Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ubora wa Swala ya Jamaa na Hukumu zake.

Hadithi 9

Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «صَلَاةُ الرَّجُلِ فِي جَمَاعَةٍ تَزِيدُ عَلَى صَلَاتِهِ فِي بَيْتِهِ وَصَلَاتِهِ فِي سُوقِهِ بِضْعًا وَعِشْرِينَ دَرَجَةً، وَذَلِكَ أَنَّ أَحَدَهُمْ إِذَا تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ، ثُمَّ أَتَى الْمَسْجِدَ لَا يَنْهَزُهُ إِلَّا الصَّلَاةُ، لَا يُرِيدُ إِلَّا الصَّلَاةَ، فَلَمْ يَخْطُ خَطْوَةً إِلَّا رُفِعَ لَهُ بِهَا دَرَجَةٌ، وَحُطَّ عَنْهُ بِهَا خَطِيئَةٌ، حَتَّى يَدْخُلَ الْمَسْجِدَ، فَإِذَا دَخَلَ الْمَسْجِدَ كَانَ فِي الصَّلَاةِ مَا كَانَتِ الصَّلَاةُ هِيَ تَحْبِسُهُ، وَالْمَلَائِكَةُ يُصَلُّونَ عَلَى أَحَدِكُمْ مَا دَامَ فِي مَجْلِسِهِ الَّذِي صَلَّى فِيهِ، يَقُولُونَ: اللهُمَّ ارْحَمْهُ، اللهُمَّ اغْفِرْ لَهُ، اللهُمَّ تُبْ عَلَيْهِ، مَا لَمْ يُؤْذِ فِيهِ، مَا لَمْ يُحْدِثْ فِيهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini, na hii ni pale mmoja wao atakapo tawadha na akaufanya vizuri udhu, kisha akaenda msikitini hakusudii kwa kwenda kwake ila swala, hakuna kinachomnyanyua isipokuwa swala, basi hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa daraja kwa hatua hiyo, na atasamehewa makosa kwa hatua hiyo mpaka atakapoingia msikitini, na anapoingia msikitini huhesabika kuwa yuko ndani ya swala madamu swala ndio bado inayomzuia kutoka, na Malaika humuombea rehema mmoja wenu madamu akiwa bado kakaa mahala aliposwali, wakisema: Ewe Mola wetu muhurumie, Ewe Mola wetu msamehe, Ewe Mwenyezi Mungu mkubalie msamaha wake, wanaendelea kufanya hivyo kwa muda atakaokuwa hajafanya maudhi yoyote, na madam hajatengua udhu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakaposwali muislamu katika jamaa, swala yake hiyo itakuwa bora kuliko swala yake nyumbani kwake au sokoni kwake kwa zaidi ya mara ishirini. Kisha akaeleza sababu ya hilo: Nayo nikuwa mtu atakapotawadha akatimiza vizuri udhu na ukaufanya vizuri, kisha akatoka kwenda Msikitini hakuna kinachomtoa ila kukusudia kusali, hatopiga hatua yoyote isipokuwa atanyanyuliwa kwa hatua hiyo daraja na nafasi ya juu, na hufutiwa kwake kwa hatua hiyo makosa, Atakapoingia Msikitini na akakaa akisubiri swala, basi atapata malipo ya swala na thawabu zake kwa muda wote atakaokaa akisubiri swala, na Malaika wakimuombea akiwa katika kikao chake aliposwalia, wakisema: "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe, ewe Mwenyezi Mungu muhurumie, ewe Mwenyezi Mungu mfutie makosa" Huendelea kumuombea madam hajaharibu udhu wake, au akafanya yanayowakera watu au Malaika.

Mafunzo
  1. Swala ya mtu mmoja nyumbani kwake au sokoni kwake ni sahihi, lakini atapata dhambi kwa kuacha swala ya jamaa bila udhuru.
  2. Swala ya jamaa Msikitni ni bora kuliko swala ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na tano au sita.
  3. Miongoni mwa kazi za Malaika ni kuwaombea waumini.
  4. Ubora wa kwenda Msikitni pamoja na udhu.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 103) (477). صحيح مسلم (1/ 459) (649). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 26). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 178). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 72). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص15). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 43). المعجم الوسيط (1/ 60).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ أَكَلَ ثُومًا أَوْ بَصَلًا، فَلْيَعْتَزِلْنَا -أَوْ قَالَ: فَلْيَعْتَزِلْ- مَسْجِدَنَا، وَلْيَقْعُدْ فِي بَيْتِهِ»، وَأَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِقِدْرٍ فِيهِ خَضِرَاتٌ مِنْ بُقُولٍ، فَوَجَدَ لَهَا رِيحًا، فَسَأَلَ فَأُخْبِرَ بِمَا فِيهَا مِنَ البُقُولِ، فَقَالَ قَرِّبُوهَا إِلَى بَعْضِ أَصْحَابِهِ كَانَ مَعَهُ، فَلَمَّا رَآهُ كَرِهَ أَكْلَهَا، قَالَ: «كُلْ فَإِنِّي أُنَاجِي مَنْ لاَ تُنَاجِي». ولِمُسْلِمٍ عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ أَكَلَ مِنْ هَذِهِ الْبَقْلَةِ، الثُّومِ - وقَالَ مَرَّةً: مَنْ أَكَلَ الْبَصَلَ وَالثُّومَ وَالْكُرَّاثَ فَلَا يَقْرَبَنَّ مَسْجِدَنَا، فَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ تَتَأَذَّى مِمَّا يَتَأَذَّى مِنْهُ بَنُو آدَمَ».
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake", Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliletewa chungu kikiwa na mbogamboga, akakuta zinaharufu, akauliza akaelezwa kilichomo katika mboga hizo, akasema: Wapewe baadhi ya Maswahaba zake aliokuwa nao, alipoiona hakupendezwa nayo, akasema: "Kula kwani mimi ninanong'ona na yule usiyenong'ona naye". Na kwa Muslim kutoka kwa Jabiri bin Abdillah, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: “Mwenye kula katika mboga hii, kitunguu saumu." – na mara nyingine alisema: "Mwenye kula kitunguu maji, na kitunguu saumu – asiukaribie msikiti wetu; Kwani hakika Malaika wanaudhika kwa yale ambayo wanadamu wanaudhika nayo.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekula kitunguu saumu au kitunguu maji asije msikitini, ili asiwaudhi ndugu zake katika wale wanaohudhuria swala ya jamaa kwa harufu yake, nalo ni katazo la kiusafi la kutokuja msikitini, na si katazo la kula; kwa sababu ni katika vyakula vya halali, na aliletewa Mtume rehema na amani ziwe juu yake chungu kikiwa na mbogamboga, aliponusa ndani yake harufu au alipoambiwa kilichomo, alikataa kula, na akakisogeza kwa baadhi ya Maswahaba zake akasema: Kula; kwani mimi husema na Malaika kwa wahyi. Na akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hukereka na harufu mbaya, kama wanavyokereka watu kwa harufu hiyo.

Mafunzo
  1. Katazo la kuja msikitini kwa atakayekula kitunguu saumu, au kitunguu maji, au chochote chenye harufu mbaya.
  2. Inaunganishwa na mambo haya, kila chenye harufu mbaya kinachowakera wenye kuswali, kama harufu ya sigara na tumbaku ugoro na mfano wa hivyo.
  3. Sababu ya kukatazwa ni harufu, ikiondoka kwa kupikwa sana au kwa kinginecho; basi chukizo litaondoka.
  4. Chukizo la kula vitu hivi kwa mwenye ulazima wa kuhudhuria swala msikitni; ili jamaa isimpite msikitini, madam hajavila kwa hila ya kukwepa kuhudhuria swala ya jamaa, hapa itakuwa ni haramu.
  5. Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukataa kula kitunguu saumu na mfano wake, si kwa ajili ya kuharamisha, bali ni kwa sababu ya mazungumzo yake na Jibril amani iwe juu yake.
  6. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba hukumu anaiambatanisha na sababu yake; ili mkusudiwa atulizane kwa kujua hekima.
  7. Amesema Al-qadhi: Na wanachuoni wametumia kipimo hiki kwa maeneo yote yanayowakusanya watu kwa ajili swala kama viwanja vya Idd na jeneza na mfano wake katika sehemu zinazowakusanya watu kwa ajili ya ibada, na vile vile sehemu wanazokusanyika kwa ajili ya elimu na kumtaja Mwenyezi Mungu na sherehe mbali mbali na mfano wake, isipokuwa masoko na mfano wake hayaingii hapa.
  8. Wamesema wanachuoni: Na katika hadithi hii kuna dalili ya kukataza kula kitunguu saumu na mfano wake wakati wa kuingia msikitini, hata kama pakiwa hakuna mtu ndani yake, kwa sababu ni mahala pa Malaika, na kwa ujumla wa maelekezo ya hadithi.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 170) (855). صحيح مسلم (1/ 394) (564)، (1/ 395) (564). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص204). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 260). تاج العروس من جواهر القاموس، للزَّبيدي (5/ 332).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ غَدَا إِلَى الْمَسْجِدِ أَوْ رَاحَ أَعَدَّ اللهُ لَهُ فِي الْجَنَّةِ نُزُلًا، كُلَّمَا غَدَا أَوْ رَاحَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amempa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kwenda msikitini kwa ajili ya ibada au elimu kwa lengo jingine katika mambo ya kheri katika wakati wowote; mwanzo wa mchana au mwisho wake kuwa Mwenyezi Mungu amemuandalia mahali na takrima ya ugeni peponi, kila anapokuja msikitini usiku au mchana.

Mafunzo
  1. Fadhila za kwenda msikitini, na himizo la kuhifadhi swala ya jamaa ndani ya msikiti, kwani anapitwa na daraja ngapi mwenye kukwepa kwenda msikitini na kheri na fadhila na malipo na ugeni aliouandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwenye kwenda katika nyumba yake.
  2. Ikiwa watu humkirimu anayewajia katika majumba yao, na kumletea chakula, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mkarimu zaidi kuliko viumbe wake! Yeyote atakayekwenda katika nyumba yake basi atamkirimu, na Mwenyezi Mungu atamuandalia mafikio ya thamani na yenye nafasi kubwa.
  3. Furaha na moyo mkunjufu wakati wa kwenda msikitini; kwa sababu anaandaliwa makazi kila anapokwenda asubuhi au mchana kwa idadi ya kwenda kwake.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 133) (662). صحيح مسلم (1/ 463) (669). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 153). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 166). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 204).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri

عَن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «تَفْضُلُ صَلاَةُ الجَمِيعِ صَلاَةَ أَحَدِكُمْ وَحْدَهُ، بِخَمْسٍ وَعِشْرِينَ جُزْءًا، وَتَجْتَمِعُ مَلاَئِكَةُ اللَّيْلِ وَمَلاَئِكَةُ النَّهَارِ فِي صَلاَةِ الفَجْرِ» ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ: فَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: {إِنَّ قُرْآنَ الفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا} [الإسراء: 78].
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri" Kisha anasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba thawabu na malipo ya swala ya mtu katika jamaa pamoja na imamu ni bora kuliko swala ishirini na tano anazoziswali peke yake nyumbani kwake au sokoni kwake, kisha akataja rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa usiku na mchana hukusanyika katika swala ya Alfajiri, kisha anasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake akitoa ushahidi kwa hilo: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78] Yaani: Qur'ani ya Alfajiri huishuhudia Malaika wa usiku na Malaika wa mchana.

Mafunzo
  1. Amesema bin Hajari: Hakika swala ya msikitini kwa jamaa inazidi swala ya nyumbani na sokoni kwa jamaa au mtu mmoja mmoja, ameisema kauli hiyo bin Daqiiq Al-Idd.
  2. Hapa kuna fadhila ya swala ya Alfajiri; kwa kufanywa pekee kukusanyika kwa Malaika ndani yake.
  3. Amesema bin Bazi: Ni wajibu kwa muumini awe na pupa ya kuhifadhi swala katika jamaa hata kama nyumba yake itakuwa mbali, ili aipate kheri hii kubwa.
  4. Amesema Nawawi katika kukusanya kati ya riwaya ya kwamba swala ya jamaa ni bora kuliko swala ya mtu mmoja kwa daraja ishirini na tano, na nyingine kwa daraja ishirini na saba: Na kukusanya kati ya kauli hizi mbili ni kwa sura tatu: Ya kwanza: Hazipingani, kwani kutajwa kidogo hakupingani na wingi, na maana ya idadi haizingatiwi kwa wasomi wa misingi ya sheria. Ya pili: Yawezekana alieleza kidogo kisha Allah Mtukufu akamjulisha ziada ya fadhila, naye akaieleza. Ya tatu: Nikuwa zinatofautiana kulingana na kutofautiana kwa wenye kuswali, baadhi yao wanakuwa na ishirini na tano, na baadhi yao ishirini na saba kulingana na ukamilifu wa swala na kuihifadhi kwake na muonekano wake na utulivu wake na wingi wa mkusanyiko wake na ubora wao na utukufu wa eneo na mfano wa hayo, na Allah ndiye mjuzi zaidi.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 131) (648). صحيح مسلم (1/ 450) (649). تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان، لعبد الرحمن آل سعدي (ص464). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 210).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Je, wasikia wito wa swala?" Akasema: Naam, akasema: "Basi ujibu

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ أَعْمَى، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّهُ لَيْسَ لِي قَائِدٌ يَقُودُنِي إِلَى الْمَسْجِدِ، فَسَأَلَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُرَخِّصَ لَهُ فَيُصَلِّيَ فِي بَيْتِهِ، فَرَخَّصَ لَهُ، فَلَمَّا وَلَّى دَعَاهُ، فَقَالَ: «هَلْ تَسْمَعُ النِّدَاءَ بِالصَّلَاةِ؟» فَقَالَ: نَعَمْ، قَالَ: «فَأَجِبْ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi sina muongozaji wa kunileta msikitini, akamuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amruhusu asali nyumbani kwake, akamruhusu, alipoondoka akamuita, akasema: "Je, wasikia wito wa swala?" Akasema: Naam, akasema: "Basi ujibu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Mtu mmoja kipofu alimjia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi sina wa kunisaidia na kunishika mkono kuja msikitini, katika swala tano, akitaka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amruhusu, alipompa mgongo alimuita na akasema: Je, unasikia adhana ya swala? akasema: Ndiyo, akasema: Basi mjibu anayenadi kwa ajili ya swala.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa swala ya jamaa; kwa sababu kutaka ruhusa huwa hakuwi ila kwa jambo la lazima.
  2. Kauli yake: "Mjibu" Kwa mwenye kusikia wito inaonyesha kuwa swala ya pamoja ni lazima; kwa sababu asili ya amri ni wajibu.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 452) (653). شرح النووي على مسلم (5/ 155). فتح ذي الجلال والإكرام، شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 254).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Safu bora kwa wanaume ni safu ya kwanza, na safu yenye shari ni ya nyuma, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho na yenye shari ni safu ya mwanzo

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «خَيْرُ صُفُوفِ الرِّجَالِ أَوَّلُهَا، وَشَرُّهَا آخِرُهَا، وَخَيْرُ صُفُوفِ النِّسَاءِ آخِرُهَا، وَشَرُّهَا أَوَّلُهَا».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Safu bora kwa wanaume ni safu ya kwanza, na safu yenye shari ni ya nyuma, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho na yenye shari ni safu ya mwanzo"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa safu bora kwa wanaume katika swala na yenye malipo makubwa na fadhila kubwa ni ya kwanza; kwakuwa watu wanakuwa karibu na imam na pia kusikiliza kisomo chake nakuwa kwao mbali na wanawake, na ya shari na yenye malipo na fadhila ndogo na iliyombali na matakwa ya sheria ni ya mwisho, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho; kwa sababu ndio inayowasitiri vizuri kwao, na iko mbali na kuchanganyikana na wanaume na macho yao na kufitinika nao, na safu ya shari ni ya kwanza; kwakuwa inakuwa karibu na wanaume na ni kujitia katika fitina.

Mafunzo
  1. Amewahimiza wanaume kufanya haraka kwenda katika ibada mbalimbali na safu ya kwanza katika swala.
  2. Inafaa wanawake kuswali msikitini pamoja na wanaume katika safu zao binafsi, lakini kwa kujistiri na kujiheshimu.
  3. Wanawake wakikusanyika msikitini, basi wanatakiwa wapange safu, kama safu za wanaume, na wala wasitengane, bali wanatakiwa kushikana katika safu na kuziba nyufa, kama ilivyo katika safu za wanaume.
  4. Kumebainishwa namna sheria ilivyotilia umuhimu kwa kuhimiza kujiweka mbali wanawake na wanaume mpaka katika mahali pa ibada.
  5. Kutofautiana kwa watu ni kwa sababu ya matendo yao.
  6. Amesema Nawawi: Ama safu za wanaume kwa ujumla wake bora zaidi kuliko zote ni ile ya kwanza, na mbaya zaidi ni safu za mwisho, na ama safu za wanawake kilichokusudiwa katika hadithi ni: Safu za wanawake wanaoswali pamoja na wanaume, lakini wakiswali kwa peke yao na si pamoja na wanaume, basi hapo ni kama wanaume; safu yao bora zaidi ni safu ya kwanza na ya shari zaidi ni ya mwisho.
  7. Amesema Nawawi: Safu ya kwanza iliyosifiwa zikaja fadhila zake katika hadithi na kuihimiza ni safu inayofuata nyuma ya imam; sawa sawa mtu aje mapema au kwa kuchelewa, na sawa iwe kamili au pungufu na mfano wake au la.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 326) (440). سبل السلام شرح بلوغ المرام، للصنعاني (1/ 374 ). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 495). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 272). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للتبريزي (3/ 851).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti

عن أُبيِّ بن كعبٍ رضي الله عنه قال: صلَّى بنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يومًا الصُّبحَ فقال: «أشاهِد فُلان؟» قالوا: لا، قال: «أشاهِدٌ فُلان؟» قالوا: لا، قال: «إنَّ هاتيَنِ الصَّلاتين أثقَلُ الصَّلَواتِ على المُنافقين، ولو تعلمون ما فيهما لأتيتُمُوهما ولو حَبْوًا على الرُّكب، وإن الصفَّ الأوّلَ على مِثلِ صَفِّ الملائكة، ولو عَلِمتُم ما فضيلتُه لابتَدَرتُموهُ، وإنّ صلاةَ الرجل مع الرجل أزكى من صلاتِه وحدَه، وصلاتَه مع الرجلَين أزكى من صلاتِه مع الرجل، وما كَثُرَ فهو أحبُّ إلى الله تعالى».
Kutoka kwa Ubai bin Ka'ab radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya asubuhi, akasema: "Hivi fulani yupo", Wakasema: Hapana, akasema: "Na je fulani yupo?", Wakasema: Hapana: Akasema: "Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti, na hakika safu ya kwanza iko katika mithili ya safu ya Malaika, na laiti mngejua ni zipi fadhila zake basi mngezijia haraka mno, na hakika swala ya mtu na mwenzie ni safi zaidi kuliko swala yake peke yake, na swala yake akiwa na watu wawili ni nzuri zaidi kuliko swala yake na mtu mmoja, na wingi unavyozidi ndio unaopendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Siku moja alisali Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala ya Alfajiri, kisha akauliza: Je, fulani kahudhuria nasi swala yetu hii? Maswahaba wakasema: Hapana. Kisha akasema: Hivi fulani kahudhuria? kwa mtu mwingine, wakasema: Hapana. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika swala ya Alfajiri na Ishaa ni swala nzito kwa wanafiki; kwa sababu ya kuzidi kwa uvivu katika nyakati hizi, na ni kwa sababu ya uchache wa kutoonekana kwa watu, kwa sababu gizani hawaonekani. Na lau kama mngejua enyi waumini yaliyomo ndani ya swala hizi mbili Alfajiri na Ishaa katika malipo na thawabu za ziada, kwa sababu malipo huwa kwa kadiri ya tabu, basi mgeziendea hata kwa kutambaa na kwa kutembea kwa mikono na magoti. Na hakika safu ya kwanza katika ukaribu wake na imam ni kama safu za Malaika ukaribu wake na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na lau waumini wangelijua ni zipi fadhila za safu ya kwanza basi wangeshindana kuiwahi, Hakika swala ya mtu na mtu mwingine inamalipo makubwa na ina athari kubwa kuliko swala yake peke yake, na swala yake pamoja na watu wawili ni bora kuliko swala yake na mtu mmoja, Na swala ambayo waswaliji watakuwa wengi hiyo ndio swala bora inayopendeka kwa Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Sheria ya imam wa msikiti kukagua hali za waumini, na kumuulizia asiyekuwepo.
  2. Kudumu na swala ya jamaa, na hasa hasa swala ya Ishaa na Alfajiri ni katika alama za imani.
  3. Ukubwa wa malipo ya swala mbili, Ishaa na Alfajiri; kwa sababu kuziendea kunahitaji kupambana na nafsi na kuwa na subira katika utiifu, ikawa malipo yake ni makubwa kuliko swala zingine.
  4. Swala ya jamaa inakamilika kwa kuanzia watu wawili na zaidi.
  5. Kumebainishwa fadhila za safu ya kwanza, na himizo la kuiendea haraka.
  6. Fadhila za wingi wa jamaa, kwani kila wingi unavyokithiri pia malipo huwa mengi.
  7. Amali njema hutofautiana ubora kulingana na kuzidiana sheria yake, na hali zake maalum.
Marejeo

سنن أبي داود (1/ 415) (554). سنن النسائي (2/ 104) (843). مسند أحمد (35/ 188) (21265). شرح الطيبي على مشكاة المصابيح، لشرف الدين الطيبي (4/ 1132). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (3/ 838). سبل السلام شرح بلوغ المرام، للصنعاني (1/ 360 ). شرح سنن أبي داود، لعبد المحسن العباد (40/ 11).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Timizeni safu ya mbele, kisha inayofuata, na kama kuna mapungufu basi yawe katika safu ya mwisho

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَتِمُّوا الصَّفَّ المُقَدَّمَ، ثُمَّ الَّذِي يَلِيهِ، فَمَا كَانَ مِنْ نَقْصٍ فَلْيَكُنْ فِي الصَّفِّ المُؤَخَّرِ».
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Timizeni safu ya mbele, kisha inayofuata, na kama kuna mapungufu basi yawe katika safu ya mwisho".
Imepokelewa na Abu Daud na NasaiDarajaSahihi
Maelezo

Amewaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume wenye kuswali kwa pamoja kukamilisha safu ya kwanza, kisha kukamilisha safu inayofuata, na kuendelea, na yakipatikana mapungufu katika safu basi yawe mapungufu haya katika safu ya mwisho.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa sunna katika kulinganisha sawa safu.
  2. Kwa wenye kuswali basi wasiache mapungufu katika safu ya mbele, bali yawe mapungufu katika safu ya nyuma.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 10) (671). سنن النسائي (2/ 93) (818). شرح سنن أبي داود للعباد (89/ 25).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 9
Hadithi 9
  1. Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini
  2. Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake
  3. Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni
  4. Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri
  5. Je, wasikia wito wa swala?" Akasema: Naam, akasema: "Basi ujibu
  6. Safu bora kwa wanaume ni safu ya kwanza, na safu yenye shari ni ya nyuma, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho na yenye shari ni safu ya mwanzo
  7. Hakika swala hizi mbili, ni swala nzito sana kwa wanafiki, na lau kama mngejua malipo yaliyomo basi mngezijia, hata kwa kutambaa kwa magoti
  8. Timizeni safu ya mbele, kisha inayofuata, na kama kuna mapungufu basi yawe katika safu ya mwisho
  9. Itakapokimiwa swala basi hakuna swala nyingine isipokuwa swala ya faradhi

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com