Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka

عن أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَسَحَّرُوا، فَإِنَّ فِي السَّحُورِ بَرَكَةً».
Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kula daku, nako ni kula mwisho wa usiku ili kujiandaa kwa ajili ya swaumu; kwa sababu ndani yake kuna baraka, na kheri nyingi, yakiwemo malipo na thawabu, na kusimama katika wakati wa mwisho kwa ajili ya kuomba dua, na kupata nguvu kwa ajili ya swaumu, na kupata uchangamfu kwa ajili yake, na kupunguza uzito wake.

Mafunzo
  1. Sunna ya kula daku na kutekeleza amri ya sheria kwa kufanya hivyo.
  2. Amesema bin Hajari katika kitabu Fat-hulbaari: Baraka katika daku zinapatikana kwa namna nyingi: Nayo ni kufuata sunna na kwenda kinyume na Mayahudi na Wakristo, na kupata nguvu kutokana na daku kwa ajili ya ibada, na kuongeza uchangamfu, na kuondoa tabia mbaya inayosababishwa na njaa, na kuwa sababu ya kutoa sadaka kwa mwenye kuomba kwa wakati huo, au akajumuika pamoja naye katika chakula, na ni sababu ya kufanya dhikri na dua katika wakati ambao kuna matarajio makubwa ya kujibiwa, na kuipata nia ya kufunga kwa yule aliyejisahau kabla ya kulala.
  3. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa akioanisha hukumu kwa hukumu; ili mioyo ya watu ikunjuke, na ujulikane utukufu wa sheria.
  4. Amesema bin Hajari: Daku inapatikana kwa chochote kidogo atakachokula mtu, katika vyakula au vinywaji.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 29) (1923). صحيح مسلم (2/ 770) (1095). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص317). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 416).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sunnah za Funga.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com