Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama,

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَانْتَهَى إِلَى سُبَاطَةِ قَوْمٍ، فَبَالَ قَائِمًا، فَتَنَحَّيْتُ فَقَالَ: «ادْنُهْ» فَدَنَوْتُ حَتَّى قُمْتُ عِنْدَ عَقِبَيْهِ فَتَوَضَّأَ فَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ.
Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, nikasimama kando naye, alipomaliza akasema: “Sogea karibu” nikasogea mpaka nikasimama karibu naye, akatawadha, kisha akapangusa juu ya soksi (Khufu) zake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Imepokelewa kutoka kwa Hudhaifa bin Al-Yaman kwamba alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akataka kukidhi haja ndogo, akaingia dampo la watu fulani; Napo ni mahali ambapo takataka na uchafu unaofagiliwa kutoka majumbani hutupwa hapo, hivyo akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, na huwa anakidhi haja ndogo akiwa kachuchumaa. Basi Hudhaifa akajisogeza mbali naye, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Njoo karibu, basi Hudhaifa akamkaribia mpaka akasimama nyuma yake, nyuma ya miguu yake; Ili awe kama mstara kwake kutokana na watu kumtazama katika hali ile. Kisha akatawadha, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na wakati wa kuosha miguu yake, alitosheka kwa kupangusa juu ya soksi (Khofu) zake - nazo ni zile zinazovaliwa miguuni, zilizotengenezwa kwa ngozi nyembamba na mfano wake na zinazofunika vifundo vya miguu, na wala hakuzivua.

Mafunzo
  1. Sheria ya kupangusa juu ya Khufu (Soksi) mbili.
  2. Inafaa kukidhi haja wima, kwa sharti asidondokewe na chochote.
  3. Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alichagua Jalala, ambapo ni mahali pa kutupia taka za wafagiaji, kwa sababu huwa ni rahisi, na haja ndogo huwa hairudi tena kwa mkojoaji.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 54) (224). صحيح مسلم (1/ 228) (273). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص51). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 61).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kufuta juu ya Khofu mbili au soksi mbili

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com