Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Visa na hali za Umma uliopita.

Hadithi 3

Kulikuwa na Mfalme mmoja katika wale waliokuwa kabla yenu, na alikuwa na mchawi wake

عَنْ صُهَيْبٍ رَضيَ اللهُ عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "كَانَ مَلِكٌ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ، وَكَانَ لَهُ سَاحِرٌ، فَلَمَّا كَبِرَ، قَالَ لِلْمَلِكِ: إِنِّي قَدْ كَبِرْتُ، فَابْعَثْ إِلَيَّ غُلَامًا أُعَلِّمْهُ السِّحْرَ، فَبَعَثَ إِلَيْهِ غُلَامًا يُعَلِّمُهُ، فَكَانَ فِي طَرِيقِهِ إِذَا سَلَكَ رَاهِبٌ فَقَعَدَ إِلَيْهِ وَسَمِعَ كَلَامَهُ، فَأَعْجَبَهُ، فَكَانَ إِذَا أَتَى السَّاحِرَ مَرَّ بِالرَّاهِبِ وَقَعَدَ إِلَيْهِ، فَإِذَا أَتَى السَّاحِرَ ضَرَبَهُ، فَشَكَا ذَلِكَ إِلَى الرَّاهِبِ، فَقَالَ: إِذَا خَشِيتَ السَّاحِرَ، فَقُلْ: حَبَسَنِي أَهْلِي، وَإِذَا خَشِيتَ أَهْلَكَ فَقُلْ: حَبَسَنِي السَّاحِرُ، فَبَيْنَمَا هُوَ كَذَلِكَ إِذْ أَتَى عَلَى دَابَّةٍ عَظِيمَةٍ قَدْ حَبَسَتِ النَّاسَ، فَقَالَ: الْيَوْمَ أَعْلَمُ آلسَّاحِرُ أَفْضَلُ أَمِ الرَّاهِبُ أَفْضَلُ؟ فَأَخَذَ حَجَرًا، فَقَالَ: اللهُمَّ إِنْ كَانَ أَمْرُ الرَّاهِبِ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ أَمْرِ السَّاحِرِ فَاقْتُلْ هَذِهِ الدَّابَّةَ، حَتَّى يَمْضِيَ النَّاسُ، فَرَمَاهَا فَقَتَلَهَا، وَمَضَى النَّاسُ، فَأَتَى الرَّاهِبَ فَأَخْبَرَهُ، فَقَالَ لَهُ الرَّاهِبُ: أَيْ بُنَيَّ أَنْتَ الْيَوْمَ أَفْضَلُ مِنِّي، قَدْ بَلَغَ مِنْ أَمْرِكَ مَا أَرَى، وَإِنَّكَ سَتُبْتَلَى، فَإِنِ ابْتُلِيتَ فَلَا تَدُلَّ عَلَيَّ، وَكَانَ الْغُلَامُ يُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ، وَيُدَاوِي النَّاسَ مِنْ سَائِرِ الْأَدْوَاءِ، فَسَمِعَ جَلِيسٌ لِلْمَلِكِ كَانَ قَدْ عَمِيَ، فَأَتَاهُ بِهَدَايَا كَثِيرَةٍ، فَقَالَ: مَا هَاهُنَا لَكَ أَجْمَعُ، إِنْ أَنْتَ شَفَيْتَنِي، فَقَالَ: إِنِّي لَا أَشْفِي أَحَدًا إِنَّمَا يَشْفِي اللهُ، فَإِنْ أَنْتَ آمَنْتَ بِاللهِ دَعَوْتُ اللهَ فَشَفَاكَ، فَآمَنَ بِاللهِ فَشَفَاهُ اللهُ، فَأَتَى الْمَلِكَ فَجَلَسَ إِلَيْهِ كَمَا كَانَ يَجْلِسُ، فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ: مَنْ رَدَّ عَلَيْكَ بَصَرَكَ؟ قَالَ: رَبِّي، قَالَ: وَلَكَ رَبٌّ غَيْرِي؟ قَالَ: رَبِّي وَرَبُّكَ اللهُ، فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الْغُلَامِ، فَجِيءَ بِالْغُلَامِ، فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ: أَيْ بُنَيَّ قَدْ بَلَغَ مِنْ سِحْرِكَ مَا تُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ، وَتَفْعَلُ وَتَفْعَلُ، فَقَالَ: إِنِّي لَا أَشْفِي أَحَدًا، إِنَّمَا يَشْفِي اللهُ، فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الرَّاهِبِ، فَجِيءَ بِالرَّاهِبِ، فَقِيلَ لَهُ: ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ، فَأَبَى، فَدَعَا بِالْمِئْشَارِ، فَوَضَعَ الْمِئْشَارَ فِي مَفْرِقِ رَأْسِهِ، فَشَقَّهُ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ، ثُمَّ جِيءَ بِجَلِيسِ الْمَلِكِ فَقِيلَ لَهُ: ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ، فَأَبَى فَوَضَعَ الْمِئْشَارَ فِي مَفْرِقِ رَأْسِهِ، فَشَقَّهُ بِهِ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ، ثُمَّ جِيءَ بِالْغُلَامِ فَقِيلَ لَهُ ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ، فَأَبَى فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أَصْحَابِهِ، فَقَالَ: اذْهَبُوا بِهِ إِلَى جَبَلِ كَذَا وَكَذَا، فَاصْعَدُوا بِهِ الْجَبَلَ، فَإِذَا بَلَغْتُمْ ذُرْوَتَهُ، فَإِنْ رَجَعَ عَنْ دِينِهِ، وَإِلَّا فَاطْرَحُوهُ، فَذَهَبُوا بِهِ فَصَعِدُوا بِهِ الْجَبَلَ، فَقَالَ: اللهُمَّ اكْفِنِيهِمْ بِمَا شِئْتَ، فَرَجَفَ بِهِمِ الْجَبَلُ فَسَقَطُوا، وَجَاءَ يَمْشِي إِلَى الْمَلِكِ، فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ: مَا فَعَلَ أَصْحَابُكَ؟ قَالَ: كَفَانِيهِمُ اللهُ، فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أَصْحَابِهِ، فَقَالَ: اذْهَبُوا بِهِ فَاحْمِلُوهُ فِي قُرْقُورٍ، فَتَوَسَّطُوا بِهِ الْبَحْرَ، فَإِنْ رَجَعَ عَنْ دِينِهِ وَإِلَّا فَاقْذِفُوهُ، فَذَهَبُوا بِهِ، فَقَالَ: اللهُمَّ اكْفِنِيهِمْ بِمَا شِئْتَ، فَانْكَفَأَتْ بِهِمِ السَّفِينَةُ فَغَرِقُوا، وَجَاءَ يَمْشِي إِلَى الْمَلِكِ، فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ: مَا فَعَلَ أَصْحَابُكَ؟ قَالَ: كَفَانِيهِمُ اللهُ، فَقَالَ لِلْمَلِكِ: إِنَّكَ لَسْتَ بِقَاتِلِي حَتَّى تَفْعَلَ مَا آمُرُكَ بِهِ، قَالَ: وَمَا هُوَ؟ قَالَ: تَجْمَعُ النَّاسَ فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ، وَتَصْلُبُنِي عَلَى جِذْعٍ، ثُمَّ خُذْ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتِي، ثُمَّ ضَعِ السَّهْمَ فِي كَبِدِ الْقَوْسِ، ثُمَّ قُلْ: بِاسْمِ اللهِ رَبِّ الْغُلَامِ، ثُمَّ ارْمِنِي، فَإِنَّكَ إِذَا فَعَلْتَ ذَلِكَ قَتَلْتَنِي، فَجَمَعَ النَّاسَ فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ، وَصَلَبَهُ عَلَى جِذْعٍ، ثُمَّ أَخَذَ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتِهِ، ثُمَّ وَضَعَ السَّهْمَ فِي كَبْدِ الْقَوْسِ، ثُمَّ قَالَ: بِاسْمِ اللهِ، رَبِّ الْغُلَامِ، ثُمَّ رَمَاهُ فَوَقَعَ السَّهْمُ فِي صُدْغِهِ، فَوَضَعَ يَدَهُ فِي صُدْغِهِ فِي مَوْضِعِ السَّهْمِ فَمَاتَ، فَقَالَ النَّاسُ: آمَنَّا بِرَبِّ الْغُلَامِ، آمَنَّا بِرَبِّ الْغُلَامِ، آمَنَّا بِرَبِّ الْغُلَامِ، فَأُتِيَ الْمَلِكُ فَقِيلَ لَهُ: أَرَأَيْتَ مَا كُنْتَ تَحْذَرُ؟ قَدْ وَاللهِ نَزَلَ بِكَ حَذَرُكَ، قَدْ آمَنَ النَّاسُ، فَأَمَرَ بِالْأُخْدُودِ فِي أَفْوَاهِ السِّكَكِ، فَخُدَّتْ وَأَضْرَمَ النِّيرَانَ، وَقَالَ: مَنْ لَمْ يَرْجِعْ عَنْ دِينِهِ فَأَحْمُوهُ فِيهَا، أَوْ قِيلَ لَهُ: اقْتَحِمْ، فَفَعَلُوا حَتَّى جَاءَتِ امْرَأَةٌ وَمَعَهَا صَبِيٌّ لَهَا فَتَقَاعَسَتْ أَنْ تَقَعَ فِيهَا، فَقَالَ لَهَا الْغُلَامُ: يَا أُمَّهْ اصْبِرِي فَإِنَّكِ عَلَى الْحَقِّ".
Imepokelewa Kutoka kwa Suhaib -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Kulikuwa na Mfalme mmoja katika wale waliokuwa kabla yenu, na alikuwa na mchawi wake, alipozeeka, akasema kumwambia Mfalme: Hakika mimi nimezeeka, nitumie kijana nitakayemfundisha uchawi, basi akamtumia kijana ili amfundishe, katika njia aliyokuwa akipita kijana huyo kulikuwa na Kasisi basi, siku moja akakaa naye na akasikiliza mazungumzo yake, yakampendeza sana, basi akawa anapokwenda kwa mchawi anapita kwa Kasisi na anakaa kwake, akifika kwa mchawi mchawi anampiga, basi akamlalamikia hilo Kasisi akasema: Ukimuhofia mchawi, basi mwambie nyumbani walinichelewesha, na ukihofia familia yako basi waambie: mchawi alinichelewesha, basi akaendelea katika maisha hayo, mara ghafla alifika mahali akakuta kuna mnyama mkubwa aliyezuia watu kutoka katika shughuli zao, basi akasema: Leo ndio nitajua je, mchawi ndio bora au yule kasisi ndio bora? Akachukua jiwe na akasema: Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa suala la huyu Kasisi ndio linapendeka zaidi kwako basi muuwe mnyama huyu, ili watu waendelee na shughuli zao, basi akampiga, akawa kamuua, na watu wakaendelea na shughuli zao, akawa kamuendea Kasisi akamueleza tukio hilo, mchamungu akasema kumwambia: Ee mwanangu basi leo wewe umekuwa bora kuliko mimi, kwa hakika jambo lako limefikia pazuri kwa namna ninavyoona, na kwa hakika utapewa majaribu, ukipewa mateso yoyote basi usimuonyeshe yeyote mahala nilipo, na kijana yule alikuwa akiponya vipofu na wenye ukoma na akiwaponya watu kutokana na maradhi mbali mbali, akazisikia habari hizo mmoja kati ya jamaa wa Mfalme alikuwa amekwishapofuka, basi akamuendea akiwa na zawadi, na akamwambia: Yote unayoyaona hapa ni zawadi yako endapo utaniponyesha. Akasema: Hakika mimi simponyeshi yeyote bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na endapo utamuamini Mwenyezi Mungu basi nitamuomba Mwenyezi Mungu naye atakuponya, basi yule kipofu akamuamini Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akamponya, basi bwana huyu akaenda kwa Mfalme na akakaa kama alivyokuwa akikaa awali, basi Mfalme kwa mshangao mkubwa akamuuliza: Ni nani aliyekurejeshea macho yako?!! Akasema: Ni Mola wangu Mlezi. Mfalme akasema: Hivi, kwani una mungu mwingine zaidi yangu? Akasema: Mola wangu Mlezi na Mola wako ni Mwenyezi Mungu, akamkamata, na akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza mahali alipo yule kijana, basi yule kijana akakamatwa na akaletwa kwa Mfalme, Mfalme akasema kumwambia: Ee mwanangu hivi uchawi wako umefikia kuponya vipofu na wakoma?, na unafanya mambo kadhaa wa kadhaa?. Akasema: Mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, akamkamata akamtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuonyesha mahali alipo Kasisi, basi akaletwa yule mchamungu, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi Mfalme akaagiza msumeno, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana mpaka upande mmoja wa kiwiliwili chake ukadondoka, kisha akaletwa yule bwana aliyekuwa akikaa pamoja na Mfalme, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana mpaka upande mmoja wa kiwiliwili chake ukadondoka, kisha akaletwa yule kijana, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, basi akamkabidhi kwa kundi la watu wake, akasema: Mpelekeni katika mlima fulani, kisha pandeni naye mlimani, mkifika keleleni, endapo atarejea katika dini yake basi muacheni, asiporejea basi mrusheni chini, basi wakaenda naye, na wakapanda naye mlimani, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi mlima ukawatetemesha na wakaanguka wote, na akarudi kwa Mfalme huku akitembea, Mfalme akasema kumuuliza: Wamefanya nini jamaa zako?! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao. Basi Mfalme akamkabidhi kwa kundi jingine katika watu wake, akasema: Nendeni mkambebe katika mtumbwi, muende naye mpaka mfike naye kati kati ya bahari, basi akikubali kurudi katika dini yake maucheni, asipokubali mtumbukizeni, basi wakaenda naye, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote utakacho, basi ule mtumbwi ukawamwaga baharini, na wakaangamia wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea, Mfalme akasema kumuuliza: Wamefanya nini jamaa zako? Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao, kisha akasema kumwambia Mfalme: Hakika wewe huwezi kuniua mpaka utekeleze ntakachokuamrisha, akasema: Ni kipi hicho? Akasema: Uwakusanye watu katika uwanja mmoja na unitundike juu ya shina la mti, kisha uchukue mshale mmoja katika ala yangu ya mishale, kisha weka mshale kati kati ya upinde, kisha sema: Bismillaah -Naanza kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola Mlezi wa kijana huyu, kisha nirushie, kwani ukifanya hivyo bila sha utaniua, basi Mfalme akawakusanya watu katika uwanja mmoja, na akamtundika yule kijana juu ya shina la mti, kisha akachukua mshale mmoja kutoka katika ala ya mishale yake, kisha akauweka mshale kati kati ya upinde na akasema: Bismillaah -Naanza kurusha kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola Mlezi wa kijana huyu, kisha akamrushia ukamchoma ule mshale kichwani kwake kati ya jicho na sikio, basi yule kijana akashika kwa mkono wake mahali palipochomwa na mshale akawa amefariki, basi watu wote wakasema kwa sauti moja: Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu!. Wapambe wakamfuata Mfalme wakamwambia: Unaona ulichokuwa ukikwepa?! Wallahi limetokea ulilokuwa ukilikwepa, tayari watu wote sasa wameamini! Basi Mfalme akaamrisha kuchimbwa Mahandaki, kati kati ya mitaa, basi yakachimbwa, na akakoka moto mkubwa ndani yake, na akasema: Yeyote ambaye hatorejea katika dini yake, basi mchomeni humo, au mwambieni jitose mwenyewe, basi wanajeshi wake wakafanya hivyo, mpaka akaja mwanamke mmoja akiwa na mtoto wake mchanga, basi mama yule akawa mzito sana kujitosa ndani ya moto ule, basi mwanaye yule mchanga akazungumza kumwambia mama yake: Ewe mama yangu kuwa na subira hakika wewe uko katika haki".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kulikuwa na Mfalme mmoja katika umma zilizopita kabla yetu, na alikuwa na mchawi wake, alipozeeka mchawi, akasema kumwambia Mfalme: Bila shaka mimi nimezeeka, nitumie kijana ili nifundishe uchawi. Basi Mfalme akamtumia kijana ili amfundishe, kukawa katika njia ya kijana anapokwenda kwa mchawi kuna mchamungu, siku moja akakaa kwake na akasikiliza mazungumzo yake, yakampendeza, basi akawa kila anapokwenda kwa mchawi anapita kwa mchamungu anakaa kwake, anapofika kwa mchawi mchawi anampiga kwa sababu ya kuchelewa, akamlalamikia mchamungu kitendo hicho, akasema: Ukimhofia mchawi, basi mwambie: Nyumbani walinichelewesha, na ukihofia watu wako basi waambie: Mchawi alinichelewesha, basi wakati akiendelea kuisha katika maisha hayo, ghafla alifika mahali kulikuwa na mnyama mkubwa sana, aliyekuwa kawazuia watu kuendelea na shughuli zao, akasema: Leo ndio nitajua je, mchawi ndio bora au mchamungu ndio bora? Akachukua jiwe, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa suala la mchamungu linapendeka zaidi kwako kuliko jambo la mchawi basi muuwe mnyama huyu, ili watu waendelee na shughuli zao, akamrushia akamuua, na watu wakaendelea na shughuli zao, akamuendea mchamungu akamueleza, mchamungu akasema: Ee mwanangu wewe leo umekuwa bora kuliko mimi, jambo lako limefikia hapa ninapopaona, na kwa hakika utapewa mitihani, ikitokea umepewa mithani basi usimuoneyshe yeyote hapa nilipo, na wakati huo kijana alikuwa akiponya vipofu na wenye mbaranga, na akiwatibu watu kutokana na maradhi yote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, akasikia taarifa hizi mmoja kati ya jamaa wa Mfalme alikuwa amekwishapofuka, akamuendea akiwa na zawadi nyingi, akasema kumwambia kijana: Zote hizi zilizoko hapa katika zawadi ni kwa ajili yako endapo utaniponya. Akasema: Hakika mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, ikiwa wewe utamuamini Mwenyezi Mungu nitakuombea na atakuponya, basi akamuamini Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akamponya, akamuendea Mfalme, akakaa karibu naye kama alivyokuwa akikaa awali, Mfalme akasema kumwambia: Ni nani aliyekururejeshea macho yako? Akasema: Ni Mola wangu Mlezi, akasema: Hivi una mola mwingine zaidi yangu? Akasema: Mola wangu Mlezi na Mola wako ni Mwenyezi Mungu. Akamchukua na kumtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza kwa yule kijana, akaletwa yule kijana, Mfalme akasema kumwambia: Ee mwanangu, hivi uchawi wako ndio umefikia kiwango cha kuponya vipofu na wenye mbaranga, na unafanya kadhaa wa kadhaa. Akasema: Hakika mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, basi akamchukua akaanza kumtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza kwa yule mchamungu. Akaletwa yule mchamungu, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, akaagiza uletwe msumeno, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana kwa msumeno huo vipande viwili. Kisha akaletwa yule jamaa wa Mfalme, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana kwa msumeno huo vipande viwili. Kisha akaletwa yule kijana, akaambiwa, rudi katika dini yako, akakataa, akamkabidhi kwa wanaume katika jamaa zake, walikuwa kati ya watatu mpaka kumi. Akasema: Nendeni naye mpaka katika mlima kadhaa wa kadhaa, kisha mpandisheni juu ya mlima, mkifikia kileleni, muulizeni, yuko tayari kurudi katika dini yake?, ikiwa atakuwa tayari kurudi basi muacheni, na asipokuwa tayari mtupeni chini, basi wakaenda naye na wakapanda naye juu ya mlima. Akasema yule kijana: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi mlima ukawatetemesha, na ukatikisika mtikisiko mkubwa sana mpaka wakaanguka wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea. Mfalme akasema kumwambia kwa mshangao mkubwa: Jamaa zako wamefanya nini?!! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao. Basi akamkabidhi kwa kundi jingine katika jamaa zake, akasema: Nendeni naye mkambebe katika boti ndogo, kisha nendeni naye mpaka kati kati ya bahari, ikiwa atakuwa tayari kurudi katika dini yake basi muacheni, akikataa basi mtupeni baharini. Basi wakaondoka naye, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi boti ikawapindua wakawa wameangamia wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea. Mfalme akasema: Wamefanya nini jamaa zako?!! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao, kisha akasema kumwambia Mfalme: Hakika wewe huwezi kuniua mpaka ufanye nitakayokuamrisha. Akasema: Ni yapi hayo? Akasema: Uwakusanye watu katika uwanja wa wazi, na unitundike juu ya shina la mti, kisha chukua mshale mmoja kutoka katika ala yangu ya mishale, kisha weka mshale katikati ya upinde, kisha sema: Bismillaah -kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola wa kijana huyu, kisha nirushie, basi ukifanya hivyo bila shaka utaniua, basi akawakusanya watu katika sehemu mmoja, kisha akamtundika juu ya shina la mti, kisha akachukua mshale mmoja katika ala yake, kisha akauweka mshale kati kati ya upinde, kisha akasema: Bismillah -kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola wa kijana huyu, kisha akamrushia, mshale ukamchoma kati ya sikio lake na jicho lake, akaweka mkono wake mahala alipochomwa mshale, na akawa amefariki. Watu wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu, Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu, Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu. Watu wakamfuata Mfalme wakamwambia: Unaona sasa, ulichokuwa ukikihofia? Bila shaka tunamuapa Mwenyezi Mungu kimekutokea ulichokuwa ukikihofia, ambacho ni watu kumfuata kijana huyo, na wote kumuamini Mola wake, akaamrisha Ardhi ipasuliwe mashimo makubwa ya msitatili (pembe nne) kati kati ya njia, na akawasha na kuuchochea moto ndani yake, na akasema: Yeyote ambaye hatorudi katika dini yake basi mtupeni humo, basi wakafanya alichokiamrisha Mfalme, mpaka akaja mwanamke mmoja akiwa na mwanaye mchanga, akasimama, na akabakia hapo na akachukia kuingia katika moto, basi mwanaye akasema kumwambia: Ewe mama yangu vumilia, kwani hakika wewe uko katika haki.

Mafunzo
  1. Hapa kumethibitishwa karama za mawalii (wachamungu), ikiwemo kumuua mnyama mkubwa kwa jinsi alivyorusha yule kijana, na kujibiwa kwa dua za kijana mara mbili, na mtoto mchanga anayenyonya kuzungumza.
  2. Kupata msaada mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Kumebainishwa utukufu wa uvumilivu, na kuwa na msimamo katika dini.
  4. Hekima ya kujifunza mwanzo wa umri; ni kwa sababu kijana mara nyingi huwa mwepesi kuhifadhi kuliko mtu mzima.
  5. Imani ya nguvu ya kijana huyu, na kwamba hakuyumbayumba katika imani yake, na wala hakubadilika.
  6. Mwenyezi Mungu hujibu maombi ya aliyedhikika anapomuomba.
  7. Inafaa kwa mtu kuiangamiza nafsi yake panapokuwa na masilahi ya waislamu wengi, kwa sababu kijana huyu alimuelekeza Mfalme katika jambo ambalo atamuua nalo na kuiangamiza nafsi yake, nalo ni achukue mshale kutoka katika ala yake, na auweke katikati ya upinde na aseme: Bismillaah -kwa jina la Mwenyezi Mungu Mola wa kijana huyu.
  8. Inafaa kusema uongo katika vita na mfano wake, na katika kuinusuru nafsi na maangamivu.
  9. Muumini hupimwa katika ukweli wa imani yake na kuwa na msimamo katika kauli ya haki, hata kama jambo litafikia katika kuiangamiza nafsi yake.
  10. Kujitoa muhanga katika njia ya kufikisha ujumbe wa kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu na kuidhihirisha haki.
  11. Nyoyo za waja ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu anamuongoza amtakaye na anampoteza amtakaye, kwani kijana aliongoka wakati ambao alikuwa katika malezi ya uchawi na chini ya usimamizi wa nguvu wa Mfalme.
  12. Inafaa mja kumuomba Mwenyezi Mungu amuonyeshe alama za kuijua kweli ili apate yakini (imani ya uhakika)
  13. Waumini hudhalilishwa kwa yote aliyowapa Mwenyezi Mungu na kuwafanya kuwa bora kwa ajili ya kuitumikia dini yake na kuwaita watu kwayo.
  14. Sababu za kuangamia ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu, akitaka anazipitisha, na akitaka anazikata.
  15. Makafiri huwa hawapungukiwi na hoja na dalili za kuwafanya waamini, bali sababu ya ukafiri wao ni ukaidi na kiburi.
  16. Matwaghuti (mashetani) na madhalimu huwa wamejipanga kuuwa watu wote ili wabakie katika maisha waliyonayo, ikiwemo kuneemeka katika dunia.
  17. Mwenyezi Mungu huwaadhibu waliodhulumu kwa namna ambavyo hawakutarajia, kwani watu wote walimuamini Mola wa kijana yule, walipoona msimamo wake, na ukweli wake na ulinganizi wake, na kutokuogopa kwake katika jambo la Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumu.
  18. Wako ambao waliozungumza katika mbeleko wakiwa wachanga tofauti na Masihi amani iwe juu yake, na hadithi hii, ndio inafafanua kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hawakuzungumza katika mbeleko isipokuwa watatu...", na akawataja, na wote akawaweka kwa wana wa Israel na si wengineo.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2299) (3005). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 86). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص39). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 412). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 210). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 62).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «ما نهيتكم عنه فاجتنبوه، وما أمرتكم به فأْتُوا منه ما استطعتم، فإنما أَهلَكَ الذين من قبلكم كثرةُ مسائلهم واختلافهم على أنبيائهم».
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ametuelekeza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake yakwamba yeye anapotukataza kitu ni wajibu kwetu kukiepuka bila kubagua, na akituamrisha chochote ni juu yetu kukifanya kwa kadiri tuwezavyo. Kisha akatutahadharisha ili tusijekuwa kama umma zilizotangulia pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao pamoja nakwenda kwao kinyume nao, akawaadhibu Mwenyezi Mungu kwa aina mbalimbali za maangamivu na adhabu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.

Mafunzo
  1. Amri ya kutekeleza maamrisho, na kuyaepuka makatazo.
  2. Katazo halikuruhusu kufanya kitu chochote miongoni mwa hivyo, na amri ikawekewa sharti la kuweza; kwasababu kuacha ni jambo linawezekana na kufanya ni jambo linahitaji uwezo wa kukileta kitendo kilichoamrishwa.
  3. Katazo la kukithirisha maswali, wameyagawanya wanachuoni maswali katika sehemu mbili: Ya kwanza: Ni yale yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza katika mambo yanayohitajika miongoni mwa mambo ya dini, haya yameamrishwa, na miongoni mwa hayo ni maswali ya maswahaba. Na ya pili: Ni yale yanayokuwa katika mfumo wa ukaidi na kulazimisha, na haya ndiyo yaliyokatazwa.
  4. Kutahadharishwa umma huu na kutokwenda kinyume na Nabii wake, kama ilivyotokea katika umma zilizokuwa kabla yake.
  5. Katazo lake linajumuisha kidogo na kingi, kwasababu haiwezi kufikia kuyaepuka makatazo ispokuwa kwa kuyaepuka yale madogo na mengi, kwa mfano: Ametukataza kula riba, katazo linajumuisha kidogo na kingi.
  6. Kuziacha sababu zote zinazopelekea katika mambo ya haramu, kwasababu kufanya hivyo ni miongoni mwa maana za kuyaepuka.
  7. Mwanadamu ana nguvu na uwezo, kwa kauli yake: "Kwa kiasi muwezavyo" ndani ya kauli hii ni jibu la madhehebu ya Jabariyya wanaosema kuwa: mwanadamu hana uwezo, kwasababu yeye amelazimishwa juu ya matendo yake, hata pale mtu anapotikisa mkono wake wakati wa mazungumzo, wanasema kutikisa mkono huku si kwa uwezo wake, bali kalazimishwa, na hakuna shaka kuwa kauli hii ni batili na inaambatana na madhara makubwa.
  8. Haitakiwi kwa mwanadamu anaposikia amri ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake aseme: Kwani hiyo ni wajibu au ni sunna? kwa kauli yake: "Lifanyeni kwa kadiri muwezavyo".
  9. Yote aliyoyaamrisha Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- au akayakataza basi hiyo ni sheria, swasawa hilo liwe ndani ya Qur'ani au lisiwemo, itafanyiwa kazi sunna ya ziyada katika Qu'r'ani iwe amri au katazo.
  10. Kukithirisha maswali ni sababu ya kuangamia, hasa hasa katika mambo ambayo haiwezekani kuyafikia, mfano kama maswala ya ghaibu kama majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake, na hali za siku ya kiyama, usikithirishe maswali ndani yake ukaangamia, ukawa ni mtu mwenye kulazimisha mambo mwenye kujikita.
  11. Umma waliotangulia waliangamia kwa kukithiri maswali yao, na waliangamia kwa kukithiri kwenda kwao kinyume na Manabii wao.
Marejeo

-التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، مطبعة دار نشر الثقافة، الإسكندرية، الطبعة: الأولى، 1380 هـ. -شرح الأربعين النووية، للشيخ ابن عثيمين، دار الثريا للنشر. -فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، دار ابن القيم، الدمام المملكة العربية السعودية، الطبعة: الأولى، 1424هـ/2003م. -الفوائد المستنبطة من الأربعين النووية، للشيخ عبد الرحمن البراك، دار التوحيد للنشر، الرياض. -شرح الأربعين النووية، للشيخ صالح آل الشيخ، دار الحجاز، الطبعة: الثانية، 1433هـ. -الأربعون النووية وتتمتها رواية ودراية، للشيخ خالد الدبيخي، ط. مدار الوطن. -الجامع في شروح الأربعين النووية، للشيخ محمد يسري، ط. دار اليسر. -صحيح البخاري، نشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ. -صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، نشر: دار إحياء التراث العربي – بيروت.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri

عَنْ أَبِي حَازِمٍ قَالَ: قَاعَدْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ رضي الله عنه خَمْسَ سِنِينَ، فَسَمِعْتُهُ يُحَدِّثُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: «كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لاَ نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ» قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّلِ فَالأَوَّلِ، أَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ، فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ».
Kutoka kwa Abuu Haazim amesema: Nilikaa karibu na Abuu Huraira kwa muda wa miaka hamsini, nikamsikia akihadithia kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema: "Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri" Wakasema: Unatuamrisha nini? Akasema: "Timizeni ahadi ya utiifu ya moja baada ya nyingine, wapeni haki zao, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza walikuongozeni vipi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa wana wa Israeli walikuwa wakiongozwa na Manabii, na wakisimamia mambo yao kama wanavyofanya viongozi na watawala kwa raia, kila unapodhihiri ufisadi Mwenyezi Mungu anawatumia Nabii kwa ajili ya kunyoosha mambo yao na kuondoa yale waliyoyabadilisha katika hukumu. Na hakika hakuna Nabii baada yangu ili afanye kama waliyokuwa wakiyafanya wale, na watakuja baada yangu watawala, na watakuwa wengi, na utatokea mzozano na kuhitilafiana baina yao. Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao wakamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Unatuamrisha tufanye nini? Akasema: Atakapochaguliwa kiongozi baada ya kiongozi; uteuzi wa kiongozi wa kwanza ndio uteuzi sahihi na ni wajibu kuutimiza na kuuheshimu, na uteuzi wa pili ni batili na ni haramu kwake kuukataa, na wapeni haki zao, na muwatii na muishi nao kwa usikivu na utii isipokuwa katika maasi, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza na atawahesabu kwa yale wanayokufanyieni.

Mafunzo
  1. Nikuwa ni lazima kwa raia kuwa na nabii au kiongozi mwenye kusimamia mambo yao, na mwenye kuwapeleka katika njia iliyonyooka.
  2. Nikuwa hakuna nabii baada ya Nabii wetu Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Tahadhari ya kujitoa kwa yule ambaye umethibiti uongozi wake kwa njia ya kisheria.
  4. Haifai kuweka makubaliano ya kuwachagua viongozi wawili kwa wakati mmoja.
  5. Ukubwa wa majukumu ya uongozi, kwa sababu Mwenyezi Mungu atamuuliza kuhusu raia wake.
  6. Amesema bin Hajari: Kutanguliza jambo la dini kuliko jambo la dunia; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliamrisha kutimiza haki ya kiongozi kwakuwa ndani yake kuna kuipa nguvu dini na kuzuia fitina na shari; na kuchelewesha swala kudai haki yake haina maana ya kuidondosha, na Mwenyezi Mungu alimuahidi kuwa yeye mwenyewe atamlipa na atamtimizia hata kama ni huko Akhera.
  7. Alama miongoni mwa alama za unabii wake rehema na amani ziwe juu yake, hakika walikithiri viongozi baada yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umma ukaongozwa na waliokuja kutengeneza miongoni mwao na walioharibu.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 169) (3455). صحيح مسلم (3/ 1471) (1842). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 707). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 544).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com