Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake zinapokuja siku kumi za mwisho wa ramadhani anajitahidi ndani yake kwa kufanya ibada na utiifu, na akipitiliza katika kufanya aina mbalimbali za kheri na aina za wema na ibada zaidi kuliko namna anavyojitahidi katika siku zingine; na hii ni kwa sababu ya utukufu na fadhila za siku hizi, na ni kwa sababu ya kuitafuta Lailatul Qadri (usiku wa cheo).
Mafunzo
Himizo la kukithirisha kutenda wema na aina mbalimbali za ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa ujumla na hasa hasa siku kumi za mwisho.
Siku kumi za mwisho wa Ramadhani zinaanzia usiku wa tarehe ishirini na moja mpaka mwisho wa mwezi.
Ni sunna kufaidika na nyakati bora kwa ibada.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 832) (1175).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (14/ 463).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 848).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 339).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com