Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Nguzo za Swala.

Hadithi 4

Nilimuuliza Anas bin Malik: alikuwa Nabii Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- akiswali na viatu vyake? akasema: ndio

عن مَسْلَمَةَ سَعِيدِ بْنِ يَزِيد قال: سألت أنس بن مالك: أكان النبي صلى الله عليه وسلم يُصَلِّي في نَعْلَيْهِ؟ قال: «نعم».
Kutoka kwa Maslama Saidi bin Yazid amesema: nilimuuliza Anas bin Malik: alikuwa Nabii Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake- akiswali na viatu vyake? akasema: ((ndio)).
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Katika madhumuni ya sheria ni kutofautiana na watu wa kitabu, (Mayahudi na wakristo), nakuondoa kila kitu ambacho ndani yake kina tabu na uzito juu ya muislamu, na alimuuliza Saidi bin thabit naye ni katika waaminifu wakubwa miongoni mwa wanafunzi wa maswahaba, kamuuliza Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuhusu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Hivi je alikuwa akiswali na viatu vyake; ili iwe kwake ni kiigizo? Au ni kwasababu aliliona hilo haliwezekani kwasababu yakuwa mara nyingi huwa na uchafu na udhia, Anasi akamjibu, Ndiyo, alikuwa akiswali na viatu vyake, nakuwa hilo ni katika sunna zake takatifu, na hili si maalumu kwa ardhi fulani au zama maalumu.

Marejeo

تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، عبد الله بن عبد الرحمن البسام، تحقيق: محمد صبحي حلاق، مكتبة الصحابة، الأمارات، مكتبة التابعين، القاهرة، الطبعة: العاشرة 1426هـ، 2006م. تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، محمد بن صالح العثيمين، مكتبة الصحابة، الإمارات، الطبعة: الأولى 1426هـ، 2005م. صحيح البخاري، محمد بن إسماعيل البخاري الجعفي، تحقيق: محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى 1422هـ. صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، الطبعة: 1423هـ. تأسيس الأحكام، أحمد بن يحيى النجمي، دار المنهاج، الطبعة: 1427هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Lau angejua mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali nini anachokipata, basi kusimama arobaini ni bora kwake kuliko kupita mbele yake

عَنْ بُسْرِ بْنِ سَعِيدٍ، أَنَّ زَيْدَ بْنَ خَالِدٍ الْجُهَنِيَّ رَضيَ اللهُ عنه، أَرْسَلَهُ إِلَى أَبِي جُهَيْمٍ رَضيَ اللهُ عنه، يَسْأَلُهُ مَاذَا سَمِعَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْمَارِّ بَيْنَ يَدَيِ الْمُصَلِّي؟ قَالَ أَبُو جُهَيْمٍ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَوْ يَعْلَمُ الْمَارُّ بَيْنَ يَدَيِ الْمُصَلِّي مَاذَا عَلَيْهِ لَكَانَ أَنْ يَقِفَ أَرْبَعِينَ خَيْرًا لَهُ مِنْ أَنْ يَمُرَّ بَيْنَ يَدَيْهِ» قَالَ أَبُو النَّضْرِ: لَا أَدْرِي قَالَ: أَرْبَعِينَ يَوْمًا أَوْ شَهْرًا أَوْ سَنَةً؟
Kutoka kwa Busru bin Saidi, ya kwamba Zaidi bin Khalidi Al-Juhani, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimtuma kwenda kwa Abuu Juhaim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amuulize alisikia nini kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mtu anayepita mbele ya anayeswali? Akasema Abuu Juhaim: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Lau angejua mwenye kupita mbele ya mwenye kuswali nini anachokipata, basi kusimama arobaini ni bora kwake kuliko kupita mbele yake" Amesema Abuu Nasri: Sijui alisema: Siku arobaini au miezi au miaka?
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupita mbele ya mwenye kuswali swala ya faradhi au sunna, na kwamba lau angelijua mwenye kufanya hivyo kwa makusudi yale anayoyapata katika madhambi; basi angechagua kusimama arobaini; hilo ni bora zaidi kwake kuliko kupita mbele yake. Amesema Abuu Nasri mpokezi wa hadithi: Sijui alisema: Siku arobaini, au miezi au miaka.

Mafunzo
  1. Uharamu wa kupita mbele ya mwenye kuswali, atakapokuwa hana kizuizi (sutra), au kupita kati yake na kizuizi atakapokuwa na kizuizi.
  2. Amesema bin Hajari: Na wakatofautiana wanachuoni katika kuweka kiwango cha hilo pakasemwa: Atakapopita kati yake na kiasi cha kusujudu kwake, na pakasemwa: Kati yake yeye na huyo kuwe na futi tatu, na pakasema: kuwe kati yake na yeye kiwango cha kurusha jiwe.
  3. Amesema Suyutwi: Makusudio ya kupita ni apite mbele yake kwa makusudi, ama akipita mbele yake akiwa anakwenda upande wa kibla hii haiingii katika ahadi hiyo ya adhabu.
  4. Kilicho bora nikuwa mwenye kuswali asiswali katika njia za watu, na katika sehemu ambazo hawana budi lazima wapite, ili asiitie swala yake katika mapungufu, na asiwatie katika makosa wenye kupita, na anatakiwa aweke kizuizi kitakachozuia kati yake na wenye kupita.
  5. Inachukuliwa katika hadithi hii kuwa; madhambi yoyote yanayohusu maasi Akhera hata kama ni kidogo basi ni makubwa mno kuliko shida yoyote ya duniani, vyovyote vile itakavyokuwa shida hiyo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 108) (510). صحيح مسلم (1/ 363) (507). تيسير العلام، للبسام تيسير العلام (ص184). تنبيه الأفهام، لابن عثيمين (2/ 239). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 154).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake

عَنْ سَعْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كُنْتُ أَرَى رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ، وَعَنْ يَسَارِهِ، حَتَّى أَرَى بَيَاضَ خَدِّهِ.
Kutoka kwa Sa'd radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Sa'di bin Abii Waqasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akiona shavu la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kugeuka kwake sana anapotoa salamu kwa ajili ya swala yake, kuliani kwake kwa ajili ya salamu ya kwanza, na kushotoni kwake kwa ajili ya salamu ya pili.

Mafunzo
  1. Sheria ya kupitiliza katika kugeuka katika upande wa kulia na upande wa kushoto.
  2. Sheria ya kutoa salamu mbili kuliani na kushotoni.
  3. Amesema Nawawi: Na lau mtu atatoa salamu mbili kuliani kwake au kushotoni kwake au mbele yake au ya kwanza kushotoni kwake na ya pili kuliani kwake swala yake itakuwa sahihi, lakini atakosa fadhila ya usahihi wake.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 409) (582). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (13/ 99). مرقاة المصابيح شرح مشكاة المصابيح (4 /30).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَوْ يَعْلَمُ النَّاسُ مَا فِي النِّدَاءِ وَالصَّفِّ الْأَوَّلِ ثُمَّ لَمْ يَجِدُوا إِلَّا أَنْ يَسْتَهِمُوا عَلَيْهِ لَاسْتَهَمُوا، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِي التَّهْجِيرِ لَاسْتَبَقُوا إِلَيْهِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِي الْعَتَمَةِ وَالصُّبْحِ لَأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura, na walau wangelijua yaliyomo katika kuwahi basi wangelishindana, na lau wangelijua yaliyomo katika swala ya usiku na swala ya Asubuhi, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba laiti watu wangelijua yaliyomo katika Adhana na safu ya kwanza miongoni mwa fadhila na kheri na baraka, kisha wakakosa namna ya kutangulizana na nani awe bora kuliko mwingine ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura, na lau wangelijua yaliyomo katika kuwahi swala mwanzo wa wakati wake basi wangelishindana kuyaendea, na laiti wangelijua kiwango cha thawabu katika kuiendea swala ya Ishaa na swala ya Alfajiri, basi kungekuwa kwepesi kuziendea hata kwa kutambaa kwa magoti kama anavyotembea mtoto mwanzo wa kukua kwake.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa fadhila ya Adhana.
  2. Kumebainishwa fadhila ya safu ya kwanza, na kuwa karibu na imamu.
  3. Kumebanisha ubora wa kuwahi katika swala mwanzo wa wakati wake unaofaa; kwakuwa ndani yake kuna fadhila kubwa, na faida zinazoambatana na hilo, ikiwemo: Kuipata safu ya kwanza, na kuipata swala kuanzia mwanzo wake, na kutekeleza swala za sunna, na kusoma Qur'ani, na kupata kuombewa msamaha na Malaika, na kwamba anapata malipo kana kwamba yupo ndani ya swala kwa muda wote atakaokaa akisubiri swala, na mengineyo.
  4. Himizo kubwa la kuhudhuria jamaa za swala hizi mbili, na fadhila nyingi katika hilo, kwa kuwa ndani yake kuna ugumu juu ya nafsi kama kuibana mwanzo wa usingizi wake na mwisho wake, na ndiyo maana zikawa ndio swala ngumu zaidi kwa wanafiki.
  5. Amesema Nawawi: Hapa kuna kuthibitishwa kupiga kura katika haki ambazo watu wanasongamana na kuzozana ndani yake.
  6. Safu ya pili ni bora kuliko safu ya tatu, na ya tatu ni bora kuliko ya nne, na kuendelea.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 126) (615). صحيح مسلم (1/ 325) (437). النهاية في غريب الحديث والأثر (1000) (185). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (10/ 267).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com