Aliwatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wale wanaonyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala wakati wa dua au kinginecho, kisha karipio lake likawa kali na akatangaza adhabu rehema na amani ziwe juu yake kwa wanaofanya hivyo kwamba yanahofiwa macho yao kupofuliwa na yakanyakuliwa kwa haraka kwa namna wasiyoitarajia, wakajikuta tayari wamepoteza neema ya macho.
- Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kubainisha kwake haki; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake hakumtaja mkosefu; kwa sababu lengo ni kubainisha haki na tayari imekwisha tendeka; na kwa sababu ndani yake kuna kumsitiri mkosefu na inahamasisha zaidi mtu kukubali ukweli.
- Katazo la msisitizo, na ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua macho yake juu mbinguni ndani ya swala.
- Amesema katika kitabu cha Aunul Ma'buud: Na sababu katika hilo ni kwamba atakaponyanyua macho yake juu mbinguni atakuwa katoka katika nembo ya kibla na ameipuuza na katoka katika muonekano wa swala pia.
- Kunyanyua macho kunaondoa utulivu ndani ya swala.
- Ukubwa wa hadhi ya swala, na kwamba ni wajibu kwa wenye kusali wawe katika adabu kamili pamoja na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
صحيح البخاري (1/ 150) (750). كشاف القناع عن متن الإقناع، لمنصور بن يونس البهوتي (2/ 404). توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 101). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 587). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة قاسم (2/ 159).