Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Zakaatul Fitri.

Hadithi 2

Tulikuwa tukitoa kipindi alipokuwa nasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul fitiri, kwa kila mdogo na mkubwa, huru au mamluki, kibaba cha chakula, au kibaba cha siyagi, au kibaba cha ngano, au kibaba cha zabibu

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا نُخْرِجُ إِذْ كَانَ فِينَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ، عَنْ كُلِّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ، حُرٍّ أَوْ مَمْلُوكٍ، صَاعًا مِنْ طَعَامٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ أَقِطٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ زَبِيبٍ، فَلَمْ نَزَلْ نُخْرِجُهُ حَتَّى قَدِمَ عَلَيْنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ أَبِي سُفْيَانَ رضي الله عنه حَاجًّا، أَوْ مُعْتَمِرًا فَكَلَّمَ النَّاسَ عَلَى الْمِنْبَرِ، فَكَانَ فِيمَا كَلَّمَ بِهِ النَّاسَ أَنْ قَالَ: إِنِّي أَرَى أَنَّ مُدَّيْنِ مِنْ سَمْرَاءِ الشَّامِ، تَعْدِلُ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، فَأَخَذَ النَّاسُ بِذَلِكَ، قَالَ أَبُو سَعِيدٍ: فَأَمَّا أَنَا فَلَا أَزَالُ أُخْرِجُهُ كَمَا كُنْتُ أُخْرِجُهُ، أَبَدًا مَا عِشْتُ.
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Kudry -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa tukitoa kipindi alipokuwa nasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul fitiri, kwa kila mdogo na mkubwa, huru au mamluki, kibaba cha chakula, au kibaba cha siyagi, au kibaba cha ngano, au kibaba cha zabibu, hatukuacha kuendelea kuitoa, mpaka alipokuja kwetu Muawia bin Abii Sufian radhi za Allah ziwe juu yake kwa ajili ya Hija, au Umra, akazungumza na watu katika Mimbari, ikawa katika yale aliyozungumza na watu alisema kuwa: Hakika mimi ninaona kuwa vibaba viwili vya kipimo cha kutoka Samraa ya Sham, vinalingana na kibaba kimoja cha tende, watu wakalichukua hilo, anasema Abuu Saidi: Ama mimi niliendelea kuitoa kama nilivyokuwa nikiitoa, milele kwa muda wote nilioishi.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Waislamu walikuwa wakitoa zakatul-fitiri katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na zama za makhalifa waongofu baada yake kwa mdogo na mkubwa, kiwango cha kibaba cha chakula. Na chakula chao kilikuwa ni ngano na (Zabibu): Zabibu kavu, na (samli): Maziwa yaliyokaushwa na tende. Na kiwango cha kibaba kimoja ni 'mudi' nne, na mudi moja inalingana na ujazo wa viganja viwili vya mtu aliyelingana sawa. Alipokuja Muawia radhi za Allah ziwe juu yake katika mji wa Madina akiwa Khalifa, na ngano ya Sham ilikuwa nyingi wakati huo, alitoa hotuba akasema: Hakika mimi ninaona vibaba viwili vya ngano ya Sham (ni nusu ya kibaba), vinalingana na nusu ya kibaba cha tende, watu wakalichukua hilo. Akasema Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake: Ama mimi ninaendelea kutoa kama nilivyokuwa nikitoa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake daima maishani mwangu.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa kiwango cha zakatul-fitiri katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kibaba cha chakula hata kama aina na kiwango vitatofautiana.
  2. Kila chakula cha binadam kinafaa kutoa zakatul-fitiri, bali zilitajwa aina nne pekee; kwa sababu ndicho kilikuwa chakula cha watu kwa zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Kutoa kisichokuwa chakula kama pesa, hakutoshelezi zakatul-fitiri.
  4. Amesema Nawawi katika Sherehe ya Muslim: Na wakihitilafiana Maswahaba na kukawa hakuna kauli inayoonyesha kuwa kauli ya baadhi yao ni bora kuliko nyingine, tunarejea katika dalili nyingine, tutakuta kuwa dhahiri ya hadithi na kipimo cha akili vimekwenda sambamba katika kuweka sharti la kibaba cha ngano kuwa ni sawa na vibaba vingine, hivyo ni lazima kulifanyia kazi hilo.
  5. Amesema bin Hajari: Na katika hadithi ya Abuu Saidi inaonyesha namna alivyokuwa na mkazo sana katika kufuata na kushikamana na mafundisho, na kuacha kuyavuka kwenda katika jitihada hali yakuwa mafundisho yapo, na katika kitendo cha Muawia na watu kuafikiana naye, ni dalili ya kufaa jitihada, nalo ni jambo zuri, lakini kukiwa na mafundisho jitihada zitakuwa mbovu na wala hazitozingatiwa.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 131) (1508). صحيح مسلم (2/ 678) (985). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص309). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 409). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 251).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الفِطْرِ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، عَلَى العَبْدِ وَالحُرِّ، وَالذَّكَرِ وَالأُنْثَى، وَالصَّغِيرِ وَالكَبِيرِ مِنَ المُسْلِمِينَ، وَأَمَرَ بِهَا أَنْ تُؤَدَّى قَبْلَ خُرُوجِ النَّاسِ إِلَى الصَّلاَةِ.
Imepokelewa kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Alifaradhisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri kibaba cha tende, au kibaba cha ngano, kwa mtumwa na aliyehuru, na mwanaume na mwanamke, na mdogo na mkubwa katika waislamu, na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amewajibisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake zakatul-fitiri baada ya Ramadhani, nayo kwa kiwango cha kibaba inafikia uzito wake machoto manne. Na mudi moja: Ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati, wa tende au ngano, kwa kila muislamu; aliye huru na mtumwa, mwanaume na mwanamke, mdogo na mkubwa, na hii ni kwa yule ambaye anachakula kinachozidi kwa siku yake hiyo na usiku wake, kwake yeye na kwa wale anaowahudumia. Na akaamrisha itolewe kabla ya watu kutoka kwenda katika swala ya Iddi.

Mafunzo
  1. Zakatul-fitiri ya Ramadhani ni lazima kutolewa kwa mtoto na mkubwa, na aliye huru na mamluki, na anasemeshwa hapa msimamizi na bosi, na anaitoa mwanaume kwa niaba yake na watoto wake na wale ambao ni wajibu kwake kuwahudumia.
  2. Si wajibu zakatul-fitiri kwa kichanga kilichoko tumboni, bali inapendeza tu.
  3. Kumebainishwa kinachotolewa katika zakatul-fitiri, nakuwa ni chakula cha watu walichokizoea.
  4. Uwajibu wa kuitoa kabla ya swala ya Iddi, na bora zaidi iwe asubuhi ya siku ya Iddi, na inafaa kuitoa kabla ya Iddi kwa siku moja au mbili.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 130) (1503). صحيح مسلم (2/ 679) (986). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص309). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 406). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 249).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com