Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Sunnah za Funga.

Hadithi 3

Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا عَجَّلُوا الْفِطْرَ».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Wanaendelea watu kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa watu wataendelea kuwa katika kheri kwa muda wote watakaofanya haraka kufuturu ndani ya Ramadhani baada kuhakiki kuzama kwa Jua; na hii ni kwa sababu ya kutekeleza sunna, na kusimama katika mpaka wake.

Mafunzo
  1. Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kuwahisha kufuturu baada ya kuhakikisha kuzama kwa Jua, na maana yake nikuwa jambo la umma litaendelea kuwa katika nidhamu nao wakiwa katika kheri madam wanadumu na sunna hii, na wakichelewesha hiyo itakuwa ni alama ya kuharibikiwa wanakoangukia.
  2. Kubakia kwa kheri kwa watu ni kwa sababu ya kufuata kwao sunna, na kuharibika kwa mambo kunahusiana na kubadilishwa kwa sunna.
  3. Kwenda kinyume na Mayahudi na wakristo na watu wa bid'a, kwani wao huchelewesha kufuturu.
  4. Amesema bin Hajari: Hapa kumebainishwa sababu katika hilo, amesema Muhallab: Na hekima katika hilo ili mchana usiongezwe kuwa mrefu kwa kuchukua sehemu ya usiku, na ni kwa sababu mchana ndio mzuri kwa kufunga na unamtia nguvu kwake ya kufunga, na wamekubaliana wanachuoni kuwa mahala pa hilo ni pale kutakapothibitika kuzama kwa Jua kwa kuliona au kupewa habari na waadilifu wawili, na hata muadilifu mmoja katika kauli yenye nguvu zaidi anatosha.
  5. Amesema bin Hajari: Angalizo: Miongoni mwa bid'a mbaya ni yale yaliyozushwa katika zama hizi kwa kutoa adhana ya pili kabla ya Alfajiri kwa takribani saa nzima ndani ya Ramadhani, na kuzima taa ambazo zimewekwa kuwa ni alama ya kuharamisha kula na kunywa kwa yule mwenye kutaka kufunga, kwa madai kutoka kwa yule aliyezusha hilo kuwa wanachukua tahadhari katika ibada, na hawalifahamu hilo ila watu wachache, na liliwatia ujasiri hilo mpaka wakafikia kutoadhini ila baada ya kuzama Jua kwa kiwango cha kuhakiki wakati wanaodai, wakachelewesha kufuturu, na wakawahisha daku, na wakaenda kinyume na sunna, na kwa hilo kheri kwao zikapungua, na zikakithiri kwao shari, tunamuomba Allah msaada.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 36) (1957). صحيح مسلم (2/ 771) (1098). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص335). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 442). خلاصة الكلام على عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص155).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tulikula daku pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama kwenda katika swala, nikasema: Ulipita muda gani baina ya adhana na daku? Akasema: Kiasi cha (kusoma) aya hamsini

عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: تَسَحَّرْنَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، ثُمَّ قَامَ إِلَى الصَّلاةِ، قُلْتُ: كَمْ كَانَ بَيْنَ الأَذَانِ وَالسَّحُورِ؟ قَالَ: قَدْرُ خَمْسِينَ آيَةً.
Kutoka kwa Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Tulikula daku pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama kwenda katika swala, nikasema: Ulipita muda gani baina ya adhana na daku? Akasema: Kiasi cha (kusoma) aya hamsini.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Walikula daku baadhi ya Maswahaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha akasimama rehema na amani ziwe juu yake kwenda katika swala ya Alfajiri. Anasi akasema kumuuliza Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake: Kulikuwa na kiwango cha muda gani baina ya adhana na kumaliza kula daku?. Akasema Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake: Kiasi cha kusoma aya hamsini za kati na kati, si ndefu wala fupi, wala si kwa kisomo cha haraka wala cha taratibu.

Mafunzo
  1. Ubora wa kuchelewesha daku mpaka kabla kidogo na Alfajiri; kwa sababu ikichelewa kunakuwa na manufaa katika mwili, na manufaa yake kwake mchana ni mengi.
  2. Pupa ya Maswahaba ya kukusanyika pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ili wajifunze kutoka kwake.
  3. Uzuri wa maisha ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Maswahaba zake, kiasi kwamba alikuwa akila pamoja nao.
  4. Wakati wa kujizuia kula ni kuchomoza kwa Alfajiri.
  5. Kauli yake: "Kulikuwa na muda gani baina ya adhana na daku", makusudio yake ni kati ya daku na kukimiwa swala, kwa kauli yake ndani ya hadihti nyingine: "Kulipita muda gani baina ya kumaliza kwao kula daku na kuingia katika swala", na hadithi hujifasiri zenyewe.
  6. Amesema Muhallab: Hapa kuna kukadiria nyakati kwa matendo ya mwili, na waarabu walikuwa wakikadiria wakati kwa matendo, kama kusema kwao: Kiasi cha kumkamua mbuzi, na kiasi cha kumchinja ngamia mnene, Zaidi bin Thabit radhi za Allah ziwe juu yake akaachana na hayo, akaenda kukadiria muda kwa kisomo cha Qur'ani; Akiashiria kuwa wakati huo ulikuwa ni wakati wa ibada ya kisomo, na lau kama wangelikuwa wakikadiria muda kwa kingine kisichokuwa matendo basi angesema kwa mfano: Kiasi cha daraja moja, au theluthi ya tano ya saa.
  7. Amesema bin Abii Jamra: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitazama ni lipi litakalokuwa na huruma zaidi kwa umma wake basi analifanya; kwa sababu lau kama asingelikula daku basi wangelimfuata, na lingewapa tabu baadhi yao, na lau angelikula daku usiku wa manane pia hilo lingewapa tabu baadhi yao miongoni mwa wale wanaozidiwa na usingizi, kwani hilo linaweza kupelekea mtu kuacha kuswali swala ya Alfajiri au akahitaji nguvu kubwa ya kukesha.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 29) (1921). صحيح مسلم (2/ 771) (1097). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص318). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (3/ 418). خلاصة الكلام على عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص147).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka

عن أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «تَسَحَّرُوا، فَإِنَّ فِي السَّحُورِ بَرَكَةً».
Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Chelewesheni kula daku, hakika katika kuchelewesha kula daku kuna baraka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kula daku, nako ni kula mwisho wa usiku ili kujiandaa kwa ajili ya swaumu; kwa sababu ndani yake kuna baraka, na kheri nyingi, yakiwemo malipo na thawabu, na kusimama katika wakati wa mwisho kwa ajili ya kuomba dua, na kupata nguvu kwa ajili ya swaumu, na kupata uchangamfu kwa ajili yake, na kupunguza uzito wake.

Mafunzo
  1. Sunna ya kula daku na kutekeleza amri ya sheria kwa kufanya hivyo.
  2. Amesema bin Hajari katika kitabu Fat-hulbaari: Baraka katika daku zinapatikana kwa namna nyingi: Nayo ni kufuata sunna na kwenda kinyume na Mayahudi na Wakristo, na kupata nguvu kutokana na daku kwa ajili ya ibada, na kuongeza uchangamfu, na kuondoa tabia mbaya inayosababishwa na njaa, na kuwa sababu ya kutoa sadaka kwa mwenye kuomba kwa wakati huo, au akajumuika pamoja naye katika chakula, na ni sababu ya kufanya dhikri na dua katika wakati ambao kuna matarajio makubwa ya kujibiwa, na kuipata nia ya kufunga kwa yule aliyejisahau kabla ya kulala.
  3. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa akioanisha hukumu kwa hukumu; ili mioyo ya watu ikunjuke, na ujulikane utukufu wa sheria.
  4. Amesema bin Hajari: Daku inapatikana kwa chochote kidogo atakachokula mtu, katika vyakula au vinywaji.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 29) (1923). صحيح مسلم (2/ 770) (1095). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص317). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 416).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com