Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Makosa ya wenye kusali.

Hadithi 5

Hakuna swala chakula kinapokuwa tayari, na wala hakuna (swala) akiwa anazuia na kubana vichafu viwili(Haja kubwa na ndogo)

عن عَائِشَةَ رضيَ الله عنها قالت: إِنِّي سمعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول: «لَا صَلَاةَ بِحَضْرَةِ الطَّعَامِ، وَلَا هُوَ يُدَافِعُهُ الْأَخْبَثَانِ».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna swala chakula kinapokuwa tayari, na wala hakuna (swala) akiwa anazuia na kubana vichafu viwili(Haja kubwa na ndogo)".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuswali kinapotengwa chakula kile anachokitamani mwenye kuswali, na moyo wake umefungamana nacho. Na vile vile amekataza kuswali mtu akiwa anazuia haja mbili -nazo ni mkojo na haja kubwa-, kwakuwa atashughulika na kuzuia udhia.

Mafunzo
  1. Ni lazima kwa mwenye kusali aweke mbali kila chenye kumshughulisha katika swala yake kabla ya kuingia ndani ya swala.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 393) (560). شرح النووي على مسلم (5/ 46). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص96). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 123).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hivi wana nini watu! wananyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala zao", ikazidi ukali kauli yake katika hilo, mpaka akasema: "Hakika, ni ima waache kufanya hivyo, au yatapofuliwa macho yao

عَن أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا بَالُ أَقْوَامٍ يَرْفَعُونَ أَبْصَارَهُمْ إِلَى السَّمَاءِ فِي صَلاَتِهِمْ»، فَاشْتَدَّ قَوْلُهُ فِي ذَلِكَ، حَتَّى قَالَ: «لَيَنْتَهُنَّ عَنْ ذَلِكَ أَوْ لَتُخْطَفَنَّ أَبْصَارُهُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hivi wana nini watu! wananyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala zao", ikazidi ukali kauli yake katika hilo, mpaka akasema: "Hakika, ni ima waache kufanya hivyo, au yatapofuliwa macho yao".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Aliwatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wale wanaonyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala wakati wa dua au kinginecho, kisha karipio lake likawa kali na akatangaza adhabu rehema na amani ziwe juu yake kwa wanaofanya hivyo kwamba yanahofiwa macho yao kupofuliwa na yakanyakuliwa kwa haraka kwa namna wasiyoitarajia, wakajikuta tayari wamepoteza neema ya macho.

Mafunzo
  1. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kubainisha kwake haki; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake hakumtaja mkosefu; kwa sababu lengo ni kubainisha haki na tayari imekwisha tendeka; na kwa sababu ndani yake kuna kumsitiri mkosefu na inahamasisha zaidi mtu kukubali ukweli.
  2. Katazo la msisitizo, na ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua macho yake juu mbinguni ndani ya swala.
  3. Amesema katika kitabu cha Aunul Ma'buud: Na sababu katika hilo ni kwamba atakaponyanyua macho yake juu mbinguni atakuwa katoka katika nembo ya kibla na ameipuuza na katoka katika muonekano wa swala pia.
  4. Kunyanyua macho kunaondoa utulivu ndani ya swala.
  5. Ukubwa wa hadhi ya swala, na kwamba ni wajibu kwa wenye kusali wawe katika adabu kamili pamoja na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 150) (750). كشاف القناع عن متن الإقناع، لمنصور بن يونس البهوتي (2/ 404). توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 101). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 587). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة قاسم (2/ 159).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنين رَضيَ اللهُ عنها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسْتَفْتِحُ الصَّلَاةَ بِالتَّكْبِيرِ، وَالقِرَاءَةِ، بِـ الحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ العَالَمِينَ، وَكَانَ إِذَا رَكَعَ لَمْ يُشْخِصْ رَأْسَهُ وَلَمْ يُصَوِّبْهُ، وَلَكِنْ بَيْنَ ذَلِكَ، وَكَانَ إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوعِ لَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَسْتَوِيَ قَائِمًا، وَكَانَ إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ السَّجْدَةِ لَمْ يَسْجُدْ حَتَّى يَسْتَوِيَ جَالِسًا، وَكَانَ يَقُولُ فِي كُلِّ رَكْعَتَيْنِ التَّحِيَّةَ، وَكَانَ يَفْرِشُ رِجْلَهُ اليُسْرَى وَيَنْصِبُ رِجْلَهُ اليُمْنَى، وَكَانَ يَنْهَى عَنْ عُقْبَةِ الشَّيْطَانِ، وَيَنْهَى أَنْ يَفْتَرِشَ الرَّجُلُ ذِرَاعَيْهِ افْتِرَاشَ السَّبُعِ، وَكَانَ يَخْتِمُ الصَّلَاةَ بِالتَّسْلِيمِ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akifungua swala kwa takbira (Allaahu Akbaru) na kisomo kwa kuanza na Alhamdulillaahi Rabbil a'alamiin, na alikuwa anaporukuu hanyanyui wala hainamishi kichwa chake, lakini kati na kati, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu hasujudu mpaka alingane wima, na alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika sijida hasujudu mpaka alingane sawa kwa kukaa, na alikuwa akisoma tahiyatu kila baada ya raka mbili, na alikuwa akiutandika mguu wake wa kushoto na kuusimamisha mguu wake wa kulia, na alikuwa akikataza mkao wa Shetani, na akikataza mtu kulaza mikono yake kama wanyama wakali, na alikuwa akihitimisha swala kwa salamu
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake sehemu ya swala ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakwamba alikuwa akifungua swala yake kwa takbira ya kufungua swala, akisema: "Allaahu Akbaru", na akifungua kisomo kwa suratul Faatiha. "Alhamdulillaah Rabbil A''alamiin..." Na alikuwa anaporukuu baada ya kisimamo, hainui kichwa chake na wala hakishushi wakati wa rukuu, bali anakifanya kilingane sawa kikiwa kimenyooka, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu ananyooka wima kabla hajasujudu, na akinyanyua kichwa chake kutoka katika sijida ya kwanza, hasujudu sijida ya pili mpaka atuliazane akiwa amekaa. Na alikuwa akikaa baada ya kila rakaa mbili kwa ajili ya tahiyatu, na anasema: "Attahiyyatu lillaahi was swalawaatu wat twayyibaatu...", na alikuwa anapokaa baina ya sijida mbili au kwa ajili ya tahiyatu analaza mguu wake wa kushoto na kuukalia, na anasimamisha mguu wake wa kulia. Na anamkataza mwenye kuswali kukaa ndani ya swala yake kama mkao wa Shetani, nao ni kulaza miguu yake yote miwili katika Ardhi, na kukaa kwa pande zake mbili za nyuma, au kuambatanisha makalio yake na Ardhi na akasimamisha miguu yake na kuweka mikono yake katika Ardhi kama anavyoitandaza mbwa, au akalaza mwenye kuswali mikono yake kwa kuinyoosha katika sijida kama anavyoilaza mnyama mkali. Na alikuwa akihitimisha swala yake kwa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullah" upande wa kulia mara moja na mara nyingine upande wa kushoto.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa kiasi kidogo cha namna ya swala ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Uwajibu wa takbira ya kuhirimia swala, inayoharamisha kila kauli au kitendo kinachopingana na kauli za swala na vitendo vyake, na kwamba kinyume na namna hiyo hakuna namna nyingine inayofaa kuingia ndani ya swala.
  3. Uwajibu wa kusoma Suratul Faatiha.
  4. Uwajibu wa kurukuu, na jambo bora zaidi ndani yake ni kulingana sawa, bila kuinuka, wala kuinama.
  5. Uwajibu wa kuinuka kutoka katika rukuu, na uwajibu wa kulingana sawa katika kisimamo baada yake.
  6. Uwajibu wa kusujudu, na uwajibu wa kunyanyuka kutoka katika kusujudu, na kulingana sawa wakati wa kukaa baada yake.
  7. Sheria ya kulaza mguu wa kushoto kwa mwenye kuswali na kusimamisha mguu wa kulia katika kukaa ndani ya swala, ama katika tahiyatu ya mwisho katika swala ambayo ina tahiyatu mbili kama Magharibi na Ishaa, sheria ni kukalia kalio moja (Tawaruku), na zimekuja hadithi zingine kuhusu hilo.
  8. Katazo la kujifananisha na Shetani katika kukaa kwake, na hiyo ni mtu kukaa juu ya makalio yake na kulaza miguu yake juu ya Ardhi, au akaisimamisha na akakaa kati kati yake ikiwa katika Ardhi.
  9. Katazo la kujifananisha na wanyama washambuliao katika kutandaza mikono yake, nayo ni kutandaza mikono yake mwenye kuswali katika Ardhi, kwani hilo ni ishara ya uvivu na udhaifu.
  10. Katazo la kujifananisha na Shetani na wanyama katika vitendo vyao.
  11. Uwajibu wa kuhitimisha swala kwa salamu, nayo ni dua kwa wenye kuswali na waliohudhuria na wema wasiokuwepo kwa kuwaombea amani dhidi ya kila shari na mapungufu.
  12. Uwajibu wa kutulizana ndani ya swala.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 357) (498). شرح النووي على مسلم (4/ 213). سبل السلام، لمحمد الصنعاني (1/ 248 ). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 172). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 51). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 189). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص145).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayeisahau swala, basi aiswali atakapoikumbuka, haina kafara nyingine isipokuwa hiyo

عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ نَسِيَ صَلَاةً فَلْيُصَلِّ إِذَا ذَكَرَهَا، لَا كَفَّارَةَ لَهَا إِلَّا ذَلِكَ: {وَأَقِمِ الصَّلاةَ لِذِكْرِي} [طه: 14]».
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeisahau swala, basi aiswali atakapoikumbuka, haina kafara nyingine isipokuwa hiyo: "Na simamisha swala kwa ajili ya kunitaja mimi" [Twaha: 14].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesahau kutekeleza swala ya faradhi mpaka ukatoka wakati wakati wake, basi anatakiwa aende mbio na afanye haraka kuilipa pale anapoikumbuka, amesema Allah katika kitabu chake kitukufu: "Na usimamishe swala kwa ajili ya kunitaja" [Twaha: 14] Simamisha swala zilizosahaulika unapozikumbuka.

Mafunzo
  1. Umuhimu swala na kutozembea katika kuitekeleza na kuilipa.
  2. Haitakiwi kuichelewesha swala nje ya wakati wake kwa makusudi bila udhuru.
  3. Uwajibu wa kulipa swala kwa aliyesahau na aliyesinzia mpaka atakapo amka.
  4. Uwajibu wa kulipa swala haraka hata kama ni katika nyakati zilizoharamishwa.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 122) (597)، صحيح مسلم (1/ 477) (684)، فتح الباري لابن حجر (2/ 71)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (14/ 612).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَسْوَأُ النَّاسِ سَرَقَةً الَّذِي يَسْرِقُ صَلَاتَهُ» قَالَ: وَكَيْفَ يَسْرِقُ صَلَاتَهُ؟ قال: «لَا يُتِمُّ رُكُوعَهَا، وَلَا سُجُودَهَا».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwizi mbaya zaidi kuliko watu wote, ni yule anayeiba swala yake" Akasema: Ataiba vipi swala yake? Akasema: "Hatimizi rukuu zake wala sijida zake".
Imepokelewa na Ibnu HibanDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwizi mbaya zaidi kuliko wote ni yule anayeiba swala yake; na hii ni kwakuwa; kuchukua mali ya mtu mwingine huenda mtu akanufaika nayo duniani, tofauti na mwizi huyu, kwa sababu kaiba haki ya nafsi yake katika thawabu na malipo, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na vipi mtu anawezaiba kutoka katika swala yake? Akasema: Kwa kutotimiza rukuu zake wala sijida zake; na hii ni pale anapofanya haraka kutoka katika rukuu na sijida, hazileti katika namna ya ukamilifu.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kuifanya vizuri sala, na kuzileta nguzo zake taratibu na kwa utulivu.
  2. Amemsifu mtu asiyetimiza rukuu yake na sijida yake kuwa ni mwizi, ikiwa ni ishara ya kulichukia hilo, na tahadhari juu ya uharamu wake.
  3. Uwajibu wa kutimiza rukuu na sijida ndani ya swala na kutulizana ndani yake.
Marejeo

صحيح ابن حبان (5/ 209) (1888)، الشّافي في شرح مسند الشّافعي (1/613)، الكاشف عن حقائق السنن (3/1020)، التنوير (2/373)، نيل الأوطار (2/ 311).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com