Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Funga za watu wenye Dharura.

Hadithi 1

Si katika wema kufunga safarini

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَرَأَى زِحَامًا وَرَجُلًا قَدْ ظُلِّلَ عَلَيْهِ، فَقَالَ: «مَا هَذَا؟»، فَقَالُوا: صَائِمٌ، فَقَالَ: «لَيْسَ مِنَ البِرِّ الصَّوْمُ فِي السَّفَرِ»، وَفِي لَفْظٍ لِمُسلِمٍ: «عَلَيْكُمْ بِرُخْصَةِ اللهِ الَّذِي رَخَّصَ لَكُمْ».
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona msongamano na mtu kazingirwa, akasema: "Nini hicho?", wakasema: Alikuwa kafunga swaumu, akasema: "Si katika wema kufunga safarini", na katika tamko la Muslim: "Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaona mtu mmoja watu wamemkusanyikia na wamemzingira ili kumkinga na joto la jua na wingi wa kiu, akasema: Kapatwa na nini? Wakasema: Anaswaumu, akasema: Si katika wema kufunga safarini, Chukuweni ruhusa ya Mwenyezi Mungu aliyokuruhusuni.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa wepesi wa Uislamu.
  2. Inafaa kufunga safarini, na pia inafaa kuchukua ruhusa ya kula.
  3. Inachukiza kufunga safarini ikiwa ataelemewa, madam hali haitomfikisha katika maangamivu.
  4. Amesema Nawawi: Si katika wema nyinyi kufunga mkiwa safarini: Maana yake: Ikiwa swaumu itawapa tabu juu yenu na mkahofia madhara, na mlolongo wa hadithi unaashiria maana hii.
  5. Kuwatilia umuhimu Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake na kuuliza kwake hali zao.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 34) (1946). صحيح مسلم (2/ 786) (1115). تيسير العلام، للبسام (ص327). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 433).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com