Waislamu walikuwa wakitoa zakatul-fitiri katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na zama za makhalifa waongofu baada yake kwa mdogo na mkubwa, kiwango cha kibaba cha chakula. Na chakula chao kilikuwa ni ngano na (Zabibu): Zabibu kavu, na (samli): Maziwa yaliyokaushwa na tende. Na kiwango cha kibaba kimoja ni 'mudi' nne, na mudi moja inalingana na ujazo wa viganja viwili vya mtu aliyelingana sawa. Alipokuja Muawia radhi za Allah ziwe juu yake katika mji wa Madina akiwa Khalifa, na ngano ya Sham ilikuwa nyingi wakati huo, alitoa hotuba akasema: Hakika mimi ninaona vibaba viwili vya ngano ya Sham (ni nusu ya kibaba), vinalingana na nusu ya kibaba cha tende, watu wakalichukua hilo. Akasema Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake: Ama mimi ninaendelea kutoa kama nilivyokuwa nikitoa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake daima maishani mwangu.
- Kumebainishwa kiwango cha zakatul-fitiri katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kibaba cha chakula hata kama aina na kiwango vitatofautiana.
- Kila chakula cha binadam kinafaa kutoa zakatul-fitiri, bali zilitajwa aina nne pekee; kwa sababu ndicho kilikuwa chakula cha watu kwa zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Kutoa kisichokuwa chakula kama pesa, hakutoshelezi zakatul-fitiri.
- Amesema Nawawi katika Sherehe ya Muslim: Na wakihitilafiana Maswahaba na kukawa hakuna kauli inayoonyesha kuwa kauli ya baadhi yao ni bora kuliko nyingine, tunarejea katika dalili nyingine, tutakuta kuwa dhahiri ya hadithi na kipimo cha akili vimekwenda sambamba katika kuweka sharti la kibaba cha ngano kuwa ni sawa na vibaba vingine, hivyo ni lazima kulifanyia kazi hilo.
- Amesema bin Hajari: Na katika hadithi ya Abuu Saidi inaonyesha namna alivyokuwa na mkazo sana katika kufuata na kushikamana na mafundisho, na kuacha kuyavuka kwenda katika jitihada hali yakuwa mafundisho yapo, na katika kitendo cha Muawia na watu kuafikiana naye, ni dalili ya kufaa jitihada, nalo ni jambo zuri, lakini kukiwa na mafundisho jitihada zitakuwa mbovu na wala hazitozingatiwa.
صحيح البخاري (2/ 131) (1508). صحيح مسلم (2/ 678) (985). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص309). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 409). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 251).