Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Matamshi yaliyokatazwa na maafa ya ulimi.

Hadithi 2

Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata na uzza, basi aseme: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na atakayesema kumwambia ndugu yake: Njoo tucheze kamari, basi na atoe sadaka

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ حَلَفَ فَقَالَ فِي حَلِفِهِ: وَاللَّاتِ وَالعُزَّى، فَلْيَقُلْ: لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَمَنْ قَالَ لِصَاحِبِهِ: تَعَالَ أُقَامِرْكَ، فَلْيَتَصَدَّقْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakaye apa akasema katika kiapo chake: Na apa kwa Lata na uzza, basi aseme: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na atakayesema kumwambia ndugu yake: Njoo tucheze kamari, basi na atoe sadaka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu; kwani muumini haapi ila kwa Mwenyezi Mungu, Na anaeleza kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu; Kwa mfano mtu akiapa kwa Lata na Uzza - masanamu mawili yaliyokuwa yakiabudiwa katika zama za kabla ya Uislamu - basi aseme ndani ya nafsi yake: Hapana apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ili ajiepushe na ushirikina na ili iwe ni fidia ya kiapo chake hicho. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayemwambia rafiki yake: Njoo tucheze kamari - ambayo ni watu wawili au zaidi watakaposhindana kwa sharti kuwa baina yao kuna pesa ambayo mshindi ataichukua, na kila mmoja wao lazima ima apate hasara au faida-; ni sunna atoe sadaka kwa kitu chochote kama kafara ya yale aliyoyahamasisha.

Mafunzo
  1. Kiapo hakiwi isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake.
  2. Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu, ama kuapa kwa masanamu kama Lata au Uzza au kuapia amana, au kuapa kwa Mtume au kitu kingine chochote.
  3. Amesema Khattwabi: Kiapo kinakuwa kwa Muabudiwa Mtukufu, basi akiapa kwa Lata na mfano wa hayo anakuwa kawaiga makafiri, basi akaamrishwa kukirekebisha kwa neno la tauhidi.
  4. Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu si lazima atoe kafara ya kiapo chake, bali anatakiwa kutubia na kuomba msamaha, kwa sababu hilo ni kubwa mno kuliko kusamehewa na kisichokuwa toba.
  5. Kumeharamishwa kamari kwa aina zake zote na mitindo yake yote, ambayo ni kamari aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na akaiambatanisha na pombe na masanamu.
  6. Ulazima wa kurudi na kuacha maasi wakati wa kuyafanya.
  7. Atakayefanya jambo baya anatakiwa afuatishe jambo jema; kwa sababu matendo mema huondoa maovu.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 141) (4860). صحيح مسلم (3/ 1268) (1647). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (2/1228). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 273).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رضي الله عنهما قال: قال رَسولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَرْبَعٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ كَانَ مُنَافِقًا خَالِصًا، وَمَنْ كَانَتْ فِيهِ خَلَّةٌ مِنْهُنَّ كَانَتْ فِيهِ خَلَّةٌ مِنْ نِفَاقٍ حَتَّى يَدَعَهَا: إِذَا حَدَّثَ كَذَبَ، وَإِذَا عَاهَدَ غَدَرَ، وَإِذَا وَعَدَ أَخْلَفَ، وَإِذَا خَاصَمَ فَجَرَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Tabia nne amezitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zitakapokusanyika kwa muislamu atakuwa na mfanano mkubwa na wanafiki kwa sababu ya tabia hizi, na hili linakuwa kwa yule ambaye sifa hizi ndio tabia yake mara kwa mara, ama atakayezifanya mara chache huyu haingii katika sifa hizi, nazo ni: Ya kwanza: Akizungumza husema uongo kwa makusudi na kutokuwa mkweli katika maneno yake. Ya pili: Akitoa ahadi katika makubaliano haitimizi, na humfanyia hiyana aliyeahidiana naye. Ya tatu: Akiahidi ahadi yoyote haitimizi na huenda kinyume. Ya nne: Akizozana na akagombana na yeyote ugomvi wake huwa mkali sana, na hupotoka katika haki, na hufanya hila ya kuipinga na kuibatilisha, na husema maneno ya batili na uongo. Unafiki ni mtu kudhihirisha tofauti na yale anayoyaficha, na maana hii ipo kwa mtu mwenye sifa hizi, na unafiki wake unamuhusu yule anayezungumza naye, na akamuahidi, na akamwamini, na akagombana naye, na akamuahidi mtu, si kwamba atakuwa mnafiki katika Uislamu anaudhihirisha na kuficha ukafiri, hapana, na atakayekuwa na sifa moja katika sifa hizi; basi atakuwa na sifa ya unafiki ndani yake hadi atakapoiacha.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa baadhi ya alama za mnafiki na tahadhari ya kutoangukia katika unafiki.
  2. Makusudio ya hadithi: Ni kuwa sifa hizi ni sifa za unafiki, na mwenye sifa hizi anafanana na wanafiki kwa sifa hizi, na amejipamba kwa tabia zao, haina maana kuwa ni mnafiki anayedhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa hii inachukuliwa kwa mtu ambaye zitakuwa nyingi kwake sifa hizi na akazipuuzia, na akaziona ndogo; basi atakayekuwa hivyo mara nyingi huwa kaharibika katika itikadi yake.
  3. Amesema Imam Ghazal: Msingi wa dini zote umekusanywa na mambo matatu: Kauli, kitendo, na nia, akatanabahisha kuwa kuharibika kwa maneno ni kwa uongo, na kuharibika kwa vitendo kunakuwa kwa hiyana, na kuharika kwa nia ni kwa kwenda kinyume; kwa sababu kwenda kinyume na ahadi hakumchafui mtu isipokuwa maazimio yake yatakapoambatanishwa na ahadi, ama atakapokusudia kisha kikamtokea kizuizi au akabadili mtazamo huyu hatokuwa na sura ya unafiki.
  4. Unafiki una aina mbili: Unafiki wa kiitikadi unamtoa mtu katika imani, nao ni kudhihirisha Uislamu na kuficha ukafiri, na unafiki wa vitendo, nao ni kujifananisha na wanafiki katika tabia zao, na huu haumtoi mtu katika imani, isipokuwa ni dhambi katika madhambi makubwa.
  5. Amesema bin Hajari: Na wamekubaliana wanachuoni kuwa atakayesadikisha kwa moyo wake na ulimi wake na akafanya mambo haya hahukumiwi kwa ukafiri, wala si mnafiki atakayekaa motoni milele.
  6. Amesema Imam Nawawi: Na wamesema wanachuoni wengi kuwa: Makusudio yake ni wanafiki waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake walizungumza kwa imani yao, na wakapinga, na wakaaminiwa kwa dini yao wao wakafanya hiyana, na wakaahidi katika swala la dini na kuinusuru, wakaenda kinyume, na wakavuka mipaka katika ugomvi wao.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 16) (34)، صحيح مسلم (1/ 78) (58)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 250)، بهجة قلوب الأبرار (ص 26)، البحر المحيط الثجاج (2/370).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com