Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kufuta juu ya Khofu mbili au soksi mbili

Hadithi 5

Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi

عَنْ المُغِيرَةِ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَأَهْوَيْتُ لِأَنْزِعَ خُفَّيْهِ، فَقَالَ: «دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ» فَمَسَحَ عَلَيْهِمَا.
Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika moja ya safari zake akatawadha, alipofikia kuosha miguu miwili alinyoosha Mughira bin Shu'ba Radhi za Allah ziwe juu yake mikono yake ili avue kilichokuwa miguuni kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika khufu (viatu mithili ya soksi) ili Mtume aoshe miguu yake! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ziache na wala usizivue, kwani mimi niliingiza miguu yangu ndaniya khufu mbili nikiwa katika twahara, Akafuta Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya khufu zake badala ya kuosha miguu miwili.

Mafunzo
  1. Sheria ya kufuta juu ya khufu mbili inakuwa wakati wa kutia udhu kwa ajili ya hadathi ndogo, ama kuoga kwa ajili ya hadathi kubwa ni lazima kuosha miguu.
  2. Kufuta kunakuwa mara moja kwa kupitisha mkono ulioloana juu ya khufu nasi chini yake.
  3. Ni sharti wakati wa kufuta juu ya khufu iwe kuzivaa kwake ni baada ya udhu kamili ambao aliosha miguu yake wakati huo kwa maji, na khufu ziwe twahara (safi) na zifunike mahali panapolazimika kuoshwa katika miguu, na kuwe kufuta ni katika hadathi ndogo si katika janaba au chochote kinachowajibisha kuoga, na kufuta kuwe katika muda uliopangwa kisheria nao ni usiku na mchana kwa mwenyeji na siku tatu kwa msafiri.
  4. Kitapimwa katika khufu mbili kila chenye kusitiri miguu miwili kama soksi na kinginecho, inafaa kufuta juu yake.
  5. Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mafundisho yake, kiasi kwamba alimzuia Mughira kumvua, na akamueleza sababu: Kuwa alizivaa akiwa twahara; ili nafsi yake itulizane, na ajue hukumu ya hilo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 52) (206). صحيح مسلم (1/ 230) (274). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص50). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 36). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص27).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama,

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَانْتَهَى إِلَى سُبَاطَةِ قَوْمٍ، فَبَالَ قَائِمًا، فَتَنَحَّيْتُ فَقَالَ: «ادْنُهْ» فَدَنَوْتُ حَتَّى قُمْتُ عِنْدَ عَقِبَيْهِ فَتَوَضَّأَ فَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ.
Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, nikasimama kando naye, alipomaliza akasema: “Sogea karibu” nikasogea mpaka nikasimama karibu naye, akatawadha, kisha akapangusa juu ya soksi (Khufu) zake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Imepokelewa kutoka kwa Hudhaifa bin Al-Yaman kwamba alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akataka kukidhi haja ndogo, akaingia dampo la watu fulani; Napo ni mahali ambapo takataka na uchafu unaofagiliwa kutoka majumbani hutupwa hapo, hivyo akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, na huwa anakidhi haja ndogo akiwa kachuchumaa. Basi Hudhaifa akajisogeza mbali naye, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Njoo karibu, basi Hudhaifa akamkaribia mpaka akasimama nyuma yake, nyuma ya miguu yake; Ili awe kama mstara kwake kutokana na watu kumtazama katika hali ile. Kisha akatawadha, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na wakati wa kuosha miguu yake, alitosheka kwa kupangusa juu ya soksi (Khofu) zake - nazo ni zile zinazovaliwa miguuni, zilizotengenezwa kwa ngozi nyembamba na mfano wake na zinazofunika vifundo vya miguu, na wala hakuzivua.

Mafunzo
  1. Sheria ya kupangusa juu ya Khufu (Soksi) mbili.
  2. Inafaa kukidhi haja wima, kwa sharti asidondokewe na chochote.
  3. Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alichagua Jalala, ambapo ni mahali pa kutupia taka za wafagiaji, kwa sababu huwa ni rahisi, na haja ndogo huwa hairudi tena kwa mkojoaji.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 54) (224). صحيح مسلم (1/ 228) (273). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص51). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 61).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi

عَنْ زِرِّ بْنِ حُبَيْشٍ قَالَ: أَتَيْتُ صَفْوَانَ بْنَ عَسَّالٍ المُرَادِيَّ، أَسْأَلُهُ عَنِ المَسْحِ عَلَى الخُفَّيْنِ، فَقَالَ: مَا جَاءَ بِكَ يَا زِرُّ؟ فَقُلْتُ: ابْتِغَاءَ العِلْمِ، فَقَالَ: إِنَّ المَلاَئِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا لِطَالِبِ العِلْمِ؛ رِضًا بِمَا يَطْلُبُ، فَقُلْتُ: إِنَّهُ حَكَّ فِي صَدْرِي المَسْحُ عَلَى الخُفَّيْنِ بَعْدَ الغَائِطِ وَالبَوْلِ، وَكُنْتَ امْرَأً مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَجِئْتُ أَسْأَلُكَ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكُرُ فِي ذَلِكَ شَيْئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كَانَ يَأْمُرُنَا إِذَا كُنَّا سَفْرًا أَوْ مُسَافِرِينَ أَلَّا نَنْزِعَ خِفَافَنَا ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيهِنَّ إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ، لَكِنْ مِنْ غَائِطٍ وَبَوْلٍ وَنَوْمٍ، فَقُلْتُ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكُرُ فِي الهَوَى شَيْئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ فَبَيْنَا نَحْنُ عِنْدَهُ إِذْ نَادَاهُ أَعْرَابِيٌّ بِصَوْتٍ لَهُ جَهْوَرِيٍّ: يَا مُحَمَّدُ، فَأَجَابَهُ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى نَحْوٍ مِنْ صَوْتِهِ: «هَاؤُمُ» وَقُلْنَا لَهُ: وَيْحَكَ اغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ، فَإِنَّكَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَدْ نُهِيتَ عَنْ هَذَا، فَقَالَ: وَاللَّهِ لاَ أَغْضُضُ، قَالَ الأَعْرَابِيُّ: المَرْءُ يُحِبُّ القَوْمَ وَلَمَّا يَلْحَقْ بِهِمْ، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ يَوْمَ القِيَامَةِ»، فَمَا زَالَ يُحَدِّثُنَا حَتَّى ذَكَرَ بَابًا مِنْ قِبَلِ المَغْرِبِ مَسِيرَةُ عَرْضِهِ، أَوْ يَسِيرُ الرَّاكِبُ فِي عَرْضِهِ أَرْبَعِينَ أَوْ سَبْعِينَ عَامًا.
Kutoka kwa Zirri bin Hubaishi amesema: Nilikwenda kwa Swafwan bin Assali Al-Muraadi, ili nimuulize kuhusu kufuta juu ya khofu mbili, akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Nikasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kile anachokitafuta, basi nikasema: Hakika mimi nimepata uzito ndani ya kifua changu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya kukidhi haja ndogo na kubwa, na wewe ulikuwa miongoni mwa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hivyo nimekuja kukuuliza: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu hilo? Akasema: Ndiyo, Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu matamanio? Akasema: Ndiyo, tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiendelea kuwa naye ghafla, Bedui mmoja alimuita kwa sauti kubwa na ya juu. Ewe Muhammadi!!!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa mfano wa sauti yake: "Ehee, niambie!" Tukasema kumwambia koma!, punguza sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kufanya hivi, akasema: Wallahi siwezi kupunguza, kisha Bedui akasema: Utakuta mtu anawapenda watu fulani lakini hajawahi kukutana nao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtu atakuwa pamoja na yule anayempenda siku ya Kiyama" Basi akaendelea kutusimulia mpaka akautaja mlango ulioko Magharibi mwendo wa upana wake, au anaweza kutembea aliyepanda kwenye upana wake kwa miaka arobaini au sabini.
Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja Zirri bin Hubaishi kwa Swafwan bin Assali radhi za Allah ziwe juu yake, ili amuulize kuhusu khofu mbili, Swafwan akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Akasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kutukuza kile anachokifanya mwenye kutafuta elimu, Zirii akasema: Hakika nimepata shaka ndani ya nafsi yangu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya haja kubwa na ndogo, na wewe ni katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nimekuja hapa kukuuliza, je, uliwahi kumsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitaja chochote kuhusu hili?. Akasema Swafwan: Ndiyo, alikuwa akituamrisha tunapokuwa wasafiri tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) kwa sababu ya hadathi (uchafu) mdogo, kama haja kubwa na ndogo na usingizi, isipokuwa janaba hapo basi ni wajibu kuvua, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu mapenzi? Akasema: Ndiyo: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiwa bado tuko pamoja naye mara ghafla Bedui mmoja aliita kwa sauti ya juu sana: Ewe Muhammadi!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa sauti ya juu karibu na sauti yake: Njoo, nasi tukasema kumwambia: Koma! Shusha sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kunyanyua sauti mbele yake. Akasema kwa sababu ya ukaidi wake: Wallahi siwezi kuishusha, Bedui akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, utakuta mtu anawapenda watu wema na hajafanya matendo mfano wa matendo yao? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Mtu atakuwa pamoja na anayempenda siku ya Kiyama, Anasema Zirri: Swafwan akaendelea kutuhadithia mpaka akataja mlango wa toba ulioko upande wa Sham aliuumba Mwenyezi Mungu siku aliyoumba Mbingu na Ardhi, anaweza kutembea aliyepanda juu ya kipando kwenye upana wake miaka arobaini au sabini, na wala haufungwi mpaka Jua lichomoze kutokea Magharibi yake.

Mafunzo
  1. Ubora wa kutafuta elimu, na nafasi ya mwenye kutafuta elimu, na Malaika kumfunika.
  2. Kumebainishwa pupa ya wanafunzi wa Maswahaba katika kutafuta elimu kutoka kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao.
  3. Kufaa kufuta juu ya khofu mbili, na muda wake: Kwa msafiri ni siku tatu (ikiwa ni pamoja na usiku wake), na kwa mkazi siku moja (masaa 24).
  4. Kufuta khofu mbili kunakuwa katika hadathi ndogo pekee.
  5. Inafaa kwa muulizaji kumuomba msomi ushahidi wa kile alichozungumza, je ni nukuu za maandiko au ni jitihada zake, na kwa msomi asijisikie vibaya kwa hilo.
  6. Kuwa na adabu na wanachuoni na watu wema, na kushusha sauti katika vikao vya kielimu.
  7. Kumfundisha asiyejua adabu nzuri na misingi ya tabia njema.
  8. Himizo la kujifunza kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika upole wake, na tabia zake njema, na kuzungumza kwake na watu kulingana na uelewa wao na akili zao.
  9. Amesema Mubaarakafuri: Hapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alinyanyua sauti yake kama sehemu ya kumhurumia ili zisiporomoke amali zake kutokana na kauli yake Mtukufu: "Msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii"; akampa udhuru kwa sababu ya ujinga wake, na alinyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake sauti yake mpaka ikawa mfano wa sauti yake au juu yake zaidi kwa sababu ya huruma yake iliyopita kiasi kwake.
  10. Kuwa na pupa ya kukaa na watu wema na kuwa karibu nao na kuwapenda.
  11. Amesema Nawawi: Na si lazima mtu kuwa nao mpaka daraja yake na malipo yake yawe mfano wao kwa namna zote.
  12. Kufungua mlango wa matumaini na matarajio, na kutoa habari njema ya kusalimika, na kuwa mpole katika mawaidha.
  13. Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kufungua kwake mlango wa toba.
  14. Himizo la kufanya haraka kuomba toba na kuihesabu nafsi na kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 505) (3535). سنن ابن ماجه (1/ 302) (478). مسند أحمد (30/ 18) (18095). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 36). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 107). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 57). المعجم الوسيط (2/ 968).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا تَوَضَّأَ أَحَدُكُمْ وَلَبِسَ خُفَّيْهِ فَلْيُصَلِّ فِيهِمَا، وَلْيَمْسَحْ عَلَيْهِمَا ثُمَّ لَا يَخْلَعْهُمَا إِنْ شَاءَ إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ».
Imepokewa kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba".
Imepokelewa na Addar- AlqutniDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu atakapovaa khofu zake baada ya kutawadha, kisha akatengukwa udhu baada ya hapo, na akataka kutawadha, basi anatakiwa afute juu yake akitaka kufanya hivyo, na aswali nazo wala asizivue kwa muda maalum, isipokuwa atakapopatwa na janaba hapo atalazimika kuvua khofu na kuoga.

Mafunzo
  1. Hairuhusiwi kufuta juu ya khofu mbili isipokuwa baada yakuwa na twahara kamili.
  2. Muda wa kufuta kwa mkazi: Ni mchana na usiku (Masaa 24), na kwa msafiri: Ni michana mitatu na usiku wake (Masaa 72).
  3. Kufuta juu ya Khofu mbili kunahusu tu hadathi ndogo nasi kubwa, ama hadathi kubwa haitakiwi kufuta, bali ni lazima kuvua khofu mbili na kuosha miguu miwili.
  4. Ni sunna kuswali na viatu na khofu na mfano wake na hii ni kwa sababu ya kwenda kinyume na Mayahudi, na hii ni pale viatu vitakapokuwa twahara (visafi), na havina udhia kwa wenye kuswali, au msikiti, mfano kama miskiti iliyotandikwa mabusati mtu hatakiwi kuswali navyo.
  5. Kufuta juu ya khofu mbili kuna urahisi na wepesi kwa umma huu.
Marejeo

سنن الدارقطني (1/ 376) (781). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 274). سبل السلام شرح بلوغ المرام، للصنعاني (1/ 86).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake

عَنْ إِبرَاهِيمَ النَّخَعِيِّ عَنْ هَمَّامِ بنِ الحَارِثِ قَالَ: بَالَ جَرِيرٌ، ثُمَّ تَوَضَّأَ، وَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ، فَقِيلَ: تَفْعَلُ هَذَا؟ فَقَالَ: نَعَمْ، رَأَيْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَالَ، ثُمَّ تَوَضَّأَ وَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ. قَالَ الأَعْمَشُ: قَالَ إِبْرَاهِيمُ: كَانَ يُعْجِبُهُمْ هَذَا الحَدِيثُ؛ لِأَنَّ إِسْلَامَ جَرِيرٍ، كَانَ بَعْدَ نُزُولِ المَائِدَةِ.
Kutoka kwa Ibrahim Nakhai kutoka kwa Hammamu bin Harithi amesema: Alikwenda haja ndogo Jariri kisha akatia udhu, na kafuta juu ya khufu zake, wakasema: Kwa nini unafanya hivi? Akasema: Ndio, Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake. Amesema A'mashi: Amesema Ibrahimu: Ilikuwa ikiwashangaza sana hadithi hii; kwa sababu kusilimu kwa Jariri kulikuwa baada ya kuteremka Suratul-Maaida.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikidhi haja ndogo Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake kisha akatawadha, na akatosheka na kufuta juu ya khofu zake na hakuosha miguu yake, wakasema kumwambia walioko nao: Mbona unafanya hivi?! Akasema: Ndio, nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatawadha na akafuta juu ya khofu zake. Na Jariri alisilimu kwa kuchelewa baada ya kuteremka kwa suratul-Maaida ambayo ndani yake ina aya ya udhu, akiashiria kuwa kufuta juu ya khufu hakukufutwa kwa aya hiyo.

Mafunzo
  1. Pupa ya Maswahaba na wanafunzi wao ya kufuata sunna ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Amesema Nawawi: Wamekubaliana wanaozingatiwa makubaliano yao juu ya kufaa kufuta juu ya khufu mbili, safarini na nyumbani, sawa sawa iwe kwa haja au bila haja, mpaka inafaa kwa mwanamke alioko nyumbani kwake na mgonjwa asiyeweza kutembea.
  3. Ubora wa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa na kifua kipana, akistahamili kukemewa na wanafunzi wake, hata kama wamekosea katika hilo.
  4. Kumjibu mwenye kukataa kufuta juu ya khufu mbili na akadai kuwa kulifutwa; kwa sababu hadithi ya Jariri radhi za Allah ziwe juu yake imechelewa kuliko aya ya udhu.
  5. Kumebainishwa kwamba ni lazima kwa mwenye kukemewa jambo na akawa akiitakidi usahihi wake asimkasirikie anayemkemea, bali ajadiliane naye kulingana na dhana yake, bali ambainishie hoja yake katika hilo kwa majibu mazuri.
  6. Kutoa ushihidi kupitia historia wakati wa haja ya kufanya hivyo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 87) (387). صحيح مسلم (1/ 227) (272). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (7/ 39).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com