Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hukumu za Maji.

Hadithi 2

Ni safi Maji yake na ni halali mizoga yake

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَأَلَ رَجُلٌ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّا نَرْكَبُ البَحْرَ، وَنَحْمِلُ مَعَنَا القَلِيلَ مِنَ الْمَاءِ، فَإِنْ تَوَضَّأْنَا بِهِ عَطِشْنَا، أَفَنَتَوَضَّأُ مِنَ الْبَحْرِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «هُوَ الطَّهُورُ مَاؤُهُ، الحِلُّ مَيْتَتُهُ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sisi tunasafiri Baharini, na tunabeba maji kidogo sana, tukiyatumia kutawadha tunakosa maji ya kunywa, je, tunaweza kutawadha kwa maji ya Bahari? Akasema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Ni safi Maji yake na ni halali mizoga yake".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika sisi tunapanda majahazi Baharini kwa ajili ya uvuvi au safari za kibiashara na mfano wa hayo, na tunabeba katika safari zetu maji kidogo katika maji yanayofaa kunywa, endapo tukiyatumia maji ya kunywa kwa udhu na kuoga basi yatamalizika, na hatutoweza kupata maji ya kunywa, je, inafaa kwetu sisi tutawadhe kwa maji ya Bahari? Akasema rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji ya Bahari: Maji yake ni safi na yanaweza kusafisha kitu kingine; yanafaa kutawadha na kuoga, na ni halali kula vinavyotoka humo kama samaki na nyangumi na vinginevyo hata kama vitapatikana vimekufa na vinaelea juu yake pasina kuvuliwa.

Mafunzo
  1. Mizoga ya wanyama wa baharini ni halali, na makusudio ya mizoga: Ni wale wanyama wa ndani ya bahari waliokufa katika wale waliofia humo miongoni mwa wale ambao hawaishi isipokuwa ndani ya maji.
  2. Kumjibu muulizaji kwa majibu zaidi ya kile alichouliza kwa ajili ya kukamilisha faida.
  3. Maji yakibadilika ladha yake au rangi yake au harufu yake kwa kitu chochote twahara (safi) basi hayo yataendelea kubaki katika utwahara wake madam bado yako katika uhalisia wake, hata kama chumvi yake itazidi au joto lake au baridi yake na mfano wa hivyo.
  4. Maji ya Bahari yanaondoa hadathi kubwa na ndogo, (uchafu usioonekana kama janaba) na yanaondoa najisi iliyojitokeza katika kitu twahara, kama mwili, au nguo, na kinginecho.
Marejeo

سنن أبي داود (1/ 62) (83). سنن الترمذي (1/ 111) (69). سنن النسائي (1/ 50) (59). سنن ابن ماجه (1/ 250) (386). مسند أحمد (12/ 171) (7233). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (1/ 28). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 59). توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 116).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu

عَن عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْمَاءِ وَمَا يَنُوبُهُ مِنَ الدَّوَابِّ وَالسِّبَاعِ، فَقَالَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا كَانَ الْمَاءُ قُلَّتَيْنِ لَمْ يَحْمِلِ الْخَبَثَ».
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maji, na vile vinavyoyaendea kama wanyama wa kawaida na wanyama pori, akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hukumu ya utwahara wa maji ambayo yanazungukiwa na wanyama wafugwao na wanyamapori kwa ajili ya kunywa na mfano wake, akasema rehema na amani ziwe juu yake kuwa: Maji yakifikia kipimo cha pipa mbili kubwa, ambazo zitakuwa na ujazo wa lita (210) basi hayo ni maji mengi hayawezi kunajisika; isipokuwa ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake au harufu.

Mafunzo
  1. Maji yananajisika ikibadilika kwa najisi moja kati ya sifa zake tatu, rangi yake, au ladha yake, au harufu yake, na hadithi imeeleza kwa ujumla na si kwa kuweka kikomo.
  2. Wamekubaliana wanachuoni kuwa maji yakibadilishwa na najisi basi yananajisika moja kwa moja, sawa sawa yawe kidogo au mengi.
Marejeo

سنن أبي داود (1/ 46) (63). سنن الترمذي (1/ 109) (67). سنن النسائي (1/ 46) (52). سنن ابن ماجه (1/ 324) (517). مسند أحمد (8/ 211) (4605). توضيح الأحكام، للبسام (1/ 121). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 67). منحة العلام، لعبد الله الفوزان (1/ 35).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com