Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Sunna za Kimaumbile.

Hadithi 8

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ يَشُوصُ فَاهُ بِالسِّوَاكِ.
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara nyingi akipiga mswaki na akiamrisha watu kufanya hivyo, na kuna baadhi ya nyakati kumetiliwa mkazo, mfano; kupiga mswaki wakati wa kuamka usiku, kwani alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akisukutua na kutakatisha kinywa chake kwa mswaki.

Mafunzo
  1. Mkazo wa sheria ya kupiga mswaki baada ya usingizi wa usiku, kwa sababu usingizi hupelekea mabadiliko ya harufu ya kinywa, na mswaki ndio kifaa cha kusafishia.
  2. Mkazo wa sheria ya kupiga mswaki kila wakati wa mabadiliko ya harufu ya kinywa, kwa kuzingatia maana ya awali.
  3. Sheria ya usafi kwa ujumla, na kwamba ni sehemu ya Sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ni katika adabu tukufu.
  4. Kupiga mswaki katika kinywa chote kunajumuisha: Meno, fizi, na ulimi.
  5. Mswaki ni kijiti kilichokatwa kutoka katika mti wa araki au mti mwingine, na hutumika kusafisha kinywa na meno, na huburudisha kinywa, na kuondoa harufu mbaya.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 58) (245). صحيح مسلم (1/ 220) (255). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص47). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص24).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa

عن أبِي هريرة رضي اللَّه عنه: سمعتُ النبِيّ صلى الله عليه وسلم يقول: «الفِطْرَةُ خمسٌ: الخِتَانُ والاستحدادُ وقصُّ الشَّارِبِ وتقليمُ الأظفارِ وَنَتْفُ الآبَاطِ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo matano katika dini ya Uislamu na sunna ya Mitume: La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi iliyozidi juu ya kichwa cha dhakari kwa mwanaume, na kukata kingozi katika tupu ya mwanamke juu ya malaha palipo tundu la uke. La pili: Kunyoa sehemu za siri, nako ni kunyoa nywele za kinena zinazozunguka tupu ya mbele. La tatu: Kupunguza masharubu, nako ni kupunguza kilichoota juu ya mdomo wa juu wa mwanaume mpaka mdomo uonekane wazi. La nne: Kupunguza kucha. La tano: Kunyofoa nywele za kwapa.

Mafunzo
  1. Sunna za Mitume anazozipenda Mwenyezi Mungu na kuziridhia na anaziamrisha, zinapelekea katika ukamilifu na usafi na uzuri.
  2. Sheria ya kushikamana na mambo haya, na kutoghafilika nayo.
  3. Mambo haya yanafaida za kidini na kidunia, miongoni mwake: Kupendezesha muonekanao, na kusafisha mwili, na kujiweka tayari kwa usafi, na kwenda kinyume na makafiri, na kutekeleza amri ya Allah.
  4. Kumetajwa katika hadithi zingine ziada ya jambo jingine la kimaumbile tofauti na matano haya, mfano: Kufuga ndevu, na mswaki na nyinginezo.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 160) (5891). صحيح مسلم (1/ 222) (257). عمدة الأحكام (ص44) (30). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 45). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص58). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 72).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Punguzeni sharubu na mfuge ndevu

عن ابن عمر رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «أحْفُوا الشَّوَارِبَ وأَعْفُوا اللِّحَى».
Imepokewa kutoka kwa Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Punguzeni sharubu na mfuge ndevu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupunguza sharubu na zisiachwe bali zipunguzwe, na azidi kupunguza zaidi. Na pamoja na hilo anaamrisha kufuga ndevu na kuziacha zikichanua.

Mafunzo
  1. Uharamu wa kunyoa ndevu.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 160) (5892). صحيح مسلم (1/ 222) (259). رياض الصالحين (ص338) (1205). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 345). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن (2/ 853). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 228). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (14/ 507). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص676). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة محمد قاسم (5/ 236).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akiwa anapiga mswaki kwa mswaki wa mti mbichi, Akasema: na ncha ya mswaki ikiwa katika ulimi wake, naye akisema: AAGH, AAGH (sauti ya kujigogoa), na mswaki ukiwa mdomoni mwake, kana kwamba anajigogoa

عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه قال: ((أتَيتُ النبي صلى الله عليه وسلم وهو يَسْتَاكُ بِسِوَاك رَطْب، قال: وطَرَفُ السِّوَاك على لسانه، وهو يقول: أُعْ، أُعْ، والسِّوَاك في فِيه، كأنَّه يَتَهَوَّع)).
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: (Nilimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akiwa anapiga mswaki kwa mswaki wa mti mbichi, Akasema: na ncha ya mswaki ikiwa katika ulimi wake, naye akisema: AAGH,AAGH (sauti ya kujigogoa), na mswaki ukiwa mdomoni mwake, kana kwamba anajigogoa).
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Abuu Musa Al Ash'ariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: yakuwa yeye alikuja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akipiga mswaki kwa kutumia mti mbichi kwasababu husafisha kikamilifu na hausambaratiki mdomoni; ukakera, na hakika alikuwa kaweka mswaki juu ya ulimi wake, mpaka akawa kana kwamba anajitapisha.

Marejeo

الإلمام بشرح عمدة الأحكام، إسماعيل بن محمد الأنصاري، دار الفكر، دمشق، الطبعة: الأولى، 1381هـ. تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، عبد الله بن عبد الرحمن البسام، تحقيق: محمد صبحي حلاق، مكتبة الصحابة، الأمارات، مكتبة التابعين، القاهرة، الطبعة: العاشرة، 1426هـ. تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، محمد بن صالح العثيمين، مكتبة الصحابة، الإمارات، الطبعة: الأولى، 1426هـ. عمدة الأحكام من كلام خير الأنام -صلى الله عليه وسلم-، لعبد الغني المقدسي، دراسة وتحقيق: محمود الأرناؤوط، مراجعة وتقديم: عبد القادر الأرناؤوط، دار الثقافة العربية، دمشق، بيروت، مؤسسة قرطبة، الطبعة: الثانية، 1408هـ. صحيح البخاري، محمد بن إسماعيل البخاري الجعفي، تحقيق: محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ. صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، الطبعة: 1423هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mswaki ni usafi wa kinywa, humridhisha Mola

عن عائشة رضي الله عنها قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «السِّوَاكُ مَطْهَرَةٌ لِلْفَمِ، مَرْضَاةٌ لِلرَّبِّ».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mswaki ni usafi wa kinywa, humridhisha Mola".
Imepokelewa na Nasai na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kusafisha meno kwa kijiti cha mti wa Arak na mfano wake husafisha kinywa kutokana na uchafu na harufu mbaya, Nakuwa ni katika sababu za kumridhisha Allah Mtukufu kwa mja; kwa sababu ndani yake kuna kumtii Allah na kuitika amri yake, na pia kuna usafi anaoupenda Allah Mtukufu.

Mafunzo
  1. Ubora wa mswaki, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuuhimiza umma wake kukithirisha kupiga
  2. Katika mswaki ni bora kutumia kijiti cha mti wa Arak, na kutumia miswaki ya brashi na dawa ya meno hukaa badala yake.
Marejeo

سنن النسائي (1/ 10) (5). مسند أحمد (40/ 240) (24203). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 342). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 852). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص675).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki

عَنِ شُرَيْحٍ بنِ هانِئٍ قَالَ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ، قُلْتُ: بِأَيِّ شَيْءٍ كَانَ يَبْدَأُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ بَيْتَهُ؟ قَالَتْ: بِالسِّوَاكِ.
Kutoka kwa Shuraihi bin Hanii amesema: Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ilikuwa katika muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuanza na mswaki anapoingia nyumbani kwake wakati wowote, usiku au mchana.

Mafunzo
  1. Sheria ya kupiga mswaki ni ya ujumla kwa nyakati zote, na inatiwa mkazo: katika nyakati ambazo sheria imehimiza, miongoni mwake ni: Wakati wa kuingia nyumbani, na wakati wa swala, na wakati wa udhu, na baada ya kuamka kutoka usingizini, na wakati wa kubadilika kwa harufu ya kinywa.
  2. Kumebainishwa pupa ya wanafunzi wa Maswahaba ya kuuliza kuhusu hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na sunna zake; ili wamuige.
  3. Kuchukua elimu kutoka kwa wenye elimu na kwa wale wenye kujua zaidi, kiasi ambacho aliulizwa Aisha kuhusu hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kuingia kwake nyumbani.
  4. Uzuri wa maisha ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na familia yake, kiasi kwamba alikuwa akisafisha kinywa chake wakati wa kuingia.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 220) (253). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 341). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 851). المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، النووي (3/ 144).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mambo kumi ni katika maumbile: Kupunguza masharubu, na kuziachia ndevu,na kupiga mswaki, na kupandisha maji puani, na kupunguza kucha, na kuosha fundo za vidole, na kunyofoa nywele za makwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kustanji kwa maji.

عن عائشة رضي الله عنها مرفوعاً: «عَشْرٌ من الفِطْرة: قَصُّ الشَارب، وإعْفَاء اللِّحْية، والسِّواك، وَاسْتِنْشَاقُ الماء، وقص الأظْفَار، وغَسْل البَرَاجِم، ونَتْف الإبْط، وحلق العَانة، وانْتِقَاصُ الماء» قال الراوي: ونَسِيْتُ العاشرة إلا أن تكون المَضْمَضَة. قال وكِيع - وهو أحد رواته - انْتِقَاص الماء: يعني الاسْتِنْجَاء.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mambo kumi ni katika maumbile: Kupunguza masharubu, na kuziachia ndevu,na kupiga mswaki, na kupandisha maji puani, na kupunguza kucha, na kuosha fundo za vidole, na kunyofoa nywele za makwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kustanji kwa maji". Anasema mpokezi : na nimelisahau la kumi nahisi huenda ikawa ni kusukutua. Amesema Wakii -naye ni mmoja kati ya wapokezi wake na kupunguza maji: Yaani kustanji.
Imepokelewa na Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake -kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- jumla ya sunna za kimaumbile. Na "Maumbile" ni umbile ambalo Mwenyezi Mungu kawaumba viumbe juu yake, na akawafanya kuumbika (kulazimika) kulifanya, nakuwa hilo ni katika kheri na makusudio yake na ni umbile salama; kwasababu umbile lililopinda halizingatiwi; kwa kauli ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:"Kila mwenye kuzaliwa huzaliwa katika maumbile basi wazazi wake humfanya kuwa Yahudi au Mkristo au mmajusi". La kwanza: "kupunguza masharubu": kuyapunguza mpaka mdomo uonekane, kwa kile kinachopatikana ndani yake katika usafi, na kujilinda na vile vinavyotoka puani, kwani nywele za masharubu zinaposogea katika mdomo hugusa kile ambacho mdomo unakipata katika vyakula au vinywaji, na kuharibu muonekano pale zinapokithiri, hata kama atalipendezesha hilo asiyejali. Ni lazima muislamu achunge sharubu zake kwa kuzinyoa au kuzipunguza na asiziache zaidi ya siku arobaini; kwa yale aliyoyapokea Muslim kutoka kwa Anasi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-tuliwekewa muda sisi katika masharubu, na kupunguza kucha, na kukwapua nywele za kwapani, na kunyoa sehemu za siri, kuwa tusiziache zaidi ya siku arobaini" "Na kuziachia ndevu" Na ndevu: ni zile zilizoota katika kidevu au sharafa (nywele za shavuni), Na makusudio ya kuziachia: kuziacha zikiwa zimejaa asiziguse kwa kuzinyoa wala kuzipunguza,si kidogo wala kingi; kwasababu neno kuziachia limetokana na wingi na kujaza,kama kauli yake Mtukufu: (Mpaka walipoachilia), na zimekuja hadithi nyingi toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- zikiamrisha kuzifuga kwa matamshi mengi; kwani imekuja kwa tamko:"jazeni ndevu" na kwa tamko:"Shusheni ndevu", na kwa tamko "Achieni ndevu", na kama inavyoonyesha amri ya kuziacha na kuzijaza na kutozigusa, na kwa msingi huu hairuhusiwi kwa muislamu kunyoa ndevu zake, ikiwa atafanya hivyo atakuwa kaenda kinyume na njia ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na atakuwa kaasi amri yake na kaangukia katika kujifananisha na makafiri."na mswaki" Yaani: katika mambo ya kimaumbile ambayo sheria imeyahimiza, Nikuwa "(mswaki) ni Kisafisha kinywa na humridhisha Mola" na ndio maana ni sheria kila wakati lakini inatiwa mkazo zaidi wakati wa udhu na swala na wakati wa kuamka toka usingizini na kubadilika kwa harufu ya mdomo, na meno kuwa ya njano na mfano wake. "na kupandisha maji puani" Yaani: nikuwa kupandisha maji ni katika maumbile, na kuondoa vilivyoko puani katika uchafu ambao unaweza kumsababishia udhia na madhara. Na kupandisha maji puani kunakuwa wakati wa udhu na kunakuwa nje ya udhu,kama mtu akihitaji kusafisha pua na kupandisha maji kwa kusafisha pua yake, na hii inatofautiana kulingana na watu, kuna baadhi ya watu hawahitaji hili isipokuwa katika udhu, na kuna watu wanalihitaji hili kwa wingi. Na miongoni mwa hilo pia: Yaani miongoni mwa sunna za maumbile ni kusukutua, kwani hilo ni katika maumbile; mdomo na pua mara nyingi vinazungukwa na uchafu, hivyo ikawa ni sehemu katika maumbile kuvizingatia."Na kupunguza kucha" Yaani katika mambo ya kimaumbile: ni kupunguza kucha, na makusudio yake ni kucha za mikono na miguu, zisiachwe zaidi ya siku arobaini; kwa mujibu wa hadithi iliyotangulia."Na kuosha fundo za mikono" Yaani na kuosha maungio ya vidole juu na ndani; kwasababu ni miongoni mwa sehemu unapokusanyikia uchafu; kwa kukunjamana kwake, hivyo huenda maji yasifike, na vikitiliwa umuhimu wa kuvisugua, na vikapitishwe tena mkono mara ya pili, basi maji yatavifikia, ikawa katika maumbile ni kuvitilia umuhimu. Na viunganishwe pamoja na fundo za vidole kila sehemu katika mwili inayokusanya uchafu kwa jasho au kinginecho kama mikunjo ya sikio na ndani ya mapaja na sehemu zinginezo zilizozidi kujikunja."Na kukwapua nywele za kwapani" Yaani: Katika mambo ya kimaumbile ni kukwapua nywele za kwapani, nako ni kuzivuta na kuzing'oa, na hiyo ni kwasababu ni sehemu inayokithiri jasho, na unakusanyika hapo uchafu, na harufu hubadilika, na zisiachwe zaidi ya siku arobaini; kwa kile kilichotangulia katika hadithi ya Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, na bora zaidi ni kuzinyofoa ikiwa ataweza, na ikiwa kunyofoa ni vigumu, basi hakuna tatizo kama atazinyoa na akatumia mafuta ya kuziondoa; kwasababu lengo ni kuziondoa na kusafisha mahali hapo, na tayari limefanyika."Na kunyoa sehemu za siri" Yaani: Katika mambo ya kimaumbile ni kuondoa nywele za sehemu ya siri, nazo ni nywele zinazoota sehemu ya siri ya mbele, kwa mwanaume na mwanamke, hivyo ni katika maumbile kuziondoa, sawa sawa iwe ni kwa kuzinyoa au kuzinyofoa au kuzipunguza au kwa kutumia vyombo vya kisasa; kwasababu lengo ni kusafisha, na tayari lengo limetimia, na wala asiziache kwa muda wa siku arobaini kwa hadithi ya Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Na kupunguza maji" Yaani ni katika maumbile kupunguza maji, na imefasiriwa kwa maana ya: kustanji, na inapewa nguvu maana hii kwa riwaya ya Abuudaudi na bin Majah kutoka Ammar bin Yaasir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:"Ni katika maumbile: Kusukutua, na kupandisha maji puani. Na kusafisha", Na kusatanji: ni kuondoa kilichotoka katika moja ya njia mbili kwa kitu kilichosafi, kama maji na jiwe na vitambaa, na mfano wa hivyo katika vile ambavyo vinahusika na kusafisha."Amesema mpokezi: Na nimesahau jambo la kumi, huenda likawa ni kusukutua "Hii ni shaka toka kwa mpokezi. Na uhakika wake nikuwa mambo haya yote, yanakamilisha muonekano wa mwanadamu na yanamsafisha na yanamtwaharisha, na yanamuondolea mambo yenye kumdhuru na machafu.

Marejeo

- رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين؛ للإمام أبي زكريا النووي، تحقيق د. ماهر الفحل، دار ابن كثير-دمشق، الطبعة الأولى، 1428ه. - دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين؛ لمحمد بن علان الشافعي، دار الكتاب العربي-بيروت - بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين؛ تأليف سليم الهلالي، دار ابن الجوزي- الطبعة الأولى1418ه - نزهة المتقين شرح رياض الصالحين؛ تأليف د. مصطفى الخِن وغيره، مؤسسة الرسالة-بيروت، الطبعة الرابعة عشر، 1407هـ. - صحيح مسلم؛ للإمام مسلم بن الحجاج، حققه ورقمه محمد فؤاد عبد الباقي، دار عالم الكتب-الرياض، الطبعة الأولى، 1417هـ. - تطريز رياض الصالحين؛ تأليف فيصل آل مبارك، تحقيق د. عبد العزيز آل حمد، دار العاصمة-الرياض، الطبعة الأولى، 1423هـ. - كنوز رياض الصالحين، لحمد بن ناصر العمار، دار كنوز إشبيليا- الطبعة الأولى1430ه - شرح رياض الصالحين؛ للشيخ محمد بن صالح العثيمين، مدار الوطن، الرياض، 1426هـ. - بهجة قلوب الأبرار وقرة عيون الأخيار في شرح جوامع الأخبار :عبد الرحمن بن سعدي - المحقق: عبد الكريم بن رسمي ال الدريني دار النشر: مكتبة الرشد للنشر والتوزيع الطبعة: الأولى 1422هـ - 2002م - فتاوى اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء - المجموعة الأولى - رئاسة إدارة البحوث العلمية والإفتاء - الإدارة العامة للطبع - الرياض.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: وُقِّتَ لَنَا فِي قَصِّ الشَّارِبِ، وَتَقْلِيمِ الْأَظْفَارِ، وَنَتْفِ الْإِبِطِ، وَحَلْقِ الْعَانَةِ، أَلَّا نَتْرُكَ أَكْثَرَ مِنْ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Aliweka kikomo Mtume rehema na amani ziwe juu yake cha mtu kupunguza sharubu, na kupunguza kucha za mikono na miguu, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, kusizidi kuziacha kwake zaidi ya siku arobaini.

Mafunzo
  1. Amesema Shaukani: Kilicho sawa nikuwa adhibiti kwa arobaini aliyoidhibiti kwayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake haitakiwi kuivuka, na haitochukuliwa kama kwenda kinyume na sunna kwa kuacha kupunguza na mfano wake baada kurefuka mpaka ifike kikomo cha muda huo.
  2. Amesema bin Hubaira: Hadithi hii ndio kikomo cha kuchelewesha hilo, na kilichobora ni kulitekeleza hilo kabla ya ukomo huo.
  3. Uislamu umetilia kipaumbele usafi na kujitwaharisha na kujipamba.
  4. Kupunguza sharubu, kwa kunyoa nywele zinazoota juu ya mdomo wa juu.
  5. Kukwapua nywele za kwapa, kwa kuondoa nywele zinazoota humo, nayo ni sehemu inayokuwa chini ya maungio kati ya mkono na bega.
  6. Kunyoa nywele za siri, nazo ni nywele zinazoota pembezoni mwa tupu ya mbele, kwa mwanaume na mwanamke.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 222) (258). شرح سنن أبي داود لابن رسلان (16/ 559). مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (3/ 115).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com