Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alichinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kondoo wawili wazuri weupe wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akasema, Bismillahi Allaahu Akbar, na akaweka mguu wake ubavuni mwao.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichinja kwa mkono wake siku ya Idil Adh-haa kondoo wawili madume wenye mapembe, weupe wenye mchanganyiko na weusi, na akasema: Bismillaahi wallaahu Akbaru, na akaweka mguu wake katika shingo zao.
Mafunzo
Sheria ya kuchinja siku ya Idi kubwa (Adh-ha), na waislamu wote wamekubaliana hilo.
Kilichobora zaidi ni kuwa kichinjwa kiwe cha aina hii aliyochinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa muonekano wake mzuri lakini pia mafuta yake na nyama yake nzuri.
Amesema Imam Nawawi: Hapa kuna sunna ya mtu asimamie mwenyewe kuchinja kichinjwa chake cha udhuhia, na wala asimuwakilishe yeyote ila kwa udhuru, na hapo pia ni sunna ashuhudie kichinjwa chake, na ikiwa atamuweka muislamu kwa niaba yake itafaa kwa itifaki ya wanachuoni.
Amesema bin Hajari: Na hapa kuna sunna ya kutoa takbira (Allaahu Akbaru) pamoja na kumtaja Mwenyezi Mungu (Bismillaah) wakati wa kuchinja, na kuweka mguu katika weupe wa shingo wa kulia wa mnyama, na wamekubaliana wanachuoni kuwa ubavu wake unakuwa upande wa kushoto ataweka mguu wake wa kulia ili iwe rahisi kumchinja wakati wa kuchukua kisu kwa mkono wa kulia na kukamata kichwa chake kwa mkono wake wa kulia
Ni sunna kichinjwa cha udh-hiya kiwe na pembe na inafaa pia kwa kinginecho.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 102) (5565).
صحيح مسلم (3/ 1556) (1966).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص724).
الإعلام بفوائد عمدة الأحكام، لابن الملقن (10/ 179).
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeandaa mnyama kwa ajili ya kuchinja, na ukaandama mwandamo wa mwezi Dhul Hija, basi asipunguze chochote katika nywele zake wala kucha zake mpaka atakapochinja mnyama wake wa Udh-hiya"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amemuamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayetaka kuchinja Udh-hiya asipunguze chochote katika nywele za kichwa chake au kwapa yake au sharubu zake au zinginezo, wala sehemu ya kucha za mikono yake wala miguu yake utakapoonekana mwandamo wa Dhul-Hija mpaka atakapochinja.
Mafunzo
Atakayenuia kuchinja baada ya kuingia siku kumi basi aanze kujizuia kulikoelezwa kwanzia wakati aliponuia mpaka atakapochinja.
Asipochinja katika siku ya kwanza, ataendelea kujizuia mpaka atakapochinja katika siku yoyote miongoni mwa siku za kubanika nyama.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1566) (1977).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 199).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 450).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1165).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com