Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Vilivyo maalumu kwa Mtume.

Hadithi 1

Hakuna yeyote atakayenisalimia isipokuwa Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu ili nimjibu salam

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلَّى الله عليه وسلم قال: «ما مِنْ أحَدٍ يُسلِّمُ علي إلا ردَّ اللهُ عليَّ رُوحي حتى أردَّ عليه السَّلامَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakuna yeyote atakayenisalimia isipokuwa Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu ili nimjibu salam".
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadDarajaUpokezi wake ni mzuri
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hurejeshewa roho yake ili ajibu salam kwa kila aliyemsalimia sawa sawa awe karibu au mbali; na maisha ya Akhera na kaburini ni jambo la ghaibu, hakuna ajuaye uhalisia wake isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee, naye juu ya kila kitu ni muweza.

Mafunzo
  1. Himizo la kukithirisha kumswalia na kumtakia amani Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Maisha ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kaburi lake ni maisha kamili anayoishi mwanadam katika kaburi lake, hakuna awezaye kujua uhalisia wake ila Mwenyezi Mungu Mtukufu pekee.
  3. Hadithi hii si hoja kwa mtu anayesema kuwa Mtume rehema na mani ziwe juu yake yuko hai anaishi kama tunavyoishi sisi, tunasema hivi ili washirikina wasiitumie kama hoja ya kumtaka msaada Mtume rehema na amani ziwe juu yake, bali hayo ni maisha ya barzakh (kaburini).
Marejeo

سنن أبي داود (3/ 384) (2041). مسند أحمد (16/ 477) (10815). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 486). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 477). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 964).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com