Kutoka kwa Sa'd radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Sa'di bin Abii Waqasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akiona shavu la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kugeuka kwake sana anapotoa salamu kwa ajili ya swala yake, kuliani kwake kwa ajili ya salamu ya kwanza, na kushotoni kwake kwa ajili ya salamu ya pili.
Mafunzo
Sheria ya kupitiliza katika kugeuka katika upande wa kulia na upande wa kushoto.
Sheria ya kutoa salamu mbili kuliani na kushotoni.
Amesema Nawawi: Na lau mtu atatoa salamu mbili kuliani kwake au kushotoni kwake au mbele yake au ya kwanza kushotoni kwake na ya pili kuliani kwake swala yake itakuwa sahihi, lakini atakosa fadhila ya usahihi wake.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 409) (582).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (13/ 99).
مرقاة المصابيح شرح مشكاة المصابيح (4 /30).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com