Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Ummu Atwiya Muanswari (mzaliwa wa Madina) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwakataza wanawake kusindikiza jeneza; na hii ni kwa sababu ya mitihani inayohofiwa juu yao, na uchache wa subira yao, kisha akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakutilia mkazo katika katazo hili kama anavyofanya katika matakazo mengine.
Mafunzo
Kuwakataza wanawake kusindikiza jeneza, nalo ni katazo la jumla la kulisindikiza, kuanzia linapoandaliwa na kuswaliwa, na mpaka makaburini linapozikwa.
Sababu ya katazo, ni kwa sababu wanawake hawawezi kuhimili mfano wa sehemu kama hizi zenye kuhuzunisha, na mazingira yenye kuathiri; huenda kukaonekana kwao kulalamika, na kupaparika, mambo yanayokwenda kinyume na subira inayohitajika.
Asili ya katazo huwa ni uharamu, isipokuwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alielewa kutokana na viashiria vya hali halisi kuwa katazo lao la kusindikiza jeneza si la mkazo uliosisitizwa, lakini zimekuja hadithi zilizoonyesha kutilia mkazo katika kusindikiza jeneza zaidi kuliko jinsi inavyoonyesha hadithi hii.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 78) (1278).
صحيح مسلم (2/ 646) (938).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص285).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 366).
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika maradhi yake ambayo hakuweza kuamka tena: "Amewalaani Mwenyezi Mungu Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kusalia" Akasema: Na lau kama isingekuwa kauli hiyo basi lingenyanyuliwa kaburi lake, isipokuwa ilihofiwa kufanywa kuwa mahali pa kuswalia.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema akiwa katika maradhi yake ambayo yalikuwa makali na akafariki ndani yake: Mwenyezi Mungu aliwalaani Mayahudi na Wakristo, na aliwafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa kuswalia, na hii ni kwa kuyajengea au kuswali hapo au kwa kuyaelekea. Kisha akasema radhi za Allah ziwe juu yake: Na lau kama si katazo hilo na tahadhari hiyo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na hofu ya Maswahaba kufanywa kaburi la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo kwa makaburi ya Manabii wao, basi lingedhihirishwa na kunyanyuliwa kaburi lake.
Mafunzo
Na huu ni mingoni mwa usia wake wa mwisho, jambo linaloonyesha umuhimu wake, na kuutilia maanani.
Katazo la msisitizo na uharamu mkubwa wa kuyafanya makaburi kuwa mahali pa kuswalia, na kuyaendea kwa ajili ya kuswali hapo swala isiyokuwa swala ya jeneza; huu ni upenyo wa kumtukuza maiti na kutufu (kuzunguka) katika kaburi lake, na kujifuta kwa nguzo zake (za kaburi), na kumuita kwa jina lake, na yote hayo ni katika ushirikina na ni katika njia zake.
Ukubwa wa kutilia umuhimu na kutilia maanani Mtume rehema na amani ziwe juu yake Tauhidi, na hofu yake juu ya kutukuzwa makaburi; kwa sababu hilo linapelekea katika ushirikina.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alimlinda Nabii wake amani iwe juu yake, isijekufanywa shirki juu ya kaburi lake, akawapa maono Maswahaba wake na wale wanaokuja baada yao, walilinde kaburi lake lisije kunyanyuliwa.
Maswahaba kuufanyia kazi usia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na pupa yao juu ya Tauhidi.
Katazo la kujifananisha na Mayahudi na Wakristo, na kwamba kuyajengea makaburi ni katika tamaduni zao.
Miongoni mwa aina za kuyafanya makaburi kuwa misikiti ni kuswali hapo, hata kusipojengwa msikiti.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 102) (1390).
صحيح مسلم (1/ 376) (529).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص292).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 376).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 236).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com