Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mauti na Hukumu zake.

Hadithi 4

hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo

عَن أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: وَجِعَ أَبُو مُوسَى وَجَعًا شَدِيدًا، فَغُشِيَ عَلَيْهِ وَرَأْسُهُ فِي حَجْرِ امْرَأَةٍ مِنْ أَهْلِهِ، فَلَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يَرُدَّ عَلَيْهَا شَيْئًا، فَلَمَّا أَفَاقَ، قَالَ: أَنَا بَرِيءٌ مِمَّنْ بَرِئَ مِنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَرِئَ مِنَ الصَّالِقَةِ وَالحَالِقَةِ وَالشَّاقَّةِ.
Kutoka kwa Abuu Burda bin Abii Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliumia Abuu Mussa maumivu makali, akazimia na kichwa chake kikiwa katika paja la mwanamke katika wake zake, akawa hakuweza kumjibu chochote, alipozinduka, akasema: Mimi najitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amesimulia Abuu Burda radhi za Allah ziwe juu yake kuwa baba yake Abuu Mussa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake aliugua maradhi makali, akazimia, na kichwa chake kilikuwa katika paja la mwanamke mmoja katika wake zake, akapiga mayowe yule mwanamke kwa kumuita, akawa hakuweza kumjibu chochote kwa sababu ya kuzimia kwake. Alipozinduka akasema kuwa: Hakika yeye anajitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alijitenga naye. Mpiga mayowe: Naye ni mwanamke anayenyanyua sauti yake wakati wa msiba. Na mnyoaji: Ni mwanamke anayenyoa nywele zake wakati wa msiba. Na mchana nguo: Ni mwanamke anayechana nguo zake wakati wa msiba. Kwa sababu haya ni katika mambo ya zama za ujinga, bali aliamrisha kuwa na subira wakati wa msiba, na kutaraji malipo yake kwa Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Katazo la kuchana nguo, na kunyoa nywele, na kunyanyua sauti wakati wa kutokea misiba, nakuwa hilo ni katika madhambi makubwa.
  2. Huzuni na kulia pasina maombolezo na kunyanyua sauti si haramu, hili halipingani na subira juu ya maamuzi ya Mwenyezi Mungu, bali ni rehema.
  3. Uharamu wa kulalamika katika makadirio ya Mwenyezi Mungu yenye kuumiza kwa kauli au vitendo.
  4. Uwajibu wa kuwa na subira wakati wa misiba.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 81) (1296). صحيح مسلم (1/ 100) (104). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص287). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 371).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza

عن عائشة رضي الله عنها قالت: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «لَا تَسُبُّوا الْأَمْوَاتَ، فَإِنَّهُمْ قَدْ أَفْضَوْا إِلَى مَا قَدَّمُوا».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- uharamu wa kuwatukana wafu na kuchafua heshima zao, nakuwa hili ni katika tabia mbaya, kwani wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza katika matendo mazuri au mabaya, kama ambavyo matusi haya hayawafikii basi hakuna lolote zaidi ya kuwaudhi waliohai.

Mafunzo
  1. Hadithi ni ushahidi wa uharamu wa kuwatukana wafu.
  2. Kuacha kuwatukana wafu kuna kuchunga masilahi ya waliohai, na kuhifadhi amani ya jamii kutokana na kutotiliana vinyongo na chuki.
  3. Hekima ya kukatazwa kuwatukana nikuwa tayari wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza, kuwatukana hakusaidii, na kuna kuwaudhi ndugu zake wa karibu.
  4. Nikuwa haifai kwa mwanadamu kusema maneno yasiyo na manufaa.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 104) (1393). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 631). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (4/ 385). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (3/ 277).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile

عَنْ مَطَرِ بْنِ عُكَامِسٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا قَضَى اللَّهُ لِعَبْدٍ أَنْ يَمُوتَ بِأَرْضٍ جَعَلَ لَهُ إِلَيْهَا حَاجَةً».
Imepokelewa kutoka kwa Matwar Bin Ukaamis -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile."
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu akimpangia mtu kuwa afie katika ardhi fulani na hali yakuwa yeye hayupo katika ardhi hiyo; Basi humfanya ahitajie kitu katika ardhi ile hivyo ataenda katika ardhi ile, basi huchukuliwa roho yake akiwa huko.

Mafunzo
  1. Hadithi inathibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na nafsi haijui itafia katika ardhi gani."
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 23) (2146)، تحفة الأحوذي (6/ 299).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah

عن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ رَضِيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهُ صلَّى اللهُ عليهِ وَسَلَّم: «لَقِّنُوا مَوْتَاكُمْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Tuseme na turudie neno la kumpwekesha "Laa ilaah illa llaah" Yaani: Hapana mola apasaye kuabudiwwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, wakati wa kufikwa kwake na tabu za kifo mpaka aliseme, ili liwe neno lake la mwisho.

Mafunzo
  1. Sunna ya kumtamkisha aliyefikwa na mauti.
  2. Inachukiza kukariri sana kumtamkisha aliyefikwa na umauti, na kumlazimisha endapo atalitamka, au ikafahamika kuwa ametamka; ili wasimsumbue akatamka maneno yasiyofaa.
  3. Amesema Nawawi: Na akilitamka mara moja basi asilikariri tena isipokuwa kama atatamka baada yake maneno mengine, hapo litarudiwa tena ili liwe neno lake la mwisho.
  4. Hadithi inakusanya kuhudhuria mbele ya aliyefikwa na umauti ili kumkumbusha na kumliwaza na kumfunga macho na kusimamia haki zake.
  5. Si sheria kumtamkisha mtu baada ya kifo na kaburini baada ya mazishi; kwa sababu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutolifanya hilo.
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 631) (916). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 569).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com