Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo

عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: نُهِينَا عَنِ اتِّبَاعِ الجَنَائِزِ، وَلَمْ يُعْزَمْ عَلَيْنَا.
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Ummu Atwiya Muanswari (mzaliwa wa Madina) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwakataza wanawake kusindikiza jeneza; na hii ni kwa sababu ya mitihani inayohofiwa juu yao, na uchache wa subira yao, kisha akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakutilia mkazo katika katazo hili kama anavyofanya katika matakazo mengine.

Mafunzo
  1. Kuwakataza wanawake kusindikiza jeneza, nalo ni katazo la jumla la kulisindikiza, kuanzia linapoandaliwa na kuswaliwa, na mpaka makaburini linapozikwa.
  2. Sababu ya katazo, ni kwa sababu wanawake hawawezi kuhimili mfano wa sehemu kama hizi zenye kuhuzunisha, na mazingira yenye kuathiri; huenda kukaonekana kwao kulalamika, na kupaparika, mambo yanayokwenda kinyume na subira inayohitajika.
  3. Asili ya katazo huwa ni uharamu, isipokuwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alielewa kutokana na viashiria vya hali halisi kuwa katazo lao la kusindikiza jeneza si la mkazo uliosisitizwa, lakini zimekuja hadithi zilizoonyesha kutilia mkazo katika kusindikiza jeneza zaidi kuliko jinsi inavyoonyesha hadithi hii.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 78) (1278). صحيح مسلم (2/ 646) (938). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص285). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 366).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Dalili za kimatamshi na namna ya kudadavua.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com