Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hukumu ya utwahara wa maji ambayo yanazungukiwa na wanyama wafugwao na wanyamapori kwa ajili ya kunywa na mfano wake, akasema rehema na amani ziwe juu yake kuwa: Maji yakifikia kipimo cha pipa mbili kubwa, ambazo zitakuwa na ujazo wa lita (210) basi hayo ni maji mengi hayawezi kunajisika; isipokuwa ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake au harufu.
- Maji yananajisika ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake, au harufu yake, na hadithi imeeleza kwa ujumla na si kwa kuweka kikomo.
- Wamekubaliana wanachuoni kuwa maji yakibadilishwa na najisi basi yananajisika moja kwa moja, sawa sawa yawe kidogo au mengi.
سنن أبي داود (1/ 46) (63). سنن الترمذي (1/ 109) (67). سنن النسائي (1/ 46) (52). سنن ابن ماجه (1/ 324) (517). مسند أحمد (8/ 211) (4605). توضيح الأحكام، للبسام (1/ 121). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 67). منحة العلام، لعبد الله الفوزان (1/ 35).