Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona mtu mmoja watu wamemkusanyikia na wamemzingira ili kumkinga na joto la jua na wingi wa kiu, akasema: Kapatwa na nini? Wakasema: Anaswaumu, akasema: Si katika wema kufunga safarini, Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni.
- Kumebainishwa wepesi wa Uislamu.
- Inafaa kufunga safarini, na pia inafaa kuchukua ruhusa ya kula.
- Inachukiza kufunga safarini ikiwa ataelemewa, madam hali haitomfikisha katika maangamivu.
- Amesema Nawawi: Si katika wema nyinyi kufunga mkiwa safarini: Maana yake: Ikiwa swaumu itawapa tabu juu yenu na mkahofia madhara, na mlolongo wa hadithi unaashiria maana hii.
- Kuwatilia umuhimu Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake na kuuliza kwake hali zao.
صحيح البخاري (3/ 34) (1946). صحيح مسلم (2/ 786) (1115). تيسير العلام، للبسام (ص327). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 433).