Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa

عن أبِي هريرة رضي اللَّه عنه: سمعتُ النبِيّ صلى الله عليه وسلم يقول: «الفِطْرَةُ خمسٌ: الخِتَانُ والاستحدادُ وقصُّ الشَّارِبِ وتقليمُ الأظفارِ وَنَتْفُ الآبَاطِ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo matano katika dini ya Uislamu na sunna ya Mitume: La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi iliyozidi juu ya kichwa cha dhakari kwa mwanaume, na kukata kingozi katika tupu ya mwanamke juu ya malaha palipo tundu la uke. La pili: Kunyoa sehemu za siri, nako ni kunyoa nywele za kinena zinazozunguka tupu ya mbele. La tatu: Kupunguza masharubu, nako ni kupunguza kilichoota juu ya mdomo wa juu wa mwanaume mpaka mdomo uonekane wazi. La nne: Kupunguza kucha. La tano: Kunyofoa nywele za kwapa.

Mafunzo
  1. Sunna za Mitume anazozipenda Mwenyezi Mungu na kuziridhia na anaziamrisha, zinapelekea katika ukamilifu na usafi na uzuri.
  2. Sheria ya kushikamana na mambo haya, na kutoghafilika nayo.
  3. Mambo haya yanafaida za kidini na kidunia, miongoni mwake: Kupendezesha muonekanao, na kusafisha mwili, na kujiweka tayari kwa usafi, na kwenda kinyume na makafiri, na kutekeleza amri ya Allah.
  4. Kumetajwa katika hadithi zingine ziada ya jambo jingine la kimaumbile tofauti na matano haya, mfano: Kufuga ndevu, na mswaki na nyinginezo.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 160) (5891). صحيح مسلم (1/ 222) (257). عمدة الأحكام (ص44) (30). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 45). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص58). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 72).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sunna za Kimaumbile.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com