Siku moja alisali Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya Alfajiri, kisha akauliza: Je, fulani kahudhuria nasi swala yetu hii? Maswahaba wakasema: Hapana. Kisha akasema: Hivi fulani kahudhuria? kwa mtu mwingine, wakasema: Hapana. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika swala ya Alfajiri na Ishaa ni swala nzito kwa wanafiki; kwa sababu ya kuzidi kwa uvivu katika nyakati hizi, na ni kwa sababu ya uchache wa kutoonekana kwa watu, kwa sababu gizani hawaonekani. Na lau kama mngejua enyi waumini yaliyomo ndani ya swala hizi mbili Alfajiri na Ishaa katika malipo na thawabu za ziada, kwa sababu malipo huwa kwa kadiri ya tabu, basi mgeziendea hata kwa kutambaa na kwa kutembea kwa mikono na magoti. Na hakika safu ya kwanza katika ukaribu wake na imam ni kama safu za Malaika ukaribu wake na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na lau waumini wangelijua ni zipi fadhila za safu ya kwanza basi wangeshindana kuiwahi, Hakika swala ya mtu na mtu mwingine inamalipo makubwa na ina athari kubwa kuliko swala yake peke yake, na swala yake pamoja na watu wawili ni bora kuliko swala yake na mtu mmoja, Na swala ambayo waswaliji watakuwa wengi hiyo ndio swala bora inayopendeka kwa Mwenyezi Mungu.
- Sheria ya imam wa msikiti kukagua hali za waumini, na kumuulizia asiyekuwepo.
- Kudumu na swala ya jamaa, na hasa hasa swala ya Ishaa na Alfajiri ni katika alama za imani.
- Ukubwa wa malipo ya swala mbili, Ishaa na Alfajiri; kwa sababu kuziendea kunahitaji kupambana na nafsi na kuwa na subira katika utiifu, ikawa malipo yake ni makubwa kuliko swala zingine.
- Swala ya jamaa inakamilika kwa kuanzia watu wawili na zaidi.
- Kumebainishwa fadhila za safu ya kwanza, na himizo la kuiendea haraka.
- Fadhila za wingi wa jamaa, kwani kila wingi unavyokithiri pia malipo huwa mengi.
- Amali njema hutofautiana ubora kulingana na kuzidiana sheria yake, na hali zake maalum.
سنن أبي داود (1/ 415) (554). سنن النسائي (2/ 104) (843). مسند أحمد (35/ 188) (21265). شرح الطيبي على مشكاة المصابيح، لشرف الدين الطيبي (4/ 1132). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (3/ 838). سبل السلام شرح بلوغ المرام، للصنعاني (1/ 360 ). شرح سنن أبي داود، لعبد المحسن العباد (40/ 11).