Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuondoa Najisi.

Hadithi 6

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدْخُلُ الْخَلَاءَ، فَأَحْمِلُ أَنَا وَغُلَامٌ نَحْوِي إِدَاوَةً مِنْ مَاءٍ وَعَنَزَةً فَيَسْتَنْجِي بِالْمَاءِ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa yeye pamoja na mtumishi mwenye kukaribiana naye katika umri wake, wakimfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi anapotoka kwenda kikidhi haja yake, walikuwa wakibeba fimbo yenye meno (mkongojo) mfano wa meno ya mshale ili aifanye kuwa sitara ya kutundukia kitu chenye kusitiri, au sitara kwa ajili ya swala yake, na walikuwa wakibeba pia chombo kidogo cha ngozi kilichojaa maji , anapomaliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukidhi haja yake, basi mmoja wao anampa chombo, basi anastanji kwa maji.

Mafunzo
  1. Muislamu anatakiwa kujiandaa kwa maji (au chochote cha kujisafishia) wakati wa kukidhi haja; ili asijekuhitaji kusimama akajichafua.
  2. Kuhifadhi uchi wakati wa kukidhi haja asijekumtazama yeyote; kwa sababu kutazama katika uchi ni haramu, kwani alikuwa kichomeka fimbo katika Ardhi na akifunga nguo yenye kusitiri.
  3. Kuna haja kubwa ya kuwafundisha watoto adabu za kiislamu na kuwalea katika adabu hizo; ili warithishane.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 42) (152). صحيح مسلم (1/ 227) (271). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص40). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 43). الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص84).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّهُ لَقِيَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي طَرِيقٍ مِنْ طُرُقِ الْمَدِينَةِ وَهُوَ جُنُبٌ، فَانْسَلَّ فَذَهَبَ فَاغْتَسَلَ، فَتَفَقَّدَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمَّا جَاءَهُ قَالَ: «أَيْنَ كُنْتَ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ؟» قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، لَقِيتَنِي وَأَنَا جُنُبٌ فَكَرِهْتُ أَنْ أُجَالِسَكَ حَتَّى أَغْتَسِلَ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سُبْحَانَ اللهِ، إِنَّ الْمُؤْمِنَ لَا يَنْجُسُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba alikutana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika barabara miongoni mwa barabara za mji wa Madina huku akiwa na janaba, akamkwepa na akaenda kuoga, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtafuta hakumpata, alipomjia akasema: "Ulikuwa wapi ewe Abuu Huraira?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikutana nami, nami nikiwa na janaba, sikufurahishwa kukaa na wewe mpaka nioge, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikutana Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika baadhi ya njia za Madina, na Abuu Huraira alikuwa na janaba, na kwa sababu ya kumuheshimu kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichukia kukaa naye na kuzungumza naye hali yakuwa yuko katika hali ile, kwa kudhani kwake kuwa yeye ni najisi, akaenda kwa uficho na akaoga, kisha akarejea na akakaa, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuuliza kuwa alikwenda wapi? Akamueleza kuhusu hali yake, na kwamba yeye alichukia kukaa naye hali yakuwa yeye ni najisi kwa sababu ya janaba, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akastaajabu, na akasema: Hakika muumini ni msafi na wala hanajisiki kwa hali yoyote; akiwa hai na hata wakiwa maiti.

Mafunzo
  1. Janaba linamzuia mtu kuswali na kugusa msahafu na kukaa msikitini, na wala halizuii kukaa pamoja na Waislamu na kukutana nao, na wala mwenye janaba hawi najisi.
  2. Usafi wa muumini akiwa hai au maiti.
  3. Kuwaheshimu watu wenye heshima, na elimu, na utengefu, na kukaa nao kwa muonekano mzuri.
  4. Hapa kuna sheria ya mfuasi kumuomba idhini ya kuondoka anayemfuata, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimkemea Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa kuondoka kwake pasina yeye kujua, na hii ni kwa sababu kuomba ruhusa ni katika adabu nzuri.
  5. Kusema: Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, wakati wa kustaajabu.
  6. Kufaa mtu kusimulia mambo yake binafsi katika yale ya aibu, kwa ajili ya masilahi.
  7. Kafiri ni najisi, lakini najisi yake si ya kuonekana, kwa sababu ya uchafu wa itikadi yake.
  8. Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii pia kuna adabu, ya kwamba msomi atakapoona kwa anayemfuata jambo analohofia kwake kwenda kinyume na usahihi basi amuulize, na amwambie lililo sahihi, na ambainishie hukumu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 65) (285). صحيح مسلم (1/ 282) (371). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 46). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص61). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 74).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

“Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.”

عَنْ أَبِي أَيُّوبَ الأَنْصَارِيِّ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا أَتَيْتُمُ الغَائِطَ فَلاَ تَسْتَقْبِلُوا القِبْلَةَ، وَلاَ تَسْتَدْبِرُوهَا وَلَكِنْ شَرِّقُوا أَوْ غَرِّبُوا» قَالَ أَبُو أَيُّوبَ: فَقَدِمْنَا الشَّأْمَ فَوَجَدْنَا مَرَاحِيضَ بُنِيَتْ قِبَلَ القِبْلَةِ فَنَنْحَرِفُ، وَنَسْتَغْفِرُ اللَّهَ تَعَالَى.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.” Abuu Ayub akasema: Basi tukaenda Sham tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea Kibla, tukawa tunageuka, na tunaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mwenye kutaka kukidhi haja kubwa au ndogo kuelekea Kibla na upande wa Al-Kaaba, na asiigeuze kwa kuiweka nyuma ya mgongo wake. Bali ni lazima ageuke akiwa ndani kuelekea Mashariki au Magharibi ikiwa Kibla chake ni kama kibla cha watu wa Madina. Kisha Abuu Ayub (radhi za Allah ziwe juu yake) akaeleza kuwa walipofika Sham walikuta vyoo vilivyotayarishwa kwa ajili ya kujisaidia vimejengwa kuelekea Al-Kaaba, hivyo wakawa wakijigeuza kutoka upande wa Kibla, pamoja na hivyo bado wanamuomba msamaha Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Hekima ya kufanya hilo ni kuitukuza Al-Kaaba tukufu na kuiheshimu.
  2. Kuomba msamaha kwa Allah baada ya kutoka mahali pa kukidhi haja.
  3. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake; Kwa sababu alipoeleza lililokatazwa akaelekeza linalofaa.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 88) (394). صحيح مسلم (1/ 224) (264). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص37). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 39).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «إِذَا شَرِبَ الْكَلْبُ فِي إِنَاءِ أَحَدِكُمْ فَلْيَغْسِلْهُ سَبْعًا». ولمسلم: « أولاهُنَّ بالتُراب».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba". Na kwa Muslim: "Moja kati ya mara hizo aoshe kwa udogo"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake chombo hicho kioshwe mara saba ikiwa mbwa ataingiza ulimi wake ndani yake, mara ya kwanza iwe kwa mchanga, ili yaje maji baada yake, hivyo usafi kamili utakuwa umepatikana kutokana na najisi yake na madhara yake.

Mafunzo
  1. Mate ya mbwa ni najisi tena ni najisi nzito.
  2. Mbwa kulamba katika chombo, kunakitia najisi chombo hicho, na kunanajisisha maji yaliyoko ndani yake.
  3. Kusafisha kwa udongo na kurudia mara saba hii ni maalum kwa kusafisha pale atakapo lamba, lakini si katika mkojo wake na uchafu wake na vyote atakavyovichafua mbwa.
  4. Jinsi ya kuosha chombo kwa udongo: Ataweka maji ndani ya chombo na kuongeza udongo ndani yake, kisha atasafisha chombo kwa mchanganyiko huu.
  5. Maana ya dhahiri ya Hadith ni kuwa hadithi hii inajumuisha mbwa wote, hata mbwa ambao sheria imeruhusu kufugwa, kama vile kuwinda, kulinda, na mbwa wa mifugo.
  6. Sabuni na majani ya miti havichukui nafasi ya udongo; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliweka sharti la kutumia udongo.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 45) (172). صحيح مسلم (1/ 234) (279). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 14). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص24).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe

عَنْ عَلِيٍّ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ رَجُلًا مَذَّاءً وَكُنْتُ أَسْتَحْيِي أَنْ أَسْأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِمَكَانِ ابْنَتِهِ فَأَمَرْتُ الْمِقْدَادَ بْنَ الْأَسْوَدِ فَسَأَلَهُ فَقَالَ: «يَغْسِلُ ذَكَرَهُ وَيَتَوَضَّأُ». وَلِلبُخَاريِّ: فَقَالَ: «تَوَضَّأْ وَاغْسِلْ ذَكَرَكَ».
Imepokewa Kutoka kwa Ally -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa ni mtu mwenye kutokwa na madhii kwa wingi na nilikuwa nikiona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutokana na nafasi ya binti yake kwangu, nikamuamrisha Mikidadi bin Aswadi, akamuuliza, akasema: "Aoshe tupu yake na atawadhe" Na katika sahihi Bukhari: Akasema: "Tawadha na uoshe tupu yako".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Ally bin Abiy Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye ilikuwa mara nyingi akitokwa na madhii -nayo ni maji meupe mepesi yenye utelezi hutoka katika tupu wakati wa matamanio au kabla ya tendo ya ndoa-, Na wala hajui afanye nini yakitoka, akaona haya kumuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu yeye ni mume wa Fatma binti wa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, Akamuomba Mikidadi bin Aswadi amuulize Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuhuus hilo, Basi akajibu Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa aoshe tupu yake kisha atawadhe.

Mafunzo
  1. Ubora wa Ally bin Abi Twalib Radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi ambacho haya haikumzuia kuacha kuuliza kupitia mtu mwingine.
  2. Inafaa kutuma mtu kwa niaba kwa ajili ya kuuliza.
  3. Inafaa kumueleza mtu mambo binafsi kwa sababu ya kuona haya ikiwa kuna masilahi.
  4. Unajisi wa madhii, na uwajibu wa kuyaosha katika mwili na nguo.
  5. Kutoka kwa madhii ni katika vitenguzi vya udhu.
  6. Uwajibu wa kuosha utupu na korodani mbili kwa kuwa zimetajwa katika hadithi nyingine.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 62) (269). صحيح مسلم (1/ 247) (303). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 39). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص53). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص29).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha

عَنْ أُمِّ قَيْسٍ بِنْتِ مِحْصَنٍ رَضيَ اللهُ عنها: أَنَّهَا أَتَتْ بِابْنٍ لَهَا صَغِيرٍ لَمْ يَأْكُلِ الطَّعَامَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَجْلَسَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجْرِهِ، فَبَالَ عَلَى ثَوْبِهِ، فَدَعَا بِمَاءٍ، فَنَضَحَهُ وَلَمْ يَغْسِلْهُ.
Kutoka kwa Ummu Qais bint Mihswan -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja mama Kaisi binti Mihswan radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake hajaanza kula chakula kutokana na udogo wa umri wake, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, mtoto akakojoa katika nguo yake rehema na amani ziwe juu yake, akaomba maji, na akanyunyiza katika nguo yake na wala hakuiosha.

Mafunzo
  1. Tabia njema za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na unyenyekevu wake wa hali ya juu.
  2. Wito wa kuishi vizuri na watu na unyenyekevu na upole kwa watoto, na kulea nyoyo za watu wazima kwa kuwakirimu watoto wao na kuwakalisha mapajani, na mfano wa hayo.
  3. Najisi ya mkojo wa mtoto mdogo hata asipokula chakula kwa matamanio.
  4. Kitendo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kinaitwa kunyunyiza, hicho ni maalumu kwa mtoto mdogo wa kiume ambaye hajaanza kula chakula, ama mtoto wa kike ni lazima kuosha mkojo wake hata akiwa mdogo.
  5. Kinyesi cha mtoto wa kiume ambaye chakula chake ni maziwa ya mama yake ni lazima kuosha kama najisi zingine.
  6. Kuosha ni lazima kuwe na jambo la ziada kama kufikisha maji.
  7. Kilicho bora ni kufanya haraka kusafisha mahali palipo na najisi; ili kufanya haraka kujitwaharisha kutokana na uchafu; na ili asisahau.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 54) (223). صحيح مسلم (1/ 238) (287). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 42). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص55). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 68).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com