Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah

عن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهُ صلَّى اللهُ عليهِ وَسَلَّم: «لَقِّنُوا مَوْتَاكُمْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Tuseme na turudie neno la kumpwekesha "Laa ilaah illa llaah" Yaani: Hapana mola apasaye kuabudiwwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, wakati wa kufikwa kwake na tabu za kifo mpaka aliseme, ili liwe neno lake la mwisho.

Mafunzo
  1. Sunna ya kumtamkisha aliyefikwa na mauti.
  2. Inachukiza kukariri sana kumtamkisha aliyefikwa na umauti, na kumlazimisha endapo atalitamka, au ikafahamika kuwa ametamka; ili wasimsumbue akatamka maneno yasiyofaa.
  3. Amesema Nawawi: Na akilitamka mara moja basi asilikariri tena isipokuwa kama atatamka baada yake maneno mengine, hapo litarudiwa tena ili liwe neno lake la mwisho.
  4. Hadithi inakusanya kuhudhuria mbele ya aliyefikwa na umauti ili kumkumbusha na kumliwaza na kumfunga macho na kusimamia haki zake.
  5. Si sheria kumtamkisha mtu baada ya kifo na kaburini baada ya mazishi; kwa sababu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutolifanya hilo.
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 631) (916). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 569).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Mauti na Hukumu zake.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com