Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Dalili za kimatamshi na namna ya kudadavua.

Hadithi 3

Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo

عَنْ أُمِّ عَطِيَّةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: نُهِينَا عَنِ اتِّبَاعِ الجَنَائِزِ، وَلَمْ يُعْزَمْ عَلَيْنَا.
Kutoka kwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Tulikatazwa kusindikiza jeneza, na hatukusisitiziwa katazo hilo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Ummu Atwiya Muanswari (mzaliwa wa Madina) radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwakataza wanawake kusindikiza jeneza; na hii ni kwa sababu ya mitihani inayohofiwa juu yao, na uchache wa subira yao, kisha akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakutilia mkazo katika katazo hili kama anavyofanya katika matakazo mengine.

Mafunzo
  1. Kuwakataza wanawake kusindikiza jeneza, nalo ni katazo la jumla la kulisindikiza, kuanzia linapoandaliwa na kuswaliwa, na mpaka makaburini linapozikwa.
  2. Sababu ya katazo, ni kwa sababu wanawake hawawezi kuhimili mfano wa sehemu kama hizi zenye kuhuzunisha, na mazingira yenye kuathiri; huenda kukaonekana kwao kulalamika, na kupaparika, mambo yanayokwenda kinyume na subira inayohitajika.
  3. Asili ya katazo huwa ni uharamu, isipokuwa Ummu Atwiya radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake alielewa kutokana na viashiria vya hali halisi kuwa katazo lao la kusindikiza jeneza si la mkazo uliosisitizwa, lakini zimekuja hadithi zilizoonyesha kutilia mkazo katika kusindikiza jeneza zaidi kuliko jinsi inavyoonyesha hadithi hii.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 78) (1278). صحيح مسلم (2/ 646) (938). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص285). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 366).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «دَعُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ، إِنَّمَا هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بِسُؤَالِهِمْ وَاخْتِلَافِهِمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ، فَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَيْءٍ فَاجْتَنِبُوهُ، وَإِذَا أَمَرْتُكُمْ بِأَمْرٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Niacheni na vile nilivyo kuachieni, hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa sababu ya maswali mengi na kuwapinga mitume wao, hivyo, nikiwakatazeni jambo basi liepukeni, na nikiwaamrisha jambo lifanyeni kadiri muwezavyo"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hukumu za kisheria zimegawanyika sehemu tatu: Zilizonyamaziwa, na makatazo, na maamrisho. Ama ya kwanza: Nayo ni ile ambayo sheria imeinyamazia: Kiasi kwamba hakuna hukumu, nakuwa asili ya mambo huwasiyo wajibu kuyafanya; Ama katika zama zake, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, ilikuwa ni lazima kujiepusha na kuuliza juu ya jambo ambalo halijatokea kwa kuhofia kuwekewa faradhi au katazo, kwani Mwenyezi Mungu aliliacha kwa ajili ya rehema kwa waja wake, na ama baada ya kufa kwake rehema na amani za Allah zimshukie, ikiwa swali liko katika mfumo wa fatwa au kujifunza kwa yale anayoyahitaji kuhusiana na mambo ya dini basi inajuzu bali imeamrishwa kufanya hivyo, na ikiwa ni katika namna ya jeuri na kuchimbua mambo, basi haya ndio maswali yanayokusudiwa kujiepusha nayo katika Hadithi hii. Na hii ni kwa sababu huenda ikapelekea katika yale yaliyowapata Wana wa Israeli, pale walipoamrishwa kuchinja ng'ombe yeyote lau wangelichinja ng'ombe yeyote basi wangelikuwa wametekeleza amri, lakini walitia mkazo, wakakaziwa pia. Ya pili: Ni makatazo; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyaacha, na anaadhibiwa mwenye kuyafanya, ni wajibu kuyaepeuka yote. Ya tatu: Ni maamrisho; nayo ni yale anayopata malipo mwenye kuyafanya, na anaadhiwa mwenye kuyaacha, hivyo ni wajibu kuyafanya kwa kadiri ya uwezo.

Mafunzo
  1. Tunapaswa kuzingatia kile ambacho ni muhimu zaidi na kinachohitajika, na kuacha kile kisichohitajika mara moja, na tusijishughulishe na kuuliza juu ya kile ambacho hakijatokea.
  2. Ni haramu kuuliza maswali ambayo yanaweza kutatiza baadhi ya mambo, na kufungua mlango wa shaka ambayo husababisha kuhitilafiana kwingi.
  3. Amri ya kuacha makatazo yote; Kwa sababu hakuna ugumu katika kuyaacha, na ndiyo maana katazo lilikuja kwa ujumla.
  4. Amri ya kufanya kile kilichoamrishwa ni kwa kadiri ya uwezo; Kwa sababu mtu inaweza kuwa vigumu kwake kuitekeleza au akashindwa kuifanya; ndio maana amri ilikuja kuwa ifanyike kwa kadiri ya uwezo.
  5. Katazo la kuuliza maswali mengi Wanachuoni wamegawanya kuuliza katika sehemu mbili: Moja wapo: Ni maswali yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza yale anayoyahitajia mtu kuhusiana na mambo ya dini, hili limeamrishwa, na miongoni mwa aina hii ni maswali ya Maswahaba, na aina ya pili: Ni maswali yanayokuwa katika sura ya kiburi na kujikalifisha, na hii ndiyo iliyoharamishwa.
  6. Tahadhari kwa Umma huu dhidi ya kumpinga Nabii wake, kama ilivyotokea katika Umma zilizokuwa kabla yake.
  7. Maswali mengi juu ya mambo yasiyohitajika na kutofautiana na mitume ni sababu ya maangamizo, na hasa katika mambo ambayo hayawezi kufikiwa, kama vile: Masuala ya ghaibu ambayo Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayeyajua, na hali za Siku ya Kiyama.
  8. Katazo la kuuliza maswali katika mambo magumu, amesema Auzaai: Hakika Mwenyezi Mungu akitaka kumnyima mja wake baraka ya elimu, anaweka upotovu katika ulimi wake, na niliwaona watu wa namna hivyo kuwa ni watu wasio na elimu, na amesema bin Wahabi: Nilimsikia Maliki akisema: Mijadala tasa katika elimu hunaondoa nuru ya elimu katika moyo wa mtu.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 94) (7288). صحيح مسلم (2/ 975) (1337). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 236). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 181). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 268).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «ما نهيتكم عنه فاجتنبوه، وما أمرتكم به فأْتُوا منه ما استطعتم، فإنما أَهلَكَ الذين من قبلكم كثرةُ مسائلهم واختلافهم على أنبيائهم».
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ametuelekeza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye anapotukataza kitu ni wajibu kwetu kukiepuka bila kubagua, na akituamrisha chochote ni juu yetu kukifanya kwa kadiri tuwezavyo. Kisha akatutahadharisha ili tusijekuwa kama umma zilizotangulia pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao pamoja nakwenda kwao kinyume nao, akawaadhibu Mwenyezi Mungu kwa aina mbalimbali za maangamivu na adhabu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.

Mafunzo
  1. Amri ya kutekeleza maamrisho, na kuyaepuka makatazo.
  2. Katazo halikuruhusu kufanya kitu chochote miongoni mwa hivyo, na amri ikawekewa sharti la kuweza; kwasababu kuacha ni jambo linawezekana na kufanya ni jambo linahitaji uwezo wa kukileta kitendo kilichoamrishwa.
  3. Katazo la kukithirisha maswali, wameyagawanya wanachuoni maswali katika sehemu mbili: Ya kwanza: Ni yale yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza katika mambo yanayohitajika miongoni mwa mambo ya dini, haya yameamrishwa, na miongoni mwa hayo ni maswali ya maswahaba. Na ya pili: Ni yale yanayokuwa katika mfumo wa ukaidi na kulazimisha, na haya ndiyo yaliyokatazwa.
  4. Kutahadharishwa umma huu na kutokwenda kinyume na Nabii wake, kama ilivyotokea katika umma zilizokuwa kabla yake.
  5. Katazo lake linajumuisha kidogo na kingi, kwasababu haiwezi kufikia kuyaepuka makatazo ispokuwa kwa kuyaepuka yale madogo na mengi, kwa mfano: Ametukataza kula riba, katazo linajumuisha kidogo na kingi.
  6. Kuziacha sababu zote zinazopelekea katika mambo ya haramu, kwasababu kufanya hivyo ni miongoni mwa maana za kuyaepuka.
  7. Mwanadamu ana nguvu na uwezo, kwa kauli yake: "Kwa kiasi muwezavyo" ndani ya kauli hii ni jibu la madhehebu ya Jabariyya wanaosema kuwa: mwanadamu hana uwezo, kwasababu yeye amelazimishwa juu ya matendo yake, hata pale mtu anapotikisa mkono wake wakati wa mazungumzo, wanasema kutikisa mkono huku si kwa uwezo wake, bali kalazimishwa, na hakuna shaka kuwa kauli hii ni batili na inaambatana na madhara makubwa.
  8. Haitakiwi kwa mwanadamu anaposikia amri ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake aseme: Kwani hiyo ni wajibu au ni sunna? kwa kauli yake: "Lifanyeni kwa kadiri muwezavyo".
  9. Yote aliyoyaamrisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- au akayakataza basi hiyo ni sheria, swasawa hilo liwe ndani ya Qur'ani au lisiwemo, itafanyiwa kazi sunna ya ziyada katika Qu'r'ani iwe amri au katazo.
  10. Kukithirisha maswali ni sababu ya kuangamia, hasa hasa katika mambo ambayo haiwezekani kuyafikia, mfano kama maswala ya ghaibu kama majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, na hali za siku ya kiyama, usikithirishe maswali ndani yake ukaangamia, ukawa ni mtu mwenye kulazimisha mambo mwenye kujikita.
  11. Umma waliotangulia waliangamia kwa kukithiri maswali yao, na waliangamia kwa kukithiri kwenda kwao kinyume na Manabii wao.
Marejeo

-التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، مطبعة دار نشر الثقافة، الإسكندرية، الطبعة: الأولى، 1380 هـ. -شرح الأربعين النووية، للشيخ ابن عثيمين، دار الثريا للنشر. -فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، دار ابن القيم، الدمام المملكة العربية السعودية، الطبعة: الأولى، 1424هـ/2003م. -الفوائد المستنبطة من الأربعين النووية، للشيخ عبد الرحمن البراك، دار التوحيد للنشر، الرياض. -شرح الأربعين النووية، للشيخ صالح آل الشيخ، دار الحجاز، الطبعة: الثانية، 1433هـ. -الأربعون النووية وتتمتها رواية ودراية، للشيخ خالد الدبيخي، ط. مدار الوطن. -الجامع في شروح الأربعين النووية، للشيخ محمد يسري، ط. دار اليسر. -صحيح البخاري، نشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ. -صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، نشر: دار إحياء التراث العربي – بيروت.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com