفة الأحوذي (9/3).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika haya unayoyasema na kuwalingania watu ni mambo mazuri, ikiwa utatwambia juu ya haya tuliyoyafanya kama yana kafara

عَنِ ‌ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: أَنَّ نَاسًا مِنْ أَهْلِ الشِّرْكِ، كَانُوا قَدْ قَتَلُوا وَأَكْثَرُوا، وَزَنَوْا وَأَكْثَرُوا، فَأَتَوْا مُحَمَّدًا صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالُوا: إِنَّ الَّذِي تَقُولُ وَتَدْعُو إِلَيْهِ لَحَسَنٌ، لَوْ تُخْبِرُنَا أَنَّ لِمَا عَمِلْنَا كَفَّارَةً، فَنَزَلَ {وَالَّذِينَ لا يَدْعُونَ مَعَ اللهِ إِلَهًا آخَرَ وَلا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللهُ إِلا بِالْحَقِّ وَلا يَزْنُونَ}[الفرقان: 68]، وَنَزَلَت: {قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللهِ} [الزمر: 53].
Imepokewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba watu miongoni mwa washirikina walikuwa wameuwa watu, na wakakithirisha mauaji, na wakazini na wakikithirisha zinaa, wakamjia Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- wakasema: Hakika haya unayoyasema na kuwalingania watu ni mambo mazuri, ikiwa utatwambia juu ya haya tuliyoyafanya kama yana kafara, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wale ambao hawamuombi pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwingine na wala hawauwi nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki na wala hawazini" [Al-Furqan: 68], na ikateremka: "Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu..." [Az-Zumar: 53].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Walikuja watu miongoni mwa washirikina kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na walikuwa wamekwisha fanya mauaji mengi na zinaa nyingi, wakasema kumwambia Mtume: Hakika Uislamu unaoulingania na mafundisho yake ni mazuri, lakini sisi tutakuwa na hali gani kwa yale tuliyoyatenda miongoni mwa ushirikina na madhambi makubwa, je, yanakafara?. Zikateremka aya mbili, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu aliwakubalia watu toba zao pamoja na wingi wa madhambi yao na ukubwa wake, na lau kama si hivyo basi wangeendelea kubaki katika ukafiri wao na ujeuri wao wala wasingeingia katika dini hii.

Mafunzo
  1. Ubora wa Uislamu na utukufu wake nakuwa Uislamu unabomoa madhambi yaliyokuwa kabla yake.
  2. Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na msamaha wake na kufuta kwake madhambi.
  3. Uharamu wa ushirikina, na uharamu wa kuua nafsi bila hatia, na uharamu wa zinaa, na ahadi ya adhabu kwa atakayeyasogelea ama kujiingiza katika madhambi haya.
  4. Toba ya kweli iliyoambatana na utakasifu (Ikhlaswi) na matendo mema, hufuta madhambi yote makubwa likiwemo la kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  5. Uharamu wa kukata tamaa na kunyongeka katika rehema za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 125) (4810)، صحيح مسلم (1/ 113) (122)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (7/ 319)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 808).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba

عَنِ ‌ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَطَبَ النَّاسَ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ، فَقَالَ: «يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللهَ قَدْ أَذْهَبَ عَنْكُمْ عُبِّيَّةَ الْجَاهِلِيَّةِ وَتَعَاظُمَهَا بِآبَائِهَا، فَالنَّاسُ رَجُلَانِ: بَرٌّ تَقِيٌّ كَرِيمٌ عَلَى اللهِ، وَفَاجِرٌ شَقِيٌّ هَيِّنٌ عَلَى اللهِ، وَالنَّاسُ بَنُو آدَمَ، وَخَلَقَ اللهُ آدَمَ مِنْ تُرَابٍ، قَالَ اللهُ: {يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُمْ مِنْ ذَكَرٍ وَأُنْثَى وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ} [الحجرات: 13]».
Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake: Ya kwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwahutubia watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka, akasema: "Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba , basi watu wako aina mbili: Mwema mchamungu mtukufu kwa Mwenyezi Mungu, na muovu mbaya dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na watu wote ni wana wa Adam, na amemuumba Mwenyezi Mungu Adam kutokana na udongo. Amesema Mwenyezi Mungu: "Enyi watu hakika sisi tumekuumbeni kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila tofauti tofauti, ili mfahamiane, hakika mbora wenu kwa Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (za mambo yote)" [Al Hujuraat: 13].
Imepokelewa na Tirmidhi na bin HibbanDarajaSahihi
Maelezo

Aliwahutubia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- watu siku ya ufunguzi wa mji wa Makka akasema: Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu amenyanyua na akaondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga na kujiona, na kujifaharisha kwa baba zenu (nasaba), bali watu wako aina mbili: Ni ima muumini mwema, mchamungu, mtiifu, mwenye kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, huyu ni mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, hata kama hana cheo au nasaba nzuri mbele za watu. Na ima kafiri muovu, na huyu ni dhalili kwa Mwenyezi Mungu, na wala hana thamani yoyote, hata kama ana ukoo mzuri na cheo na mamlaka. Na watu wote ni watoto wa Adam, na Mwenyezi Mungu kamuumba Adam kutokana na udongo, haifai kwa kiumbe ambaye asili yake ni udongo kuwa na kiburi na kujiona yeye ni bora, na hili linasadikishwa na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Enyi watu! hakika sisi tumekuumbeni nyinyi kutokana na mwanaume na mwanamke na tukakufanyeni kuwa mataifa na makabila ili mpate kujuana, hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu, hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi na ana habari (ya myafanyayo) [Alhujrat:13].

Mafunzo
  1. Katazo la kujifaharisha kwa ukoo na vyeo.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 309) (3270)، صحيح ابن حبان (9/ 137) (3828)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (14/ 16)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص587).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema

عَنْ ‌الزُّبَيْرِ بْنِ الْعَوَّامِ قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ: {ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ} [التكاثر: 8]، قَالَ الزُّبَيْرُ: يَا رَسُولَ اللهِ، وَأَيُّ النَّعِيمِ نُسْأَلُ عَنْهُ، وَإِنَّمَا هُمَا الْأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالْمَاءُ؟ قَالَ: «أَمَا إِنَّهُ سَيَكُونُ».
Kutoka kwa Zubairi bin Awwam amesema: Ilipoteremka: "Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema" [Takathur: 8], akasema Zubairi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazooulizwa juu yake, au ni hivi vyeusi viwili tende na maji (Vyakula na vinywaji kwa ujumla)? Akasema: "Hakika bila shaka zitakuwa hizo".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ilipoteremka aya: "Kisha hakika bila shaka mtaulizwa siku hiyo kuhusu neema" Yaani: Mtakuja kuulizwa kuhusu kutekeleza shukurani kwa yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu juu yenu miongoni mwa neema, akasema Zubairi bin Awwam radhi za Allah ziwe juu yake: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazoulizwa juu yake?! Ni neema mbili ambazo hazihitaji kuziomba ambazo ni tende na maji!. Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ama hakika nyinyi mtaulizwa kuhusu neema pamoja hali hii iliyo nayo, ni hizi neema mbili kubwa katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mafunzo
  1. Msisitizo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema.
  2. Neema ni miongoni mwa vile ambavyo mja ataulizwa kwavyo siku ya Kiyama.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 375) (3356)، سنن ابن ماجه (5/ 262) (4158)، شرح سنن ابن ماجه للسيوطي (ص: 307)، تحفة الأحوذي (9/203)، مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (25/ 251).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 10
Hadithi 10
  1. Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini
  2. Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe
  3. Mayahudi wameghadhibikiwa, na Wakristo ni wapotofu
  4. Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya
  5. Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa
  6. Hakika haya unayoyasema na kuwalingania watu ni mambo mazuri, ikiwa utatwambia juu ya haya tuliyoyafanya kama yana kafara
  7. Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba
  8. Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema
  9. bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako
  10. Funguo za mambo ya ghaibu ni tano

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com