عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمِنينَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَجْتَهِدُ فِي الْعَشْرِ الْأَوَاخِرِ مَا لَا يَجْتَهِدُ فِي غَيْرِهِ.
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake zinapokuja siku kumi za mwisho wa ramadhani anajitahidi ndani yake kwa kufanya ibada na utiifu, na akipitiliza katika kufanya aina mbalimbali za kheri na aina za wema na ibada zaidi kuliko namna anavyojitahidi katika siku zingine; na hii ni kwa sababu ya utukufu na fadhila za siku hizi, na ni kwa sababu ya kuitafuta Lailatul Qadri (usiku wa cheo).
Mafunzo
- Himizo la kukithirisha kutenda wema na aina mbalimbali za ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa ujumla na hasa hasa siku kumi za mwisho.
- Siku kumi za mwisho wa Ramadhani zinaanzia usiku wa tarehe ishirini na moja mpaka mwisho wa mwezi.
- Ni sunna kufaidika na nyakati bora kwa ibada.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 832) (1175).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (14/ 463).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 848).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 339).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ يَقُمْ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kusimama usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) kwa imani na kutaraji malipo, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu fadhila za kusimama usiku wa cheo unaokuwa katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, nakuwa yeyote mwenye kujitahidi ndani yake kwa ibada ya swala na dua na kusoma Qur'ani na kumtaja Allah, akiwa na imani na hayo, na kwa fadhila zilizoelezwa kwayo, akitaraji kwa amali yake malipo ya Allah Mtukufu, si kwa kutaka kuonekana na kusikika, basi husamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake.
Mafunzo
- Fadhila za usiku wa cheo, na himizo la kusimama ndani yake.
- Matendo mema hayakubaliki isipokuwa kwa nia ya dhati na ya kweli.
- Fadhila za Allah na huruma yake, kwani mwenye kusimama usiku wa cheo kwa imani na kwa kutaraji malipo husamehewa madhambi yake yaliyotangulia.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 16) (35).
صحيح مسلم (1/ 523) (760).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (14/ 435).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 337).
نزهة المتقين، (2/ 846).
شرح النووي على مسلم (6/ 40).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 220).
شرح صحيح البخاري، لابن بطال (4/ 21).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «تَحَرَّوْا لَيْلَةَ القَدْرِ فِي الوِتْرِ مِنَ العَشْرِ الأَوَاخِرِ مِنْ رَمَضَانَ».
Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufanya juhudi kuutafuta usiku wenye cheo kwa kuzidisha amali njema, nao hutarajiwa zaidi kupatikana katika siku za witiri za siku kumi za mwisho wa Ramadhani kila mwaka, nazo ni: Ishirini na moja, na ishirini na tatu, na ishirini na tano, na ishirini na saba, na ishirini na tisa.
Mafunzo
- Fadhila za usiku wenye cheo (Lailatul-Qadri) na himizo la kuutafuta.
- Katika hekima za Mwenyezi Mungu na rehema zake aliuficha usiku huu ili watu wafanye jitihada katika ibada, kwa ajili ya kuutafuta, ili zikithiri thawabu zao.
- Usiku wenye cheo uko katika kumi la mwisho la Ramadhani, na katika siku za witiri ndio hutarajiwa zaidi.
- Usiku wenye cheo ni moja kati ya siku za kumi la mwisho la Ramadhani, nao ndio usiku ambao Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur'ani ndani yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akaufanya usiku huu kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja katika baraka zake, na utukufu wa heshima yake, na athari ya matendo mema ndani yake.
- Umeitwa kuwa ni usiku wa Lailatul-Qadri, kwa kuiwekea sakna dali, ima ni kwa sababu ya utukufu wake, husemwa: Fulani anacheo kikubwa, inakuwa kuuambatanisha usiku ni katika sehemu ya kuambatanisha kitu katika sifa yake, yaani usiku mtukufu, yaani unacheo kikubwa kwa utukufu na thamani na nafasi mpaka mwisho wake, "Hakika sisi tumeiteremsha katika usiku wenye baraka" [Ad-Dukhan: 3]. Na ima imetokana na kukadiria: Inakuwa kuambatanishwa kwake ni kuambatanishwa kwa kuambatana na kile kinachokizunguka, yaani ni usiku ambao ndani yake kunakuwa na makadirio ya yale yatakayoendelea katika mwaka mzima, "Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima" [Ad-Dukhan: 4].
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 46) (2017).
صحيح مسلم (2/ 828) (1169).
تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص347).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (3/ 470).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رِجَالًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُرُوا لَيْلَةَ القَدْرِ فِي المَنَامِ فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَرَى رُؤْيَاكُمْ قَدْ تَوَاطَأَتْ فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ، فَمَنْ كَانَ مُتَحَرِّيهَا فَلْيَتَحَرَّهَا فِي السَّبْعِ الأَوَاخِرِ».
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-: Yakwamba kuna baadhi ya watu katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, walionyeshwa Lailatul qadri ndotoni katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Naona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho, basi atakayetaka kuitafuta basi na aitafute katika siku saba za mwisho".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Wanaume katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake waliona ndotoni kuwa Lailatul Qadri inakuwa katika siku saba za mwisho wa Ramadhani. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ninaona ndoto zenu zimeafikiana katika siku saba za mwisho wa Ramadhani, atakayeitaka, akiwa na pupa ya kuitafuta, basi ajitahidi kuiwinda na kuitafuta kwa kukithirisha matendo mema kwani inatarajiwa zaidi kuwa katika siku saba za mwisho, nazo zinaanza kwanzia usiku wa tarehe ishirini na nne mwezi wa Ramadhani unapokuwa na siku thelathini, na zinaanza usiku wa tarehe thelathini na tatu mwezi unapokuwa wa siku ishirini na tisa.
Mafunzo
- Ubora wa Lailatul-Qadri na himizo la kuitafuta.
- Miongoni mwa hekima za Mwenyezi Mungu na huruma yake aliuficha usiku huu ili watu waongeze juhudi katika ibada, kwa ajili ya kuutafuta, ili zikithiri thawabu zao.
- Usiku wa Lailatul-Qadri uko katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, na katika siku saba za mwisho ndio hutarajiwa zaidi.
- Usiku wenye cheo ni moja kati ya siku za kumi la mwisho la Ramadhani, nao ndio usiku ambao Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur'ani ndani yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akaufanya usiku huu kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja katika baraka zake, na utukufu wa heshima yake, na athari ya matendo mema ndani yake.
- Umeitwa kuwa ni usiku wa Lailatul-Qadri, kwa kuiwekea sakna dali, ima ni kwa sababu ya utukufu wake, husemwa: Fulani anacheo kikubwa, inakuwa kuuambatanisha usiku ni katika sehemu ya kuambatanisha kitu katika sifa yake, yaani usiku mtukufu, yaani unacheo kikubwa kwa utukufu na thamani na nafasi mpaka mwisho wake, "Hakika sisi tumeiteremsha katika usiku wenye baraka" [Ad-Dukhan: 3]. Na ima imetokana na kukadiria: Inakuwa kuambatanishwa kwake ni kuambatanishwa kwa kiambata na kile kinachokizunguka, yaani ni usiku ambao ndani yake kunakuwa na makadirio ya yale yatakayoendelea katika mwaka mzima, "Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima" [Ad-Dukhan: 4].
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 46) (2015).
صحيح مسلم (2/ 822) (1165).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (3/ 467).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص347).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ الْعَشْرُ أَحْيَا اللَّيْلَ، وَأَيْقَظَ أَهْلَهُ، وَجَدَّ وَشَدَّ الْمِئْزَرَ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhani) anauhuisha usiku, na anawaamsha watu wake, na anaongeza juhudi na anakaza kikoi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi za mwisho wa ramadhani anauhuisha usiku wote kwa aina mbali mbali za ibada, na anawaamsha familia yake kwa ajili ya swala, na anajitahidi katika ibada zaidi ya kawaida yake, na anajitenga kwa ajili yake na anajitenga na wake zake.
Mafunzo
- Himizo na kufaidika na nyakati bora kwa matendo mema.
- Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii: Nikuwa inapendeza kuzidisha katika ibada mbali mbali katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, na kupendeza kuhuisha siku zake kwa ibada mbali mbali.
- Yampasa kila mja awe na pupa kwa familia yake ya kuwaamrisha kufanya ibada, na awe mvumilivu juu yao.
- Kufanya mambo ya heri kunahitaji uthubutu na subira na kuvumilia.
- Amesema Nawawi: Wametofautiana wanachuoni katika maana ya (Kukaza kikoi) wakasema: Ni kuongeza juhudi katika ibada zaidi ya kawaida yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati zingine, na maana yake: Ni kujipinda katika ibada, husemwa: Jambo hili nimelifungia kikoi, yaani: Nimelidhamiria na nimetenga muda wangu kwa ajili yake, na wamesema wengine: Ni fumbo la kujitenga na wanawake kwa ajili ya kushughulika na ibada.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 47) (2024).
صحيح مسلم (2/ 832) (1174).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 132).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 181).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com