Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayeandaa mnyama kwa ajili ya kuchinja, na ukaandama mwandamo wa mwezi Dhul Hija, basi asipunguze chochote katika nywele zake wala kucha zake mpaka atakapochinja mnyama wake wa Udh-hiya

عَن أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رضي الله عنها قَالت: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ كَانَ لَهُ ذِبْحٌ يَذْبَحُهُ فَإِذَا أُهِلَّ هِلَالُ ذِي الْحِجَّةِ، فَلَا يَأْخُذَنَّ مِنْ شَعْرِهِ، وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا حَتَّى يُضَحِّيَ».
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeandaa mnyama kwa ajili ya kuchinja, na ukaandama mwandamo wa mwezi Dhul Hija, basi asipunguze chochote katika nywele zake wala kucha zake mpaka atakapochinja mnyama wake wa Udh-hiya"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayetaka kuchinja Udh-hiya asipunguze chochote katika nywele za kichwa chake au kwapa yake au sharubu zake au zinginezo, wala sehemu ya kucha za mikono yake wala miguu yake utakapoonekana mwandamo wa Dhul-Hija mpaka atakapochinja.

Mafunzo
  1. Atakayenuia kuchinja baada ya kuingia siku kumi basi aanze kujizuia kulikoelezwa kwanzia wakati aliponuia mpaka atakapochinja.
  2. Asipochinja katika siku ya kwanza, ataendelea kujizuia mpaka atakapochinja katika siku yoyote miongoni mwa siku za kubanika nyama.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1566) (1977). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 199). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 450). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1165).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Vichinjwa.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com