Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Tafsiri ya Qur'an.

Hadithi 13

Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu

عن سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ، جَاءَهُ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَوَجَدَ عِنْدَهُ أَبَا جَهْلٍ وَعَبْدَ اللهِ بْنَ أَبِي أُمَيَّةَ بْنِ الْمُغِيرَةِ، فَقَالَ: «أَيْ عَمِّ، قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اللهِ»، فَقَالَ أَبُو جَهْلٍ وَعَبْدُ اللهِ بْنُ أَبِي أُمَيَّةَ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، فَلَمْ يَزَلْ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَعْرِضُهَا عَلَيْهِ، وَيُعِيدَانِهِ بِتِلْكَ الْمَقَالَةِ، حَتَّى قَالَ أَبُو طَالِبٍ آخِرَ مَا كَلَّمَهُمْ: عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: «وَاللهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ»، فَأَنْزَلَ اللهُ: {مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَنْ يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ} [التوبة: 113]، وَأَنْزَلَ اللهُ فِي أَبِي طَالِبٍ، فَقَالَ لِرَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم: {إِنَّكَ لا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَكِنَّ اللهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ} [القصص: 56].
Kutoka kwa Saidi Bin Musayyab, kutoka kwa baba yake amesema: Yalipomfika mauti Abuu Twalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimjia akamkuta yuko pamoja na Abuu Jahali na Abdallah Bin Umaiyya bin Mughiira, akasema: "Ewe baba yangu mdogo, sema: Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu) neno ambalo nitakutetea kwalo mbele ya Mwenyezi Mungu", Abuu Jahali akasema: Hivi unataka kuichukia mila ya Abdul Muttwalib (Yaani baba yake) Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaendelea kumrejelea neno hilo, nao pia wakirudia kumwambia maneno yao, mpaka Abuu Twalib akasema kwa neno lake la mwisho alilowasemesha: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, na akakataa kusema: Laa ilaaha illa llaah, mpokezi anasema: Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Wallahi (Namuapia Allah) nitakuombea msamaha kwa muda wote madam sijakatazwa, Allah akateremsha: "Haifai wala haitakiwi kwa Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina" [Attauba: 113], Na akateremsha kuhusu Abuu Twalib, akasema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika wewe humuongoi umpendaye, lakini Allah anamuongoa amtakaye" [Al-Qasas:56]
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliingia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa Ami yake Abuu Twalib akiwa katika hali ya kukaribia kufa, akasema kumwambia: Ewe Ami yangu sema "Laa ilaaha illa llaah", neno ambalo nitakutolea ushahidi kwalo mbele ya Allah, Abuu Jahali na Abdallah Bin Abiiy Umaiyya wakasema: "Wewe Abuu Twalib!, unaacha mila ya baba yako Abdul Muttwalib?! ambayo ni kuabudu masanamu, wakaendelea kumwambia hivyo mpaka akasema neno lake la mwisho alilowaambia kuwa: Niko katika mila ya Abdul Muttwalib, mila ya ushirikina na kuabudu masanamu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nitakuombea msamaha madam sijakatazwa na Mola wangu kuhusu hilo, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Haipasi kwa Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, hata kama watakuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni" [Attauba: 113], Na ikateremka kumuhusu Abuu Twalib kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wewe, humuongoi, unayependa aongoke. Lakini Mwenyezi Mungu, Anamuongoa Anayemtaka. Na Yeye Ndiye Anayemjua zaidi anayefaa kuongoka". Kwani hakika wewe humuongoi umpendaye kumuongoa, bali jukumu lako ni kufikisha, na Allah anamuongoa amtakaye.

Mafunzo
  1. Uharamu wa kuwaombea msamaha washirikina vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wao na matendo yao na wema wao.
  2. Kuwaiga mababa na wazee katika batili ni katika vitendo vya watu wa zama za ujinga.
  3. Ukamilifu wa huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na pupa yake katika kuwalingania watu na kuwaongoza.
  4. Hili ni jibu kwa watu wanaodai kuwa Abuu Twalib alisilimu.
  5. Matendo huzingatiwa mwisho.
  6. Kubatilika kujifungamanisha na kushikamana na Mtume au mwingine asiyekuwa yeye kwa lengo la kupata kheri na kuzuia madhara.
  7. Atakayesema "Laa ilaaha illa llaah" kwa kuwa na elimu na yakini na kuitakidi kwa dhati juu yake basi atakuwa kaingia ndani ya Uislamu.
  8. Madhara ya watu waovu na marafiki wabaya kwa mwanadam.
  9. Maana ya "Laa ilaaha illa llaah": Ni kuacha ibada za masanamu na wachamungu na watu wema na kumpwekeshea ibada Mwenyezi Mungu peke yake, nakwamba washirikina wanaju maana yake.
  10. Inafaa kumtembelea mgonjwa mshirikina ikiwa anatarajiwa huenda akasilimu.
  11. Uongofu wa kumuafikisha mja afungue moyo wake uko mkononi mwa Allah peke yake hana mshirika, bali jukumu la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kuongoza kwa kuelekeza, muongozo, na kufikisha ujumbe.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 112) (4772). صحيح مسلم (1/ 54) (24). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص155). الجديد في شرح كتاب التوحيد، للقرعاوي (ص169).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ: {إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا لِيَغْفِرَ لَكَ اللهُ} إِلَى قَوْلِهِ {فَوْزًا عَظِيمًا} [الفتح: ١-٥] مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ، وَهُمْ يُخَالِطُهُمُ الْحُزْنُ وَالْكَآبَةُ، وَقَدْ نَحَرَ الْهَدْيَ بِالْحُدَيْبِيَةِ، فَقَالَ: «لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَيَّ آيَةٌ هِيَ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنَ الدُّنْيَا جَمِيعًا».
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Ilipoteremka: "Hakika Sisi tumekufungulia wewe, ewe Mtume, ufunguzi ulio waziwazi, ili akusamehe Mwenyezi Mungu" mpaka katika kauli yake: "Ushindi mkubwa" [Fat-hi: 1-5] marejeo ya hili ni katika suluhu ya Hudaibia, na wao wakiwa wamejawa na huzuni na unyonge, na alichinja vichinjwa vyake hapo Hudaibia, akasema: "Hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya ninayoipenda zaidi kuliko dunia nzima".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Anasi bin Maaliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kauli yake Mtukufu: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi (1) Ili akusameheme Mwenyezi Mungu yaliyotangulia katika madhambi yako na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika njia iliyonyooka (2) Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu (3) Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waumini ili wazidi imani juu ya imani yao. Na Mwenyezi Mungu ndiye mwenye majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye ujuzi, mwenye hekima (4) Ili awaingize Waumini wanaume na Waumini wanawake katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo, na awafutie makosa yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu (5) [Al-Fat-hi: 1-5]. Hili lilikuwa Wakati wa kurejea kwake kutoka Hudaibia, na wakati Maswahaba wakiwa wamegubikwa na huzuni na unyonge, wakiwa wamezuiliwa kutekeleza Umra, kwa sababu ya yale waliyokubaliana katika mkataba, na dhana yao ilikuwa; yote hayo hayana masilahi na Waislamu, na walichinja vichinjwa vyao hapo Hudaibia, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwa hakika imeteremshwa juu yangu aya ni aya inayopendeka zaidi kwangu kuliko dunia nzima, kisha akaisoma.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa ukubwa wa yale aliyomneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu Mtume wake Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake katika ushindi mkubwa katika suluhu ya Hudaibia; pale aliposema kumwambia: "Hakika sisi tumekufungulia ufunguzi wa wazi wazi". mpaka mwisho wa aya mbili.
  2. Kumebainishwa yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu Mtukufu Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, walipotii amri yake na wakanyenyekea, kiasi ambacho aliteremsha kwao kauli yake Mtukufu: "Ili awaingize waumini wa kiume na waumini wa kike Pepo zinazopita chini yake mito" mpaka mwisho wa aya.
  3. Kumebainishwa fadhila za Mwenyezi Mungu juu ya Nabii wake, na kwa waumini kwa kuwaahidi ufunguzi na ushindi.
  4. Amesema Assa'di katika kuitafsiri kwake aya hii: "Hakika sisi tumekufungulia ewe Muhammadi ufunguzi wa wazi wazi" [Al-Fatha], Ushindi huu uliotajwa hapa ni Mkataba wa amani wa Hudaibia, pale washirikina walipomzuilia Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake – alipokuja kwa ajili ya kufanya Umra, katika kisa kirefu, ambacho mwisho wake ulikuwa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - alifanya nao suluhu juu ya kumaliza vita kati yake na wao kwa muda wa miaka kumi, na kwamba atafanya Umra katika mwaka uliofuata, na kwamba anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Makuraishi, ana ruhusa ya kufanya hivyo, na anayetaka kuingia katika mkataba wa kusaidiana na Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani ziwe juu yake, basi anaweza kufanya hivyo. Na sababu ya hilo kwamba pindi watu walipopata amani kutokana na wao kwa wao, eneo la kulingania kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu likapanuka, na akawa kila Muumini katika sehemu yoyote iliyopo katika nchi hizo anaweza kufanya hivyo, na likamwezesha mwenye uchu wa kuujua ukweli wa Uislamu kuujua. Kwa hivyo watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi wakati wa kipindi hicho. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akauita (mkataba huo) ushindi, na akauelezea kwamba ni ushindi ulio wazi. Kwa sababu makusudio ya kuziteka nchi za washirikina ni kuimarisha dini ya Mwenyezi Mungu na kuwapa ushindi Waislamu, na hili lilitokea kwa ushindi huo.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1413) (1786). تفسير القرطبي (16/ 259-265). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (31/ 234).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com